Hivi nyie mnaobeza na kukandia 'watoto wa 2000s' mna hoja au ni wivu tu na maslahi binafsi?

Hivi nyie mnaobeza na kukandia 'watoto wa 2000s' mna hoja au ni wivu tu na maslahi binafsi?

Wazazi wao walizaliwa 60s, 70s na early 80s. Tuseme nao wa hovyo tu, yaani kama vitoto vya 2000s ni vya hovyo, hilo ni zao la wazee wao.

Miaka ya 2000s ndio arv zimekuja kwa kasi kupunguza vifo vya aids, uzazi wa mpango umeshika kasi, y2k na mambo yake mengi.
Watoto wengi wa 2000s hawana ugumu wa kuanza maisha na kupiga hatua, sio kama wazazi wao ambao kabla ujenge nyumba yako ilibidi ujengee wazazi wako kwanza.
 
Kupakatwa wameanza zamani tu, tena si ajabu mifano yooote unayoijua hakuna wa 2000s..... bado naamini ni chuki na wivu tu.

Suala la kumiliki gari na kujenga ni basic needs, wala haipaswi kuwa gumu kwa umri wowote.... zamani mlikuwa na vitisho ndivyo vimewachelewesha wengi.
Mkuu au na wewe mtoto wa 2000s husomi kwa uelewa!??
Embu nirudie maelezo soma kwa makini.
Kwanza nikuweke sawa,sijasema kama kupakatwa wameanza sasa hivi laa hasha.
Vijana wa sasa hivi wanataka mambo makubwa pasi na KUJISHUGHULISHA.
Unaweza ukamkuta akakwambia nataka gari nzuri,nyumba nzuri na pesa,ila ukimuuliza una mipango gani ya kutimiza hivyo vyote,jibu hana anakaa kushangaa tu.
Ndio maana nikakwambia kuna uamko wa kupambana ufanikiwe mapema na kuna mihemko ya kutaka ufanikiwe mapema.
Uamko utakufanya ujenge mikakati na upambane kijuhudi na kiakili.
Ila mihemko itakufanya utake vitu kwa pupa pasi na kujua unavipata kwa mikakati ipi,hivyo hiyo hupelekea kufanya hata vitu visivyotakiwa kufanywa ili ufanikiwe.
Ndio maana nikasema vijana wa siku hizi kupakatwa ni kitu rahisi sana ili afanikishe yake.
Hata mabinti wamekua ni wakujiuza sana mapenzi kwao ni pesa kama una pesa atakupa chochote kile.
Ndio maana mabinti wa siku hizi wanachezeleka sana.
Embu fuatilia kipindi cha nyuma na sasa kipindi kipi ushoga umezidi kama sio sasa hivi!?
Vijana wa sasa hivi walaini laini sana kimwili na kiakili.

Nakusisitiza mkuu,kuna uamko wa kufanikiwa na kuna mihemko ya kufanikiwa.
Vijana wa siku hizi wana mihemko.
Kama hujanielewa hapa mkuu SHIKAMOOOOO pia mimi wala sio mkubwa ni wa 1990s.
 
Love Hujawahi kutana na twakike twa 2000's utupe mwongozo??😊🤔🤔🤔!

Nasikia ni noumaaa narobotatu
😂😂😂Sikuwahi kuku quote dada ila leo imenibidi.
Kudate visichana vya 2000s aisee uwe na uvumilivu,ustahamilivu,ujasiri,busara na hekima ya hali ya juu.
 
Sio wivu ila hawana akili....
Yaani hawana akili aiseee
Screenshot_20240406_104459.JPG
 
😂😂😂Sikuwahi kuku quote dada ila leo imenibidi.
Kudate visichana vya 2000s aisee uwe na uvumilivu,ustahamilivu,ujasiri,busara na hekima ya hali ya juu.

Asante sana kwa mwongozo! Kwa kifupi vya 2000's ni changamoto sana japo viko vyedi vinaita!


Smart911 love bakinamimibabee😁🤭
 
Wenyewe wanajiita Gen Z mara Gen Z Baddie😂😂😂

Eniwei tuendelee kupambana
 
Ni watoto wa Faraoh!

Watoto wa 2000 wanavaa visendo manyoya

Hawaogopi UKIMWI

Changamoto kuwa nao kwenye mahusiano

Wengi wanaonekana wazee kuliko wa 90s na 80s.

Wadudu wa Arusha nao ni wa 2000
 
Aaah yamenifika hapa!















Nahisi hii ni vita kali na wengi wetu tunaingizwa mkumbo tu, wekeni sababu za msingi hapa tuone.















Mimi rasmi simo kwenye huo upotoshaji, kama kuna sehemu niliwahi kunukuliwa basi nasema nilikuwa nimelewa au nilishinikizwa.















Puuzeni kauli hiyo na mnisamehe bure, nimezaliwa upya.















Ncha KSaali.







Kutoka kwa kaboo snoop



Kutoka kwa kaboo snoop
 
Aaah yamenifika hapa!

Nahisi hii ni vita kali na wengi wetu tunaingizwa mkumbo tu, wekeni sababu za msingi hapa tuone.

Mimi rasmi simo kwenye huo upotoshaji, kama kuna sehemu niliwahi kunukuliwa basi nasema nilikuwa nimelewa au nilishinikizwa.

Puuzeni kauli hiyo na mnisamehe bure, nimezaliwa upya.

Ncha Kali.
Leejay49 njoo uwape mwongozo hawa mama!
 
Inafikia mahala sasa nieleweshwe hili jambo. Hao watoto wa 2000's wazazi wao hasa ni akina nani?

Sio hao hao wanaoona shule bora za kuwapeleka ni hizo saint kufanyaje huku mkiwaita akina junia? Au wazazi wao ni wa nje ya dunia hii!???
 
Hawa watoto hawajui jinsi gani tumechapwa kwa cassete ya msondo kukwama kwenye redio..
Au singi kurudi umeme umekata VHS imekwama kwenye deki tuacheni tuu.. watoto wa 2000 mkipunguza ujuaji itakuwa sawa..
Cc min -me nawenzakoo kina cacutee
 
Back
Top Bottom