Hivi Rais Magufuli alifanya maamuzi ya busara kwa kuwaita Wakuu wa Vyombo vya Usalama kuongelea COVID19, badala ya kuwaita Wataalamu wa Afya?

Hivi Rais Magufuli alifanya maamuzi ya busara kwa kuwaita Wakuu wa Vyombo vya Usalama kuongelea COVID19, badala ya kuwaita Wataalamu wa Afya?

Wataalamu wa afya walikua katika majukumu


Izo tangawizi na limau ziwe nyingi
The-Monk
Unataka kuniambia kuwa hao wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama hawakuwa na majukumu mengine?

Ni watu wachache sana waliohitajika kwenye kikao hicho cha Rais, ambao ni waziri Mkuu na waziri wa Afya, kwa hiyo usitafute sababu za "ku-justify" maamuzi ya Jiwe
 
The-Monk
Unataka kuniambia kuwa hao wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama hawakuwa na majukumu mengine?

Ni watu wachache sana waliohitajika kwenye kikao hicho cha Rais, ambao ni waziri Mkuu na waziri wa Afya, kwa hiyo usitafute sababu za "ku-justify" maamuzi ya Jiwe
Mkuu
Ilo jibu nililiandika tu ili nifurahi

Kwa sababu jiwe kashafanya hatuna case mpya

Ongeza tangawizi na limau

Twafa
 
Maslahi ya umma ndio muhimu, yale ya wapigaji hayapaswi kukuumiza kichwa.

Ukimsikiliza kila mtu wasio na shukrani baadae watakuita dhaifu.
Hayo maslahi ya Umma ndiyo yapi hayo?

Unaweza ukaita hiyo ya kuwaita wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuwa ndiyo maslahi ya Umma??

Mimi naona kama angekuwa amewaita wataalamu wa Afya akawahutubia na baadaye akaruhusu maswali ya papo kwa hapo, hicho kikao ndiyo kingekuwa cha maslahi mapana ya Umma
 
Hayo maslahi ya Umma ndiyo yapi hayo?

Unaweza ukaita hiyo ya kuwaita wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuwa ndiyo maslahi ya Umma??

Mimi naona kama angekuwa amewaita wataalamu wa Afya akawahutubia na baadaye akaruhusu maswali ya papo kwa hapo, hicho kikao ndiyo kingekuwa cha maslahi mapana ya Umma
Katika wageni waalikwa aliapishwa mmojawapo ambaye nu mtu wa afya, ujumbe wa afya unakwenda kufanyiwa kazi kupitia yeye.

Umuhimu wa ulinzi na usalama ni kitu muhimu sana ndio maana nchi yetu ipo salama.
 
Mimi kilichonistua na nikadhani kua jamaa wenda siyo mTanzania halisi ni hali ya kuona jambo aliloliita ya kupumbavu inafanyika yeye yupo kimya then anakuja kuibuka baadae ..sijui ingekua na madhara kwa wananchi angesemaje.
 
Amefanya busara kwa sababu hawa watamuelewa zaidi kuhusu tiba ya mvuke kuliko wataalamu wa afya.
 
Maadui wa taifa hutumia kila mbinu kupata upenyo kufanya wanayotaka. Usidhani kila anayehubiri corona anawaza hilo tu. Maadui wanatumia nafasi ya sisi kuwa busy na corona, wao wataingiza vyao au hata watu wao kwa malengo yao. Hata aliposema angalieni wasijeingiza vitu vya hatari atakuwa ameshanusa harufu ya jambo fulani.

Kwa maadui zetu hata sherehe zetu ni hatari kwetu. Misiba yetu ya kitaifa na ziara za viongozi na wafanyabiashara toka nje ni hatari kwetu. Kwao ni fursa.

Nakumbuka Mkapa akiwa rais kulikuwa na tukio la harusi katika familia yao. Kuna mdau alitaka kuchangia 30m. Mkapa alikataa. Ni mfano tu wa maadui zako wanavyoweza kutumia raha au shida zako kukuteka na kisha kukuangamiza.
Labda corona ingekua TZ peke yake ningeunga mkono haya uyasemayo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikataza wagonjwa wapya wa corona kutangazwa
Ni utaratibu wa WHO ni lazima utaje kwa uwazi, idadi ya wanaoambukizwa, idadi ya wale waliopona na idadi ya waliokufa

Sasa yeye alitaka kufanya siri siri, kama alivyozoea kufanya mambo yake mengine??
 
Sababu za kuwa lilivyo sasa zipo za kisayansi mkuu, tatizo hakuna ukamilifu katika kila akifanyacho binadamu.
Mbona wenzetu wanafanikisha.Tusipoweka Sheria za kuwafunga viongozi yaani wakitoka madarakani ni jela maisha wataendelea kuchezea Kodi zetu na maendeleo tutayasikia kwenye radio
 
Mbona wenzetu wanafanikisha.Tusipoweka Sheria za kuwafunga viongozi yaani wakitoka madarakani ni jela maisha wataendelea kuchezea Kodi zetu na maendeleo tutayasikia kwenye radio
Sisi tunafanikisha tena sana tu, inategemea wewe binafsi mtazamo wako upo vipi.

Kama glass imejaa nusu kwenda juu au imepungua nusu kwenda chini, hilo ni suala la akili yako binafsi.
 
Tuliona wenyewe Rais Magufuli akiwaita wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini, wengi wakitoka jijini Dar na wengine wakitokea Dodoma, umbali mrefu wa kilometa maelfu, kuongelea ugonjwa wa corona, ambao unatikisa dunia nzima hivi sasa, ikiwemo Tanzania.

Nimekuwa nikijiuliza hivi si yeye mwenyewe ndiye aliyeunda hii Tume ya kitaifa, inayoshughulikia na kuratibu masuala yote ya ugonjwa wa corona nchini, akiwemo waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, mbona sijawaona wakiwa ni miongoni ya waalikwa kwenye kikao hicho?

Hivi Mheshimiwa Rais, anadhani kuwa ugonjwa wa corona utaondoka nchini kwa vifaru vya kijeshi, au mabomu ya machozi, au bunduki "zilizokokiwa" risasi za moto, au magari ya washawasha ya IGP Sirro?

La hasha, asijidanganye, hivyo virusi haviwezi kamwe kuondoka nchini kwa nguvu za kijeshi nchini, kwa kuwa hivyo virusi vya corona ni "invicible enemy"

Kwa kuwa kama nguvu za kijeshi zingekuwa na uwezo wa kuondoa virusi hivyo, basi Taifa kama Marekani linaloongoza duniani kwa nguvu za kijeshi, lisingekuwa linapelekwa "mchakamchaka" hadi sasa hivi likiwa ndilo linaloongoza duniani kwa maambukizi mengi na vifo pia

Mimi sikuona mantiki ya kuwaita wakuu wa vyombo vya usalama wa nchini kuongelea ugonjwa wa Corona nchini, wakati akiwaacha wataalamu wa Afya,ambao hivi sasa ndiyo wako mstari wa mbele kabisa katika vita hii ya kuutokomeza ugonjwa wa Corina nchini.

Kwa kuwa tunadadavua kujua mantiki ya Mheshimiwa Rais, kuwaita wakuu hao wa vyombo vya usalama nchini kwenda kijijini kwake Chato na kwenda kuwahutubia kuhusu suala la kiafya, nawakaribisha sana wadau nanyi mtoe maoni yenu
Tulishaandika hapa hidden facts in President magufuli's speech on 22th aprill 2020 - jamii forums
 
Back
Top Bottom