Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Wakuu, achaneni na mambo ya siasa na uchumi, njoeni hapa pande za ChitChat tupige story za ukweli.
Leo nataka tuongee kuhusu hawa viumbe wa ajabu wanaoitwa "Vibenten" na "Mamarioo." Nitaongea lugha kipimo chao.. Nisamehewe😂
Hivi nyie wavulana wa hovyo mna akili timamu kweli au mmerogwa na hawa Mashugamami wa mjini? Maana sio kwa uvivu huu na kupenda mteremko kulikopitiliza!
Kijana una nguvu zako, dume zima, lakini ratiba yako ya siku nzima ni kama mrembo anayejiandaa kwenda kwenye harusi.
Asubuhi upo saluni unafanya scrubbing ya uso na kucha, mchana unaenda gym kubeba chuma ili kutengeneza six packs!
kisa unajiandaa kwenda kuliwaza "shugamami" lako jioni.
Unahongwa ka-IST au ka-Vitz chakavu na bando la chuo, basi unajiona umeyapatia maisha na kuanza dharau mtaani.
Hivi huo si ni ukichaa?.
Ujinga wenu mkubwa ni kudhani kuwa hiyo miili yenu laini haitochoka. Hamjui kuwa ujana ni moshi na unakata chap?
Subiri uanze kuota mvi, uzeeke, au nguvu zako za kiume zianze kusuasua uone cha mtema kuni.
Huyo mama atakupiga chini kama nguo ya deki na kuchukua kibenten kingine kipya chenye pumzi ya moto na nguvu za transformer.
Wewe utarudishwa Uswahilini kwenu kwa miguu, ukiwa huna mbele wala nyuma, huna ujuzi wowote wa kazi, na aibu juu!
Inasikitisha dume zima unanyongwa uhuru wako, unafokewa na kupangiwa muda wa kurudi nyumbani saa kumi na moja jioni kama mtoto wa chekechea.
Utu wenu mmeuza kwa sahani ya chipsi zege na safari za kupiga picha za kuwaringishia masikini wenzenu kule Instagram. Mmekuwa kama chawa au pambo la sebuleni linalosubiri kupanguswa vumbi.
Shtukeni enyi wavulana wa darasa la saba la mapenzi! Tafuteni vya kwenu, vyombo vya kuazima haviendesheki mjini!