Hivi Serikali inajua rushwa inayoendelea kwenye shirika la Hifadhi ya Jamii?

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,468
Reaction score
32,167
Nadhani kwa sasa hawa wafanyakazi wa hilli shirika wamepiku askari wa babarani kwa kuonea watu na kula rushwa. Mtu akiwa nafuatilia haki yake atazungushwa sana ili mradi tu atoe rushwa.

Kuna mama mmoja ni kati ya wafanyakazi wa DSTV walioachishwa kazi toka mwaka juzi, amefuatilia anaambiwa atoe 20% ya pesa yake ndipo apewe ela yake kagoma, ila kila akienda wanamwambie leta hiki leta kile anafuata utaratibu wao akikaribia kumaliza wanamrudisha mwanzo kuwa kuna kitu kimemiss ambacho hakuwa kaambiwa.

Kuna mtu akamwambia hawa wanakufanyia makusudi hata haya wanayokwambia ulete hayana maana kwakuwa vitu vyote wanavyo kwenye system yao sasa yanini wakusumbue hivi?

Mimi pia nina ndugu yangu anafuatilia toka mwezi wa 3 aliambiwa atawekewa ela, wakamwambia mara afungue akaunti mpya mara hivi mara vile akakaribia kufika mwisho, eti sijui afungue akaunti nyingine na kumbuka akifanya hivi anaanza machakato mpya. Ndipo wakamwambia atoe milioni moja cash na mwingine ampelaki tano ndipo ela yake itaingia.

Kuna watu weengi wanalalamika sana juu ya haya mambo sijui kwanini serikali imeyafumbia macho.

Iweje mtu aweke pesa yake halafu akijaichukua asumbuliwe kama anasaidiwa?
Serikali itazame kwa umakini haya mashirika watu wanateseka sana na hawana pa kusemea
 
Mwambie huyo mstaafu ajiongeze la sivyo ataendelea kupauka
 
  • Thanks
Reactions: 30P
Watanganyika acheni ujinga , si uende takukuru mumlambishe hela za Moto iwe fundisho.

Kama mnaona hamuwezi nenda kwa meneja wa hilo tawi mwambie utakuja kufanya tukio hata Mungu atashangaa
Hawapokei ela kindezi hivyo nao wanajua kuwa kuna za moto
 
Nadhani kwa sasa hawa wafanyakazi wa hilli shirika wamepiku askari wa babarani kwa kuonea watu na kula rushwa. Mtu akiwa nafuatilia haki yake atazungushwa sana ili mradi tu atoe rushwa.
Kuna mama mmoja ni kati ya wafanyakazi wa DSTV walioachishwa kazi toka mwaka juzi, amefuatilia anaambiwa atoe 20% ya pesa yake ndipo apewe ela yake kagoma, ila kila akienda wanamwambie leta hiki leta kile anafuata utaratibu wao akikaribia kumaliza wanamrudisha mwanzo kuwa kuna kitu kimemiss ambacho hakuwa kaambiwa. Kuna mtu akamwambia hawa wanakufanyia makusudi hata haya wanayokwambia ulete hayana maana kwakuwa vitu vyote wanavyo kwenye system yao sasa yanini wakusumbue hivi?
Mimi pia nina ndugu yangu anafuatilia toka mwezi wa 3 aliambiwa atawekewa ela, wakamwambia mara afungue akaunti mpya mara hivi mara vile akakaribia kufika mwisho, eti sijui afungue akaunti nyingine na kumbuka akifanya hivi anaanza machakato mpya. Ndipo wakamwambia atoe milioni moja cash na mwingine ampelaki tano ndipo ela yake itaingia.
Kuna watu weengi wanalalamika sana juu ya haya mambo sijui kwanini serikali imeyafumbia macho.
Iweje mtu aweke pesa yake halafu akijaichukua asumbuliwe kama anasaidiwa?
Serikali itazame kwa umakini haya mashirika watu wanateseka sana na hawana pa kusemea
Nawashauri enyi wastaafu msiwe watumwa kwenye vyombo kama hivyo. Naamini muda mliofanya kazi umewapa ujasiri na uelewa wa mambo mengi katika nchi hii, sasa kwa nini mnakubali kuwa wanyonge mbele ya HIVYO VIKARANI kwenye hayo mashirika.

Acheni UNYONGE daini haki zenu kwa ujasiri na kama wanawakwamisha, nawashauri nendeni mkawaone wakubwa wao, wao siyo mwisho, in fact wao ni mwanzo tu wa system kwenye hilo shirika. Halafu kama mnao ushahidi wa kutosha basi nendeni TAKUKURU, hawa ndio kiboko yao!
 
Nenda takukuru utapewa utaratibu hao wataingia online
Mimi siyo mhusika ila nimeweka hapa tu viongozi wa serikali walioko humu waone jinsi watu wanavyopata tabu kufuatilia pesa yao
 
Watanganyika acheni ujinga , si uende takukuru mumlambishe hela za Moto iwe fundisho.

