Tatizo ni moja tu. Jiwe aliamini kuwa "ka-corona" ni kaugonjwa kanakowahusu mabeberu tu na kwa maana hakutarajia nchi "ingepigwa" na huu ugonjwa.
Maambukizi yalipoongezeka kwenye nchi yake kwa zaidi ya asilimia 500 ndani ya wiki moja akili yake ikampa kwamba "si bure, bali kuna mkono wa mtu" ambao ni wakala wa mabeberu unafanya hujuma kwa kusambaza corona kupitia fumigation, barakoa za msaada na hata vifaa vya kupimia ugonjwa wenyewe (Covid-19 test kits).
Kwa mtazamo wake huu corona ni tatizo la kiafya linalotokana na "mambo ya kiusalama" kutoka kwa maadui na kwa maana hiyo vyombo vya ulinzi na usalama vinatakiwa vifanye kazi yake kama ifuatavvyo.
1. Wachunguze ni nani alitoa amri ya kufanya fumigation Mwanza na Dar,
2. Wachunguze kubaini endapo "fumigants" zilizotumika hazikuwa na virusi vya corona kwa kuwa mlipuko uliongezeka mara dufu mara baada ya zoezi la fumigation.
3. Vyombo vya ulinzi na usalama viingie maabara kuu ya taifa ya afya (NHL-QATC) na kuchunguza ubora na usalama PCR kits zinazotoa majibu chanya mengi kwa sampuli zinazopimwa. Lakinini pia wabaini hizo kits zilitoka wapi na ziliingia kwa utaratibu gani.
4. Jeshi la polisi kwa kushirikiana na TCRA wachunguze na kupambana na watu wanaoandika taarifa "mbaya" kuhusu corona hapa nchini.
5. Wizara ya afya ichunguzwe kwani huenda inatekeleza maelekezo ya mabeberu kutoa taarifa zinanazoelemea idadi ya maambukizi mapya peke yake bila kutaja idadi ya wagonjwa ambao wamepona kama mh. Rais ali yodokezwa na "watu wake" kuwa ni zaidi 100 ndo wamepona.
Kiufupi ni kwamba Mh Rais hana imani na mabeberu. Anahisi wamesambaza ugonjwa huu ili nchi zipigike kiuchumi na ziendelee kuwa tegemezi kwa misaada na mikopo toka kwao.
Kwa Magufuli "offer" ya mkopo iliyotolewa na Benki ya Dunia katikati ya janga la corona maana yake ndo hiyo. Ndiyo maana ameijibu ofa hiyo kwa "challenge" kwamba kama kweli mabeberu wana nia njema kwa nchi zilizoathirika kiuchumi kutokana na corona, basi hiyo "offer" isiwe mikopo badala yake watoe nafuu kwa kusamehe "asilimia fulani" katika madeni yao wanayodaiwa sasa.