rajiih
JF-Expert Member
- Apr 4, 2019
- 489
- 744
Habari wana JF poleni na Majukumu ya kikazi. Nianze na maada kama kichwa changu hapo juu kinavyosomeka.
Nikiwa mmoja wa wahanga katika suala zima la wamachinga nimeona nije mbele yenu pengine jambo hili la Unyanyasaji na lenye kutia hasira, hasara zaidi linaweza komeshwa.
Tumekuwa wanyonge sana hatuna shida na serikali hii ila kwa namna mambo ya kikatili yanayoendelea pengine siku moja zitakuja tokea athari mbaya na sina hakika kama Mh rais anatambua ukatili huu unaotokea tena katika wilaya ambayo ndio kitovu cha Mapato nchini.
Tulio wengi tumefilisiwa vibaya kiasi hatuna tena pakushika ukizingatia na mikopo midogo ya wajasirimali tuliokopa kwa ajili ya kukwamua tatizo la ajira nchini lakini swali ni Je, tumekopeshwa ili waje watupole kwa nguvu?! Pesa zao tutazirudisha kwa namna gani ikiwa wameajiri migambo kadhaa kwa ajili ya kuzuiwa mamia ya vijana kwa watu wazima ambao tayari walikua wamepiga hatua ambayo kwa siku za usoni wangeweza toa fursa za kuajili wenzao.
Ni namna gani serikali inamsupport kijana ambaye anamtaji mdogo swala la ondoa machinga limechukuliwa kama mateso kwa machinga tukale wapiii? Tuishi vipi?
Wamechukua mzigo wangu wa 240k wanadai nilipe faini 300k hivi kweli kuna support hapo kwa serikali yetu kwa vijana ambao hawana hata hio pesa ya kodi kwa vizimba vya Biashara ?!
Mama unatengeneza taifa gumu sana huko mbeleni vijana hawatakua na maisha yenye msimamo kwa familia zao matokeo yake wizi, Ujambazi na matukio ya kutisha hayatakoma sababu ya ugumu wa Kimaisha.
Mwenye uwezo wa kuufikisha ujumbe huu kwa niaba ya vijana watafutaji atusaidie kufikisha kilio hiki tunaimani na Mama
Kwa niaba ya wamachinga soko kuu la nguo na viatu Karume.
NAWASILISHA