Hivi Rais Samia anajua namna Machinga wanavyopigwa na kuporwa Biashara zao?

Hivi Rais Samia anajua namna Machinga wanavyopigwa na kuporwa Biashara zao?

rajiih

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2019
Posts
489
Reaction score
744
Habari wana JF poleni na Majukumu ya kikazi. Nianze na maada kama kichwa changu hapo juu kinavyosomeka.

Nikiwa mmoja wa wahanga katika suala zima la wamachinga nimeona nije mbele yenu pengine jambo hili la Unyanyasaji na lenye kutia hasira, hasara zaidi linaweza komeshwa.

Tumekuwa wanyonge sana hatuna shida na serikali hii ila kwa namna mambo ya kikatili yanayoendelea pengine siku moja zitakuja tokea athari mbaya na sina hakika kama Mh rais anatambua ukatili huu unaotokea tena katika wilaya ambayo ndio kitovu cha Mapato nchini.

Tulio wengi tumefilisiwa vibaya kiasi hatuna tena pakushika ukizingatia na mikopo midogo ya wajasirimali tuliokopa kwa ajili ya kukwamua tatizo la ajira nchini lakini swali ni Je, tumekopeshwa ili waje watupole kwa nguvu?! Pesa zao tutazirudisha kwa namna gani ikiwa wameajiri migambo kadhaa kwa ajili ya kuzuiwa mamia ya vijana kwa watu wazima ambao tayari walikua wamepiga hatua ambayo kwa siku za usoni wangeweza toa fursa za kuajili wenzao.

Ni namna gani serikali inamsupport kijana ambaye anamtaji mdogo swala la ondoa machinga limechukuliwa kama mateso kwa machinga tukale wapiii? Tuishi vipi?

Wamechukua mzigo wangu wa 240k wanadai nilipe faini 300k hivi kweli kuna support hapo kwa serikali yetu kwa vijana ambao hawana hata hio pesa ya kodi kwa vizimba vya Biashara ?!

Mama unatengeneza taifa gumu sana huko mbeleni vijana hawatakua na maisha yenye msimamo kwa familia zao matokeo yake wizi, Ujambazi na matukio ya kutisha hayatakoma sababu ya ugumu wa Kimaisha.

Mwenye uwezo wa kuufikisha ujumbe huu kwa niaba ya vijana watafutaji atusaidie kufikisha kilio hiki tunaimani na Mama

Kwa niaba ya wamachinga soko kuu la nguo na viatu Karume.

NAWASILISHA
 
Poleni sana mkuu, ngoja wasaidizi wake wapite kwenye hii thread
 
Fuateni sheria,hakuna mwenye biashara rasmi anayefuatwa na migambo, machinga na bodaboda ni janga la taifa, lazima wadhibitiwe ipasavyo, nimesema hivyo kama unataka vita njoo
 
Naona kuna operation maalumu, maeneo ya Tegeta pamesafishwa

Mbagala pia

Mbezi
 
Japo si sawa lakini je ni sahihi kufanyia biashara barabarani? Hadi sisi wapita njia tunakosa sehemu ya kupita? Tuna koswa koswa magari kama sio kugongwa kabisa?!!juzi mwanza wamachinga ndio wanatoa maagizo ni wapi wanataka kukaa na sio sehemu nyingine!la sivyo hawakubali. Hata hao wenye maduka waoneeni huruma jamani.
 
Fuateni sheria, mbona mnataka kujifanya nyie ndio raia kuliko wengine?
 
Fuateni sheria,hakuna mwenye biashara rasmi anayefuatwa na migambo, machinga na bodaboda ni janga la taifa,lazima wadhibitiwe ipasavyo,nimesema hivyo kama unataka vita njoo
Hakuna sheria wagambo ni watu wenye njaa na dhiki, haijalishi unafuata sheria au hapana,kwanza wagambo wenyewe wanafanya kazi pasipo kufuata sheri, na hawazijui vilevile, we unamkamata muuza madafu ambae anatembeza madafu yake ili iweje,huezi kumkataza asifike posta, kwani posta watu hawanywi madafu, upuuzi na uonevu na ujinga, panya road wanasumbua sana,wagambo badala watumiwe kudhibiti panya road, wanaenda kupora kwa kutumia sheri, haya madafu wakipora wanapeleka wapi? Wali wanapeleka wapi.
 
