MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Haiwezekani mtu mwaka unaisha anafuatilia pesa yake na amekwisha staafu anazungushwa tu hakuna majibu ya kueleweka. Hivi huyu mzee mnata aingie mtaani aishi vipi wakati mshahara hana na pesa anazodai ni zake?
Hii siyo kujitafutia laana na chuki ni kitu gani? Mnadhani kiwango cha chuki nchini mwetu kiko juu, mnadhani kwa hali hii watu watalipendaje taifa?
Wazee hawa kila wakienda kwenye ofisi za mifuko yao ya hifadhi ya jamii wanaambiwa shida haipo kwao, tatizo Hazina ndio hawatoi pesa. Hivi Hazina hizi pesa ni za kwenu? Mtu process zote za kupatiwa pesa zake zimeshakamilika, mnachochelewesha ni kitu gani? Huu ubabe hata kwenye mali za watu utawasaidia kitu gani hasa?
Wabunge wanamaliza miaka yao 5 kabla hata ya kuanza uchaguzi mpya tayari wameshalipwa pesa zao, huu upendeleo ni wa hovyo kabisa na ni madhambi makubwa. Mungu ataendelea kuwalaani wote wanaohusika na kuwasumbua wazee hawa.