Hivi ni Taasisi yetu tu au Taasisi zote za Umma pesa imekua ngumu kwa Wafanyakazi?

Hivi ni Taasisi yetu tu au Taasisi zote za Umma pesa imekua ngumu kwa Wafanyakazi?

Wakuu, especially waajiriwa wa serikali.

Hivi Na nyie ofisini kwenu pakavu kama kwetu au ofisi yetu ndio imekua mfano? Maana kusema kweli 2023 na 2024 hii miaka imekua migumu sana.

Posho hazitoki yapo madeni tu tokea ya September 2023, safari imekua kitu hadimu, vikao vya hela hamna wala kazi za masaa za ziada hazilipwi.

Okay, sasa sijui pesa ipo wengine tunabaniwa tuliopo chini au Taasisi zote sahivi zimebaniwa hela?

Nimechoka kushinda kwenye uzi wa Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Mliojiajiri karibuni kunitukana!
Mambo ni magumu japo sio kote
 
Kaka we acha tu! Unafahamu ile clip bibi mmoja anasema “We niache tu nachanganyikiwa mjukuu wangu “

😂

Kazi ni mpaka wa akili yako, hadi ufukuzwe kazi ndio utambue kipaji chako
Mshahara umejaa makato, biashara zimejaa mapato...

Nikweli, wanasema ukitaka kupata utamu wa juice ya chungwa, likamue sana.

Kuna mazingira mfano hiyo kufukuzwa kazi inakufanya utumiwe akili na maarifa yako yote uweze kukabiliana na changamoto za maisha.
 
😅😅😅😅😅 pole ndiyo ukubwa huo, unakumbuka wazazi wako, ukiwa mdogo. Ukiomba hela, wanasema hawana ndiyo hivi 😊😊😊
By the way, Taasisi gani hiyo imefulia hivyo?
Hii ndio ila maana ya maneno,kua uyaone mwanangu.
 
.

Ni vizuri sana kuwa na ndoto, jitihada, bidii, maarifa na kila aina ya ubunifu kwenye kutafuta pesa, ila hakikisha afya yako, furaha yako, amani yako na uhuru wako hauathiriki kwa namna yeyote ile, hapo sijaongelea heshima yako.
Ume nikumbusha marehemu mzee wangu, nili kuwa niki mtembelea tuna kula bata Sana.

siku akiwa hayuko vizuri, ana sema jembe langu Leo mfuko ume azimwa.
Ila haimaanishi hatu wezi kufurahi.
haya nenda Buchani au supermarket, kalete hiki na kile tuishi.

hapo mta weka movies, story za hapa na pale. Jioni ume pewa 10k maisha yaka enda.

Ali wahi sema "familia ndo kila kitu, kukosa hela sio kigezo Cha kuto kufurahi na kuishi.
 
Back
Top Bottom