Baada ya Mzee Abdul kumpiga mimba mamake Darleen na hatimae kuzaliwa Darleen, hapo ukawa ndio mwisho wa uhusiano wa Darleen na mamake Darleen! Ninachotaka kusema ni kwamba, hata Queen Darleen hakukulewa na babake! Na mbali na Quuen Darleen, pia ana mtoto mwingine wa kike ambae anaishi na shangazi yake, yaani dadake na Mzee Abdul!Lakini hakukuwahi kuwa na habari kuwa Quuen hakulelewa na baba yake, ila ni Diamond tu ndio hakupata msaada wa baba yake kipindi bado mdogo, Ningemuona Queen ni wa maana kama yeye angekuwa wa kwanza kwenda kumsaidia baba yake kitu ambacho Diamond roho ingemuuma na yeye angesaidia kimya kimya, ingesaidia huyu mzee kuacha kuzunguka mitandanoni kitu ambacho kinawadhalilisha wote.p
Tatizo Mzee Abdul alikuwa na usela wa kupitiliza! Hivi humuoni tu hata jinsi anavyoongea ukalinganisha na umri wake?! Halafu nikujuze jambo lingine! Hao wote sio kwamba wanawake walikuwa wanaishi kwa Mzee Abdul bali Mzee Abdul alikuwa ndo anahamia kwa mwanamke; wakizinguana, anasepa!