Hivi nyie wenzangu huwa mnawezaje kula viporo?

Mjomba wewe utakuwa wa kishua sana yani viporo mbona unyama sana tena upate wali na kisamvu cha Nazi unapiga na chai fulani hivi
 
Wakati tukiwa field iitwayo block teaching practice kuna kundi la wenzetu kambini kwao walikuwa hawali kiporo wakikiita sleeping food. Sisi wengine wa kambi yetu tulikula poro sana tu, hata tulipoingia kazini asubuhi tulikula poro, msosi uliolala baada ya kubaki ile jioni au usiku. Ni poro la ugali au wali, au makande au ndizi, hakuna kutupa msosi, unapashwa au haupashwi, poro na chai au hivyo hivyo linapigwa kibingwa. Wenzetu vidosho wakataa viporo waliishiwa vyakula mapema wakaanza kumangamanga kila mmoja kula kivyake magengeni kwa mama lishe au mahotelini kutokana kumwaga chakula umoja wao wa kupika na kula pamoja ulivunjika ikabidi waishi kwa kujitegemea mifukoni mwao, chakula cha pamoja walikimwaga
 
Wabongo banaπŸ˜€

Kwenye keyboard kila mmoja hali kiporo anapata kichefuchefu ila pale anapoishi majiuharo yanatiririka mlangoni wana haoni hizo hali, analamba tu chips yai na nzi wa kijani wanamsalimia tuπŸ˜›πŸ˜›
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Njoo huku kwetu migodini Kahama ulete huo ubitozi ndio utajua kuwa hujui....
 
Niliona majuzi huyu Dr tuliyemtuma huko WHO akisema viporo siyo mbaya

Anyways nilikuwa sili kabisa viporo ila sasa nitakuwa na kula once
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…