Wakati tukiwa field iitwayo block teaching practice kuna kundi la wenzetu kambini kwao walikuwa hawali kiporo wakikiita sleeping food. Sisi wengine wa kambi yetu tulikula poro sana tu, hata tulipoingia kazini asubuhi tulikula poro, msosi uliolala baada ya kubaki ile jioni au usiku. Ni poro la ugali au wali, au makande au ndizi, hakuna kutupa msosi, unapashwa au haupashwi, poro na chai au hivyo hivyo linapigwa kibingwa. Wenzetu vidosho wakataa viporo waliishiwa vyakula mapema wakaanza kumangamanga kila mmoja kula kivyake magengeni kwa mama lishe au mahotelini kutokana kumwaga chakula umoja wao wa kupika na kula pamoja ulivunjika ikabidi waishi kwa kujitegemea mifukoni mwao, chakula cha pamoja walikimwaga