GENTAMYCINE ( alias East African Brain ) ni Mkristo tena wa Dhehebu la Katoliki ila leo hii ( Usiku huu ) bila ya Unafiki nasema wazi kuwa Ndugu zetu Waislamu ni Watu Waungwana, Wastaarabu na Wavumilivu sana, ila Wakristo ni Wanafiki na Wabinafsi mno.
Nina uhakika wa 100% kuwa Waislamu nao wangekuwa Wanakesha Kuabudu huko Misikitini Kwao kwa Kupiga Kelele kama za Makanisani Kwetu Wakristo kila Siku tungesikia Malalamiko dhidi yao na hata Wakristo kutaka Kuandamana kwenda Ikulu ili Mheshimiwa Rais azuie / awazuie.
Nichukieni ila Ukweli nimeshawapa.
Kwa heshima na taadhima naomba kusema wewe siyo MKRISTO! Ungekuwa mkristo ungeelewa wanachokifanya wakristo na usingetumia muda wako kugombana nao juu ya hizo unazoita kelele!
Katika Tanzania, kila mtu ana haki ya kuamini chochote! Wapo wanaoamini ushirikina, wapo wanaoamini mawe!, Wapo wanaoamini ng'ombe nk
Walokole walichagua kumuamini Mungu wa kweli! Kwakuwa Imani yao ni ya kweli na isiyo na mawaa siku zote hawaoni sababu ya kujifichaficha kama wafanyavyo wachawi! Wapo huru kuitangaza Imani yao ulimwenguni pote ili kila mtu na kila kiumbe asikie!
Ukiona walokole wameweka kambi mtaani kwako wamefanya hivyo kwa sababu maalumu! Bila shaka wametumwa kuokoa roho yako na Mungu mkuu na hawatanyamaza mpaka umpokee Yesu! Hizo kelele zinakuhusu wewe kwa 100%! Siku utakayompokea Yesu hautazisikia! Utakuta hapo mtaani ni wewe tu ndiyo unayepata shida na ni kwa sababu ya makandokando yako!
Ukiona kuna dhehebu halipigi kelele za kumtangaza Mungu wao kimbia! Siyo watu wema hao! Siku zote hatuwashi mshumaa na kuuficha la! Tukiwasha mshumaa lazima tuuweke juu ya meza ili uangaze nyumba nzima! Narudia, kama kuna dhehebu linawasha mshumaa kisha kuuficha chini ya kitanda kimbia hilo dhehebu!
Nakusihi, acha kujaribu kuuzima mshumaa wa Yesu! Ikikupendeza, kama umewashindwa, jiunge nao! Vinginevyo hama huo mtaa!