Kama mnaona hamuwezi nenda kwa meneja wa hilo tawi mwambie utakuja kufanya tukio hata Mungu atashangaa
Hata mimi nawashangaa watanzania wana unyonge wa kipumbavu.
Wewe unajua kwamba akaunti ya benki ulishapeleka,unaambiwa upeleke tena akaunti halafu unaitikia tu bila kuhoji kwamba ile akaunti ya kwanza imepelekwa wapi,na kama imepotea kwa nini ipotee.
Lakini uwaulize maswali ya kina sio unapelekwa tu kama ling'ombe halafu unaitikia tu
 
Mimi siyo mhusika ila nimeweka hapa tu viongozi wa serikali walioko humu waone jinsi watu wanavyopata tabu kufuatilia pesa yao
Acheni kutegemea viongozi Nyie watanganyika ndio maana shida hazipungui Licha ya viongoz kupambana kwa ajili yenu. Kiongozi ana nafasi Yake na raia mna nafasi yenu.

Sasa issue Kama hii kiongoz unamtaka wa nini?

Nendeni pale muuwashe Moto na ombeni kuonana na meneja mkuu sio hao vidagaa muone Kama hamtaanza kuogopwa.

Tatizo la watanzania hamjui haki zenu laiti mngekuwa mnajua Haki zenu Kitu Kama hiki sio Cha kutegemea Kiongozi akuteteee huo n upumbavu na ujinga tunaoulea wenyewe wakati uwezo wa kupambana na huu upuuzi uko mikonon mwenu
 
Hata mimi nawashangaa watanzania wana unyonge wa kipumbavu.
Wewe unajua kwamba akaunti ya benki ulishapeleka,unaambiwa upeleke tena akaunti halafu unaitikia tu bila kuhoji kwamba ile akaunti ya kwanza imepelekwa wapi,na kama imepotea kwa nini ipotee.
Lakini uwaulize maswali ya kina sio unapelekwa tu kama ling'ombe halafu unaitikia tu
Matanzania ni mapumbavu Sana hata awe na elimu ya PhD bado unamkuta kakaliwshwa kwenye mbao za nssf anadanganywa.

Mimi nilimaliza kazi sehemu flani ikabidi niombe pesa yangu nssf ubungo plaza , Kitu nilichokifanya sidhani Kama watasahau.
 
Nawashauri enyi wastaafu msiwe watumwa kwenye vyombo kama hivyo. Naamini muda mliofanya kazi umewapa ujasiri na uelewa wa mambo mengi katika nchi hii, sasa kwa nini mnakubali kuwa wanyonge mbele ya HIVYO VIKARANI kwenye hayo mashirika. Acheni UNYONGE daini haki zenu kwa ujasiri na kama wanawakwamisha, nawashauri nendeni mkawaone wakubwa wao, wao siyo mwisho, in fact wao ni mwanzo tu wa system kwenye hilo shirika. Halafu kama mnao ushahidi wa kutosha basi nendeni TAKUKURU, hawa ndio kiboko yao!
Hata mimi nawashangaa sana watanzania.
Yaani vile vikarani vya dirishani vinawababaisha na kuona kama wakisema kitu ni sheria.

Halafu hao watu wanaoomba rushwa waziwazi hivyo mbona ni rahisi sana kuwakamata.
Unawapanga takukuru unawapa hela za moto ili iwe fundisho
 
Acheni kutegemea viongozi Nyie watanganyika ndio maana shida hazipungui Licha ya viongoz kupambana kwa ajili yenu. Kiongozi ana nafasi Yake na raia mna nafasi yenu.

Sasa issue Kama hii kiongoz unamtaka wa nini?

Nendeni pale muuwashe Moto na ombeni kuonana na meneja mkuu sio hao vidagaa muone Kama hamtaanza kuogopwa.

Tatizo la watanzania hamjui haki zenu laiti mngekuwa mnajua Haki zenu Kitu Kama hiki sio Cha kutegemea Kiongozi akuteteee huo n upumbavu na ujinga tunaoulea wenyewe wakati uwezo wa kupambana na huu upuuzi uko mikonon mwenu
Issue ni kwamba viongozi wahakikishe wametengeneza mifumo iliyo rahisi wameweka vyombo vitakavyohakikisha hakuna urasimu. Sasa wewe data za mwanachama waowanazo, wamempa kitambulisho na namba halafu wanaanza kumwambia sijuia alete barua toka serikali za mtaa, sijui kitambulisho cha uraia, birth certificate, mara afungue akauntinyingine, mara barua sijui ya nini.

