Hivi ni vifaa muhimu kuwa navyo nyumbani kwako

Hivi ni vifaa muhimu kuwa navyo nyumbani kwako

Kuna rika letu flani hivi kufunga na kufungua vitu ilikuwa kawaida sana, tulianzia kwenye radio tape cassette pale mkanda unapoliwa au kujigeuza, unafungua unarekebisha unafunga, tukaja kwenye redio yenyewe, mambo ya capacitor, conductor, mota, baadae sakiti nzima, leo hii kabla sijapeleka mzigo kwa fundi lazima nifanye uchunguzi wa awali, (diagnosis), unaweza ukakuta tatizo ni fuse tu imeungua ama cable imekatika umeme haufiki, matatizo madogo madogo unamalizana nayo we mwenyewe kama mwanaume.😃, na hapo sikuwa nimesomea fizikia😃
 
Vifaa karibia vyote ninavyo, bado kwenda veta tu🤔
 
Hpo inabidi uongeze vingine vi nne muhimu.
- kadi ya ccm.

-kadi ya chadema.

-kadi ya simba.

-kadi ya yanga
 
Nyumbani kwako ni muhimu uwe na vifaa hivi, kwani vinahitajika sana.
1.Star screw drivers kubwa na ndigo
2.Flatted screw drivers ndogo na kubwa
3.Tester ya umeme
4.Plier au plaiz
5.Nyundo
6.msumeno wa mbao
7.msumeno wa chuma
8.tupa inanolea vifaa vya chuma.
9.Futi
10.Jembe
11.Panga
12.Koleo
13.Shoka
14.Star na flatbed screws
15.Waya wa umeme japo mita 10
16.Spana ya kufungulia vifaa vya mabomba.

Hivyo vifaa uviweke kwa mpangilio wake na mwenza wako awe anajua. Kuna dharura inaweza kutokea na fundi akaja lakini akawa hana vifaa vyote,akikuulizia vifaa hivyo unampa.

Utafurahia sana maisha maana kila dosari ikitokea itarekebishwa haraka.Na mara zote fundi akija jitahidi kuwa karibu yake kwenye kila kazi utakayompa ili uwe unajua dosari kadhaa wa kadhaa na namna ya kuzitatua.

Mimi ndivyo navyoishi hapa kwangu ni kila kila aina ya vifaa na mafundi wakija kurekebisha kazi,huniuliza baba kuna kifaa hiki au kile nawaambia kipo nawaletea na kazi inafanyika.

Hivi sasa mafundi wajenzi,mafundi umeme,mafundi wa magrili na mafundi wa aluminiamu wote ni rafiki zangu na wengi huniita baba,na wanapofanya kazi hata kwa majirani wakipungukiwa vifaa huja kwangu nami nawapa.Hivyo na wewe usomae hili bandiko iga mfano huu
Leo nimeongeza kifaa hiki ni wire stripper,hiki kinafanya kazi nyingi sana,kuchuna waya,kubana waya kwenye holder zake.Na kwa wiki nzima nilikuwa najifunza kufungabtaa za umeme
 

Attachments

  • IMG20260506113923.jpg
    IMG20260506113923.jpg
    339.8 KB · Views: 5
Back
Top Bottom