Hivi Serikali inajua rushwa inayoendelea kwenye shirika la Hifadhi ya Jamii?

Watanzania wengi ni waoga sana na tumezoea maisha ya connection. Huwezi nipotezea muda wangu kwa upuzi.

Mwambie aende aseme sasa imetosha. Ainane na manager na ikishindikana aende makao makuu. Haki ya mtu hupiganiwa na kutafutwa kwa nguvu zote.
 
Bila serikali kuingilia watakaoweza kupigania haki yao ni wachache.
Kwani serikali imeshindwa kufanya haya mashirika yatoe haki pasipo watu kupigania au kutumia nguvu?

Hivi ukiwa na mtoto tahira utamuacha tu aonewe au utamjengea mazingira ya kumwezesha kumudu kuishi kwa urahisi zaidi?
 
Fika pale washa moto nenda kwa meneja washa Moto kuwa Kama mbogo uone Kama kadi hupewi.

Ikifikia kipindi raia wakiwa agressive hata wao wanapata funzo kuwa Hawa maraia sio wa kuchezea.
 
Mimi sijawahi kuweka ela NSSF wala kokotekwakuwa sijawahi ajiliwa serikalini wala sekta binafsi toka nianze kujitegemea. Ila hiki nikilio cha wengi kuanzia ndugu marafiki na wengine.

Ninalosikia ukmbishia anageuza shingo anaacha hata kukusikiliza au anaita mlinzi akurushe nje. Watu wanalalamika sana huyo meneja utamwona wapi bank wakati hawakuruhusu hata uingie. Umesahau wabongo uwa hawapendi umuone boss.
 
Ndio maana hii nchi haitakuja kuendelea kwa kuwa na raia wapumbavu sampuli yako. Mtanyanyasika sana na utasubiri Sana uwe unapiganiwa haki zako na Serikali. Endelea kusubiri tu.

Kuna Haki na wajibu , kasome wajibu wako Kama raia na sio kutaka haki zako tu wakati wajibu wako kama raia wa kukemea uovu maofisini hutaki kufanya.

Utasubiri saaaaaaaana
 
Unaongea vitu hata huvijui.

Endelea kulia na kukuza upumbavu kwa hao ndugu zako. Naomba nssf waendelee kuwakandamiza kisawa sawa maana ukoo wenu mzima ni mabogus
 
Unaongea vitu hata huvijui.


Endelea kulia na kukuza upumbavu kwa hao ndugu zako. Naomba nssf waendelee kuwakandamiza kisawa sawa maana ukoo wenu mzima ni mabogus
Asante ndugu kutoka ukoo wa wenye maakili
 
NInakuuliza tena serikali imeshindwa kumanage taasisi zake zikatoa haki bila watu kutumia nguvu? Au utaratibu ni mpaka kila mtu atumie nguvu?
 
Dawa yao ni kuwapa hela za moto tu,kama hawajakuonea huruma nao pia hupaswi kuwaonea huruma.
 
Hivyo kumbe imekuwa ni mojawapo ya utaratibu uliohalalishwa kama mojawapo ya procedures?
Ni ujinga pesa uliyoisotea halafu umpe mtu rushwa wachukue hatua ikiwemo kuwapeleka mahakamani wameua ssra makusudi
 
Sikiliza nikwambie mkuu.
Watu wabaya au wala rushwa hawawezi kuisha wapo kila mahali popote duniani hata uende marekani.
Cha msingi ni wewe raia mwenyewe ujitambue.
Sasa wewe karani wa dirishani anakuzubaisha kukwambia lete akaunti yako,na wewe unaitikia wakati unajua akaunti ulishapeleka halafu unashindwa kumwambia,halafu ukitoka hapo eti ukamsemshitaki kwa serikali kisa alikwambia ulete akaunti mara 2.
 
Ila una point ya msingi.
Ila tatizo ni kubwa sana wanasumbuka watu wengi sana. Unahisi huo uoga ni hulka ya mtanzania, elimu au ni kitu gani? Kwanini wengi ni waogoa na wachache ndiyo wana ujasiri?
 
Utopolo people wapo Tanzania na ni endemic kwa Tanzania. Poleni mikia endeleeni na utopolo
 
Nawapongeza sana kwa jumbe zenye jazba tuendelee hivi hivi ili hawa mautopolo wazinduke, bora mbwai iwe mbwai, wakati mwingine nendeni maofisini na vibuyu akizingua unaongea na wajuba, unakuwaje na smart phone unaingia ofisi za serikali kwa Mambo ya maana bila kurekodi mazungumzo tena kuanzia getini ukiingia mpaka getini wakati wa kutoka simu inarekodi na unajipanga kwa sauti ya juu, tuache ujinga ujinga, tuamke tuamke, jua lile lile tutelemke mamaa ..........hamjaimba huu wimbo don't be utopolo wake up please.
 
toa taarifa TAKUKURU haraka , kuna namaba ya bure siikumbuki lkn utashughulikiwa haraka,
 
Ni unyonge wa hali ya juu..
 
Safi sana watu wanakuwa wazembe sana kudai haki zao
 
Sasa wewe unakubali vipi kila siku unaambiwa mashine mbovu unakubali.
Ni haki yako kujua hiyo mashine imeharibikaje,tangu lini,na lini itakuwa tayar kurekebishwa,muhusika wa kutengeneza hiyo mashine yuko wapi?anafanya nini kwa sasa?kwa nini asiitengeneze kwa wakati huu?Una wajibu wa kuuliza hivi kwa sababu hizo mashine zinanunuliwa kwa kodi zetu.
Ukiwauliza haya maswali hawatakupa tena majibu ya kimbumbumbu,watakupa kitambulisho chako kwa haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…