Tanzania hakuna haki, inategemea unazungumzia haki kwa mtazamo unaomfurahisha nani. Ukitaka kujua kuwa hakuna haki hadi vyombo vya kusimamiahaki vinavunja haki mfano mtu anashikiliwa kituo cha polisi zaidi ya masaa 48 bila hata ndugu zake kuambiwa ana kosa gani.
 
Matanzania ni mapumbavu Sana hata awe na elimu ya PhD bado unamkuta kakaliwshwa kwenye mbao za nssf anadanganywa.

Mimi nilimaliza kazi sehemu flani ikabidi niombe pesa yangu nssf ubungo plaza , Kitu nilichokifanya sidhani Kama watasahau.
Ila tuache kuwa watanzania ni wapumbavu, je inapaswa kuwa hivi?
Kwanini mtu mpaka atumie nguvu kupata haki yake?
Kwanini isiwepo misingi ambayo hata asiyejua aende wapi apate haki yake kiurahisi tu? Nini kinashindikana hapo kama serikali ikiamua kwa nia ya dhati kabisa.
 
Hata mimi nawashangaa sana watanzania.
Yaani vile vikarani vya dirishani vinawababaisha na kuona kama wakisema kitu ni sheria.
Halafu hao watu wanaoomba rushwa waziwazi hivyo mbona ni rahisi sana kuwakamata.
Unawapanga takukuru unawapa hela za moto ili iwe fundisho
Nchi hii ina raia wapumbavu Sana mtu haki yake anataka aje apiganiwe na Kiongozi hahahaha
 
Ndio hivyo sio kila kitu hadi serikali ije kukusaidia sasa watasaidia wapumbavu wangapi.
Mimi kawaida yangu huwa nawataimu miezi 6 ifike kama sheria yao inavyosema baada ya hapo huwa nakuwa mbogo hadi wenyewe wanaicheua pesa yangu,huwa sibembelezi kwenye pesa yangu mwenyewe.
Matanzania ni mapumbavu Sana hata awe na elimu ya PhD bado unamkuta kakaliwshwa kwenye mbao za nssf anadanganywa.

Mimi nilimaliza kazi sehemu flani ikabidi niombe pesa yangu nssf ubungo plaza , Kitu nilichokifanya sidhani Kama watasahau.
 
Matanzania ni mapumbavu Sana hata awe na elimu ya PhD bado unamkuta kakaliwshwa kwenye mbao za nssf anadanganywa.

Mimi nilimaliza kazi sehemu flani ikabidi niombe pesa yangu nssf ubungo plaza , Kitu nilichokifanya sidhani Kama watasahau.
Mkuu NSSF Ubungo Plaza kuna mama mmoja mweupe flani hivi, mfupi kiasi ana vidoti usoni. Tangu mwaka jana July nikienda kutafuta kadi ananambia mashine imeharibika, anataka kumaanisha hawajawahi toa kadi tangu nijiandikishe. Nikawa nawasikia wanapiga story za watoto wao wako Uturuki wanasoma.
 
Issue ni kwamba viongozi wahakikishe wametengeneza mifumo iliyo rahisi wameweka vyombo vitakavyohakikisha hakuna urasimu. Sasa wewe data za mwanachama waowanazo, wamempa kitambulisho na namba halafu wanaanza kumwambia sijuia alete barua toka serikali za mtaa, sijui kitambulisho cha uraia, birth certificate, mara afungue akauntinyingine, mara barua sijui ya nini.
Tanzania hakuna haki, inategemea unazungumzia haki kwa mtazamo unaomfurahisha nani. Ukitaka kujua kuwa hakuna haki hadi vyombo vya kusimamiahaki vinavunja haki mfano mtu anashikiliwa kituo cha polisi zaidi ya masaa 48 bila hata ndugu zake kuambiwa ana kosa gani.
SAsa kama data zako wanazo wewe kwanini usiseme data mnazo msinisumbue nipeni hela zangu. Sikia wewe mimi huko napajua na nimechukua visent vyangu si Mara moja.

Tatizo la wabongo ni uoga na ujinga ... Mitanzania mingi Ni mijinga hata awe na madegree hata 100 ila Kuna ule ujinga wa asili. Na kupitia huu ujinga ndio mtaji mkubwa wa hawa wapuuzi .

Kama unajua umekamilisha kila kitu kwanini utumwe vitu vingine... fanya reasoning sio unapelekwa Kama limbuzi. Vitu vingine kataa sema unataka kuonana na Meneja wa tawi ukifika ndani washa moto acha uoga.

Haki haijawahi kuombwa unaitafuta Tena kwa Damu na jasho. Sio mnakaa kulia Lia tu. Hakuna nchi mabadiriko yamefanywa na viongozi tu lazima wanachi muwe sehemu ya hayo mabadiriko.

Hata viongozi wajitahidi vipi kuweka system vizuri Kama wewe raia hutaki kuwa sehemu ya kufanikisha hayo mabadiriko hakuna litakalotokea.
 
Back
Top Bottom