Ukigombea Urais unaweza ukapata au usipate, na wakati unagombea unatokea kwenye nyumba yako ambayo naamini haizidi vyumba vitano vyakulala.
Ukipata Urais huwa serikali inakwenda kuyajenga makazi yako ku accommodate facilities zote za ulinzi na makazi ya walinzi? Au kila kiongozi ufanya maamuzi yakujengewa au kutokujengewa?
Pale butihama au Msasani ukiingia uoni sehemu yakuishi watu mia moja, kule msoga the same na hata kule milimani Tanga hakuna eneo kubwa hivi.
Hizo facilities ukistaafu zinakuwa Mali yako au Mali ya serikali? Kama zinakuwa Mali yako unazifanyia Nini?
Nakumbuka Zuma alijaribu kujenga kasiri kwake wakamvua madaraka sasa hivi anasota mahakamani, kwanini mataifa mengine ya Afrika hayafuati huu mfumo.
Kuwa na kasiri kunaatract kuendelea kuwa na watu wakulihudumia ambapo ili uwapate lazima lazima uzidi kubaki kwa pawer.
Tuelimishane kuhusu nyumba binafsi za watawala