Hivi ni vifaa muhimu kuwa navyo nyumbani kwako

Hivi ni vifaa muhimu kuwa navyo nyumbani kwako

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
6,699
Reaction score
9,323
Nyumbani kwako ni muhimu uwe na vifaa hivi, kwani vinahitajika sana.
1.Star screw drivers kubwa na ndigo
2.Flatted screw drivers ndogo na kubwa
3.Tester ya umeme
4.Plier au plaiz
5.Nyundo
6.msumeno wa mbao
7.msumeno wa chuma
8.tupa inanolea vifaa vya chuma.
9.Futi
10.Jembe
11.Panga
12.Koleo
13.Shoka
14.Star na flatbed screws
15.Waya wa umeme japo mita 10
16.Spana ya kufungulia vifaa vya mabomba.

Hivyo vifaa uviweke kwa mpangilio wake na mwenza wako awe anajua. Kuna dharura inaweza kutokea na fundi akaja lakini akawa hana vifaa vyote,akikuulizia vifaa hivyo unampa.

Utafurahia sana maisha maana kila dosari ikitokea itarekebishwa haraka.Na mara zote fundi akija jitahidi kuwa karibu yake kwenye kila kazi utakayompa ili uwe unajua dosari kadhaa wa kadhaa na namna ya kuzitatua.

Mimi ndivyo navyoishi hapa kwangu ni kila kila aina ya vifaa na mafundi wakija kurekebisha kazi,huniuliza baba kuna kifaa hiki au kile nawaambia kipo nawaletea na kazi inafanyika.

Hivi sasa mafundi wajenzi,mafundi umeme,mafundi wa magrili na mafundi wa aluminiamu wote ni rafiki zangu na wengi huniita baba,na wanapofanya kazi hata kwa majirani wakipungukiwa vifaa huja kwangu nami nawapa.Hivyo na wewe usomae hili bandiko iga mfano huu
 
1774677029313.jpeg
 
sijaona ngazi hapo
Ni kweli ngazi ni muhimu sana,sasa hapa naongezea vifaa vifuatavyo:
1.ngazi,hii ni kila mtu na uwezo wake kuna zile za kununua au za kutengeneza ama za mbao au chuma na ukijiweza uwe nazo 2,moja ndefu na moja ya wastani.Mimi ninazo 2 moja ya kutengeneza ni ndefu na moja ya kununua ni fupi.
2.Kompyuta na printa yake.Mimi ninayo desktop na hp printa ila kwa vijana wa sasa wana laptop au simu zenye uwezo wa bluetooth na printa yenye bluetooth hivyo zinafanya kazi vizuri tu.
3.Uwe na panchi ya kutoboa makaratasi na staple machine.
4.vifaa vya umeme: wireless multi plug na plug ambayo pia ina uwezo wa kuchaji simu
 
Wewe jamaa au ulipita jana jioni ukasikia mazungumzo yangu na mke wangu nini? Haiwezekani ugonge mulemule nilimokuwa namwambia mke wangu (ingawa kwako vimeongezeka vingine ambavyo sikuviwaza hata)

Kwa sisi wa vijijini inabidi kuongezea hapo
Fyekeo
Kibao cha nazi
Flampeni
Sufuria kubwa
Kinu na mchi
Reki
Misumari kadhaa
Tochi safi
Manati
Kalamu
Karatasi
Chepe(beleshi)

Iko hivi...
Jana jioni wife almanusura ashindwe kupika chakula alichokusudia kisa eti frying pan aliazimisha kwa jirani na jirani alitoka. Basi nikawa namwambia kuna vitu muhimu kuwepo ndani inabidi ukikaa na mashoga zako uwaambie wanunue hii mambo ya kuombaomba/kuazima ni mambo ya zamani. Zamani vitu hivyo ilikuwa ni nadra sana kutumika na ndiyo maana wakaazimana bila tabu lakini kwa sasa ni muhali
 
Uzee nao shida,nilikuwa nakagua hapa nyumbani nimekuta vitu hivi ni muhimu sana:
1.spiriti , pamba na bandeji
2.mkasi kwa kukata nguo au karatasi
3.sindano ya kushonea nguo na uzi wake
 
Wewe jamaa au ulipita jana jioni ukasikia mazungumzo yangu na mke wangu nini? Haiwezekani ugonge mulemule nilimokuwa namwambia mke wangu (ingawa kwako vimeongezeka vingine ambavyo sikuviwaza hata)

Kwa sisi wa vijijini inabidi kuongezea hapo
Fyekeo
Kibao cha nazi
Flampeni
Sufuria kubwa
Kinu na mchi
Reki
Misumari kadhaa
Tochi safi
Manati
Kalamu
Karatasi
Chepe(beleshi)

Iko hivi...
Jana jioni wife almanusura ashindwe kupika chakula alichokusudia kisa eti frying pan aliazimisha kwa jirani na jirani alitoka. Basi nikawa namwambia kuna vitu muhimu kuwepo ndani inabidi ukikaa na mashoga zako uwaambie wanunue hii mambo ya kuombaomba/kuazima ni mambo ya zamani. Zamani vitu hivyo ilikuwa ni nadra sana kutumika na ndiyo maana wakaazimana bila tabu lakini kwa sasa ni muhali
Hapana sijasikia kitu ila mimi vifaa vya upushi sikuwa na wazo navyo ila umeongezea kitu muhimu ni tochi
 
Back
Top Bottom