Hivi ni sawa hili la kuhubiri ndani ya mabasi ya umma?

Hivi ni sawa hili la kuhubiri ndani ya mabasi ya umma?

Siku nitamkata mitama mmoja ndio watashika adabu,
Wanakera sana hawajui tu..
 
Kuna mwaka fulani nilisafiri kipindi cha Pasaka, basi nililopanda wakaweka mawaidha ya dini ya kiislamu, ikawa muda wote ni kuponda ukristo na hiyo sikukuu ya Pasaka.

Ile safari ilikuwa ndefu balaa, na hakuna hata mmoja aliyeweza kumwomba dreva abadili, dreva na kondakta wote wamefuga ndevu.
Yashatukuta siku moja tunaenda mkoa nilikaa na mshikaji wangu mhuni hivi akawaambia wabadili wakakataa kukawa na mabishano adi wakaleta dharau kama tunaona kero tushuke.....
Sababu tulikua siti ya nyuma ya dereva tukaambiana akisimama penye trafiki tunamchoma na kweli tukafanya hivyo trafiki kaingia kwa gari kauliza abiria karibu wote tukaungana akala cheti fasta.
 
Wanaboa kinyama,nilishawahi kushuka kituo sio changu sababu ya huo upuuzi

Nikiwa na earphones naeka na mziki hadi mwisho
Hata uweke musikii hadi mwisho momiree..injili utaipata tuu..iwe danguroni..baani..chooni..everywhere
 
Hata uweke musikii hadi mwisho momiree..injili utaipata tuu..iwe danguroni..baani..chooni..everywhere
Ktk mahubiri mazingira yanahusika ndg yng,,,,,kitu kikifanyia sehemu isiyo mahali pake kinakuwa hakina maana.
 
Ukiona Injili inahubiriwa (mahali popote) wewe ukawa unajisikia vibaya, jua kuwa wewe ni wa baba yenu Ibilisi.

Bwana Yesu alishawahi kuwaambia watu flani "Ninyi ni wa baba yenu ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya ... " YOHANA 8:44

hakika YESU ni Mwokozi.
 
Wadau naomba kuzungumzia kuna hili jambo kwa sasa limezidi kushika kasi kuhubiri ndani ya daladala imekuwa sehemu nyingi hasa mabasi ya Tegeta toka mjini yaaani mnakosa utulivu kwenye mabasi na mwisho wa siku wanachangisha sadaka sasa najiuliza hii hali vipi wadau
Kinachokukera zaidi ni sadaka? Au ni neno la Mungu ?
 
Injili ni muhimu sana kwa wote

Ila kwa taarifa fupi tuu ni kwamba sio wote wana nia njema

Bali wengine mule ni wachawi,wapigaji/matapeli

Itoshe kusema Dunia hii ina makubwa kuliko uyajuayo
 
Kwa upande wangu siyo kosa kuhubiri sehemu yoyote ila lazima utaratibu uzingatiwe tu.

Ila wanachonichosha wake jamaa mtu akiwachallange kwamba hawapaswi kuhubiri sehemu hiyo wanakasirika na kuanza kumuita mtu huyo mchawi au anamapepo na hapa wanakuwa wanaharibu Sana kwasababu umenikuta nimekaa kwenye usafiri na ninalipia then unakuja kuniambia mchawi au nina mapepo. Huu siyo ustaarabu kabisa

Wanapoenda kwenye vyombo vya usafiri wajue kabisa kwamba watakutana na mawazo tofauti na watu wenye Imani tofauti, so wanatakiwa kuwa na majibu ya maswali wanayoulizwa badala ya kuanza kutukana watu ambao wamelipia nauli ili kusafiri.

Mathayo 24:14
 
Ktk mahubiri mazingira yanahusika ndg yng,,,,,kitu kikifanyia sehemu isiyo mahali pake kinakuwa hakina maana.
Kwa kuwa neno linasema injili itahubiriwa kote, hivyo mahali popote, kwa wakati usiofaa na ufaao, injili lazima ihubiriwe mana ni habari njema.
Hivyo MUNGU hapangiwi sehemu ya kunena wala kuonya popote pale neno litafika.
 
Hii injili au uharamia sasa?
Ni injili mkuu..
Mahali popote neno lazima lifike yaan hakuna namna..
Makanisani watu hawajii..kwenye mikutano ya injili watu hawafiki kwa kuwa maisha yamekuwa changamoto watu hawalali ni kutafuta pesa kwa ajili ya tumbo hivyo wanapokuwa kwenye utafutaji tutahakikisha injili inawafikia mana tukisubir jpl waje hawaji tukiweka mikutano ya injili hawaji..
Hivyo tutawafuata huko huko kwenye shughuli zao.
enendeni ulimwenguni kote mkawabitize watu kwa jina la BABA , MWANA NA ROHO MTAKATIFU.
 
Mahali popote?

Peleka Injili Maka uone.
 
Usikwazike mkuu hao ni masikini tu wanaojitutumua na ufalme wao wa mabox.
 
Mahali popote?

Peleka Injili Maka uone.
Heee..maka tena..mbona makanisa yapo kiongozi..hahaha..kumbe hujui fuatilia kwa ukaribu wachana na propaganda za facebook, instagram, twiter na JF..watu wanasali vizuri tu jpil..
Ukiona jambo linapingwa ujue linanguvu kubwa fuatilia utagundua
 
Kuna makanisa Maka? Maka ya wapi, Saudi Arabia au nyingine mmeichonga ya maigizo?

Wewe unaelewa kwamba mimi huwa sitaji kitu bila research?

Unaweza kuyataja hayo makanisa haliyopo Maka?

Weka link hapa tuyajue.
 
Hiyo link uliyonipa wewe mwenyewe inasema hivi.

"Churches
Currently there are no official churches in Saudi Arabia of any Christian denomination.[8] The small number of Christians in Saudi Arabia meet in internet chat rooms and private meetings.[8]

According to the Society of Architectural Heritage Protection Jeddah and the Municipality of Jeddah, a long-abandoned house in Al-Baghdadiyya district has never been an Anglican church, contrary to the "'myth' that had spread on the Internet". However, in 1930 there was a non-Muslim cemetery in Jeddah.[13]"

Hakuna sehemu ilipoandikwa kwamba kuna kanisa Maka hapo.

Nendeni kajengeni kanisa Maka muone utamu wa jambia.
 
Niliwahi kuhoji dhana ya Mtumishi mmoja wa Mungu kupeleka injili kwenye jamii ya wafugaji ambayo walikuwa hawaihitji. Matokeo yake eti wakawa wanampiga mpaka wapigaji wanazimia. Sasa unapelekaje kitu kule ambako hakihitajiki na wakati kuna sehemu zingine nyingi tu ambazo hazina kitu kile kile, na zinakihitaji?
 
Back
Top Bottom