Hivi nyie watu, nini kinawafanya Mpende Pizza? sitaki hata kusikia

Hivi nyie watu, nini kinawafanya Mpende Pizza? sitaki hata kusikia

Majina tu hayo Malyafyare ni chapati za kuchoma na mikate ya nyama katikati, wala hakuna jipya.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] na kweli ni majina tu ndo yanatu changanya
 
Hiyo ni misosi ya Wazungu.
Sisi Wanaume wa Dar tunakula embe kwa chumvi na limao. Chipsi zege, Mahindi ya kuchoma na pilipili, mchicha wa bonde la msimbazi, pweza na chachandu, ngisi, supu ya maharage na chapatti nk.

Karibu D'aslam......Huku Viongozi wako wakuu ndipo wanapoishi.
Hujawahi kuona kwenye tafrija zetu tunakunywa juice kwa pipi?

Kalaghabaho
Hahahahahahahah........eti supu ya maharage
 
Majina tu hayo Malyafyare ni chapati za kuchoma na mikate ya nyama katikati, wala hakuna jipya.
Ni sawa na mshikaji mmoja hapa alikuwa analalamika alienda kwa hoteli akatajiwa majina ya vyakula akifikiri amepatia kumbe kaagiza MAKANDE
 
Dah! Bora nimepata mwenzangu. Haya mauchafu huwa siyafagilii hata kidogo. Huwa nashangaa sana nikiona watu wanavyohehuka nayo. Niwekee ugali wangu na samaki wa kukaanga mchicha chukuchuku au wa nazi, pilipili debe na gudulia langu la maji roho yangu KWATUU.
Duh! hapo kwenye red unatisha
 
nikila piza au bags naharisha sana yani filimbi tupu maliwtoni had I aibu
Hahahahahah.... umenikumbusha hata mimi kuna siku na mimi watu waliagiza bag na mimi nikafanya mbwembwe nikaagiza pia, nilipofika nyumbani ni siri yangu coz tumbo lilianza kuzingua kabla sijafika nyumbani nikawa mnajikaza tu
 
pizza inategemea ni ya nini na imeandaliwaje!!

pizza naweza kuitetea ila hayo mabarger hapana.
 
Mkuu wewe upo vizuri. Tutafutane tukale burger, Yule jamaa alokuwa akitengeneza pale Moroco kahamia Africa sana. Twenzetu baada ya hapo tukanywe soda pale kwenye bustani ya Ambiance. Tutakaa huku tukijadiliana fujo za akina espy kule MMU.
umechanganya wa Africasana mwingine na alikuwepo hata kabla wa morocco hajahama,wa morocco walihamia leaders nlienda majuzi na lara1 hata hatukuenjoy ile taste hakuna,kwa hasira tukaenda mlimani kula vipapatio vyenye pilipili
 
lara1 mzima lkn!
 
Pizza ni tamu mno inategemea umekula ya aina gani mie nnayopenda ni chicken Na pineapple
 
Back
Top Bottom