Muda mwingine nanyinyi ni wasumbufu sana, yani mnaziba njia kanabaki kaupenyo kadogo sasa watu wapite wapi? Nendeni sehemu rasmi mkafanye biashara sasa nyinyi kila wanapo simama au kupita watu mnafanya ni soko hii haijakaa sawa.
 
We bila shaka hujazaliwa Dar es Salaam. Umachinga siyo kazi kimsingi. Umewahi sikia nchi za wenzetu hata pale Rwanda kuna umachinga. Ni kazi isiyokuwa na utaratibu wala ustaarabu. Biashara tafuta fremu lipia vyote vinavyohitajika fuata taratibu na sheria za nchi.

Km huwezi rudi kijini kafanye shughuli zingine ukipata mtaji rudi mjini. Kwa hiyo kwa akili yako barabara za lami za mjini ndiyo meza zenu za kufanyia biashara? Na kuvia wateja kwenye korido za maduka ya watu ndiyo biashara? Hizo tayari ni fujo lazima ushughulikiwe. Kipindi cha JPM niliona pale Arusha mjini mtaa wa kati maeneo ya soko kuu malori yalikuwa yashindwa kupeleka bidhaa madukani barabara zote wametandika wanazoziita biashara, ile ilikuwa fujo na uchafu.

Msitumie gia ya unyonge au umaskini kuvuruga taratibu za miji. Kwanza umaskini na unyonge siyo sifa. Halafu bila aibu unatishia mtaishia kwenye uwizi, ujambazi na matukio mengine. Inavyoonekana we tayari ni mwizi unatumia umachinga kuchora ramani. Vile vile uwe wa kwanza kuanza hizo kazi uone matokeo yake km watashindwa kukuwahisha kwa mola wako. Shenzi kweli unatishia mtakuwa majambazi?
 
we bila shaka hujazaliwa Dar es Salaam. Umachinga siyo kazi kimsingi. Umewahi sikia nchi za wenzetu hata pale Rwanda kuna umachinga. Ni kazi isiyokuwa na utaratibu wala ustaarabu. Biashara tafuta fremu lipia vyote vinavyohitajika fuata taratibu na sheria za nchi...
Nimependa Sana hiyo sentence ya mwisho. Dah [emoji23][emoji23][emoji23]

Kuna Mtu sio mmachinga ila hapendi kuibiwa Sasa ajichanganye ***** kama hatobaki jina. Yaani Kuna Maamuzi Mtu ukichukukua unaweza kujikuta hata hiyo familia Yako yenyewe unaitia matatizoni.
 
We bila shaka hujazaliwa Dar es Salaam. Umachinga siyo kazi kimsingi. Umewahi sikia nchi za wenzetu hata pale Rwanda kuna umachinga. Ni kazi isiyokuwa na utaratibu wala ustaarabu. Biashara tafuta fremu lipia vyote vinavyohitajika fuata taratibu na sheria za nchi.

Km huwezi rudi kijini kafanye shughuli zingine ukipata mtaji rudi mjini. Kwa hiyo kwa akili yako barabara za lami za mjini ndiyo meza zenu za kufanyia biashara? Na kuvia wateja kwenye korido za maduka ya watu ndiyo biashara? Hizo tayari ni fujo lazima ushughulikiwe. Kipindi cha JPM niliona pale Arusha mjini mtaa wa kati maeneo ya soko kuu malori yalikuwa yashindwa kupeleka bidhaa madukani barabara zote wametandika wanazoziita biashara, ile ilikuwa fujo na uchafu.

Msitumie gia ya unyonge au umaskini kuvuruga taratibu za miji. Kwanza umaskini na unyonge siyo sifa. Halafu bila aibu unatishia mtaishia kwenye uwizi, ujambazi na matukio mengine. Inavyoonekana we tayari ni mwizi unatumia umachinga kuchora ramani. Vile vile uwe wa kwanza kuanza hizo kazi uone matokeo yake km watashindwa kukuwahisha kwa mola wako. Shenzi kweli unatishia mtakuwa majambazi?
Mkuu ndio hiki kilichokuja katika akili yako na uko sahihi hivi nikuulize swali

kuzaliwa dar es salaam kuna uhusiano gani na kuwa au kutokuwa Machinga?!

kama una maisha mazuri wacha unyanyapaa kwa wasio kua nacho nawe kama sio Muhaya bahati na kilicho kero kwako mwenzako kina mpatia faraja katika maisha yake.
 
Back
Top Bottom