Hivi nyie wenzangu mnawezaje kuishi na wanaume wazubaifu?

Hivi nyie wenzangu mnawezaje kuishi na wanaume wazubaifu?

Ukikaa mbele wanataka ukae nyuma, ukikaa nyuma wanataka ukae mbele!!
Na ukikaa kati ni haiwezekani 😁😁

Kifupi mwanamke haeleweki
Taabu kweli kweli ukiwa busy ni shida ukikosa cha kukufanya uwe busy nayo shida. Ukichelewa kurudi tabu, ukiwahi napo tabu yaani kueleweka kwao n ngumu.
 
Kuna raha fulani wanawake hupenda kuona mwanaume akiwa na mishe mishe nyingi. Yaani, kaingilia mlango huu, katokea huku, kisha kafika nyumbani, kakaa lisaa limoja, na kuendelea na misele yake. Mwanaume anarudi na mazaga mkononi, mnapiga stori, mnataniana, mnafurahi na kucheka. Kwa kifupi, mwanaume asiye poa ni furaha ya nyumba.

Lakini kuna majanaume fulani sijui kama yamekulia vijijini huko. Yenyewe yanazubaa tu, hayana mishe. Yanategemea mishahara pekee na yakitoka kazini ni moja kwa moja nyumbani, mpaka yanaboa. Wanaume hawa wanafuatilia tamthilia kwenye Azam TV, hawanywi hata wine, na gubu ndio usipime! Kununa kwa vitu vya kipuuzi ni kawaida. Kuvaa, hawajui; wanajua tu kuvaa manguo ya vitenge kama wacheza sindimba.

Jamani, wenzangu, mnawezaje kuishi na wanaume wazubaa hivyo?
Machepele na mwenye fujo kama Mimi itaniweza sasa?
 
Back
Top Bottom