Uchaguzi 2020 Hivi pamoja na "promo" yote ya mabango yaliyotapakaa nchi nzima, ni kwanini CCM inapelekwa mchamchaka na Tundu Lissu?

Slogan yetu watanzania ni hii:
" .......kufuli tunavunja, pombe tuna mwaga na Ikulu tunaingia, tumeamua Kwa ridhaa yetu wenyewe kumkataa shetani na kazi zake zote "
hapo kwenye kumkataa .sheitwani............. na kazi zake zote umenifanya nicheke kama fala hapa mtaani
 
Subiri matokeo utaona kama alikuwa anawapelekesha au alikuwa anapelekeshwa utakapoona % atakayo pata
 
Ccm ndio hii ambayo imekuwa ikilalamikiwa miaka yote na kuambiwa imechoka na kwamba inatumia nguvu ya dola kuendelea kuwepo madarakani sijui inaiba kura,2015 vyama vikaungana ila bado ccm ikaendelea kuwa madarakani. Sasa sijui ni stress tu zinawafanya watu kuona kwamba et sasa ndio ccm ina hali mbaya kisa mtu mmoja tu Lissu.

Kama unaamini ccm imekuwa ipo madarakani kwa sababu ya kutumia nguvu ya dola basi ni wazi kuwa ccm ipo kwenye hali mbaya muda wote na ndiyo maana inaiba kura,sasa haya ya kupamba Lissu hata sioni mantiki yake na ukizingatia cha msingi ni ccm ing'oke na sio kuishia kuipeleka mchakachaka halafu mwisho wa siku tunakuja kulalamika yaleyale ya aiku zote.
 
Subiri matokeo utaona kama alikuwa anawapelekesha au alikuwa anapelekeshwa utakapoona % atakayo pata
Nyinyi mwaka huu hamtoboi.......

Mategemeo yenu makubwa ni kubebwa na vyombo vya dola, kama vile Jeshi la Polisi, NEC na TISS, katika kuwanusuru.......
 
Fedha yote ya kampeni CCM ni fedha za umma. Hii inazidisha hasira kubwa sana. Kifo cha CCM kwa lugha yeyote ile ni tarehe 28 Oktoba 2020.
Kwani hizo mnazofanyia nyinyi ni kutoka kwa nani?
 
...wapinzani wa kisiasa wako hoi bin taabani...mh...wanawezaje kupeleka puta Ccm?
 
Masikini ni kiumbe kimoja dhaifu na jinga sana ,hataki tajiri awe na kitu ambacho yeye hana uwezo nacho kukimiliki, hanakuwa hana tofauti na mchawi.chadema hamjakatazwa kuweka mapicha na mabango.
Hivi kweli unadhani CHADEMA hata wakitaka kuweka mabango hapo ubungo interchange watakubaliwa? ile kulishika tu kabla hata ya kufikia nguzo tayari virungu!! Hakuna usawa katika hili, ndio maana nadhani wameamua kutojisumbua nayo!!
 
Halafu picha yake, rangi ya chama chake, na mabango yenyewe ni uchafu mtupu! Ni Kichefuchefu kabisa. Miji imechafuka kwa mibendera yao na mabango yao. Wanashindwa kutumia fedha hizo kuajiri vijana wetu wao wameingia kwenye anasa ya kuuza sura ya Dikteta wao, Nduli Idd Amin wa Chattle.
 
Namkataa shetani, na kazi zake zote na mambo yake yote........... Najitoa kwa mtu wa watu ili nimpigie kura na kumuombea kwa Mungu amlinde hadi atakapoingia Ikulu ila akasafishe nyumba yetu iliyogeuka pango la wanyangányi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…