Hivi soka inayochezwa Ulaya na hii ya kwetu ni mchezo mmoja au inafanana tu?

Hivi soka inayochezwa Ulaya na hii ya kwetu ni mchezo mmoja au inafanana tu?

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Nitakataa mpaka kesho ukiniambia mechi za ligi yetu ya mpira wa miguu ni mchezo sawa na mpira wa miguu wa wenzetu tunaowaona kwenye Tv zile game za akina Mbappe, Messi na Ronaldo, adhani ni michezo miwili inayofanana tu, kama ilivyo soccer ya ufukweni nk.

Mbona hawa wa kwetu wote wanakimbilia mpira tu mpira na hawana nguvu.
 
Aina za soka zinatofautiana kulingana na mental ability, body physique, football technique n.k.

Mwisho wa siku zote ni soka kwa sababu zinasimamiwa na kanuni zile zile.
 
Nadhani unaiongelea hii ya yanga leo, ni mechi mbovu sana kwakweli
 
Labda tumuulize Nahodha wetu Samata maana yeye Kacheza Zote soka la Afrika na huko Ulaya..
 
Nadhani ubora wa viwanja ndio unaotofautisha, kwa maana sidhani kama ulaya huwa wanacheza kwenye vichuguu km mkwakwani stadium
 
Nadhani ubora wa viwanja ndio unaotofautisha, kwa maana sidhani kama ulaya huwa wanacheza kwenye vichuguu km mkwakwani stadium
Kwa hiyo ile mechi ya mkwakwani ikihamishiwa anfield au stanford bridge tutapata bonge la burudani
 
Absolutely true, kwa maana timu zetu sasa zinaweza kuweka mpira chini na kucheza kwa kuonana, rejea mechi zilizowai kuchezwa uwanja wa taifa Yanga vs Dodoma, Yanga vs Biashara, Yanga vs Simba mechi zote mbili za mwaka huu Simba vs Nkana, Simba vs Aly Ahly. Unaona kabisa timu zinaweza kucheza mpira Safi tatizo viwanja ndio vibovu sana. Hapo nadhani sijazungumzia kuhusu ubora kwa maana wewe umehoji ile ladha ya muonekano wa mpira wetu ukiulinganisha na ule uliokuwa ukiuangalia kwa kideo
 
Nadhani unaiongelea hii ya yanga leo, ni mechi mbovu sana kwakweli
Ungezungumzia viwanja ningekuelewa ila kusema yanga mbovu hapana

Yanga akiwa mbovu hakuna timu tanzania utakayo kuwa nzima.

Viwanja vinafanya mpira uonekane wa kipuuzi sana rejea mechi ya ruvu na mtibwa, costal na yanga kiukweli vile viwanja vina ubora hafifu mno Hadi kupelekea mpira kuonekana wa ajabu mno
 
Wachezaji wetu wana stress, hawana lishe bora, hawana skills, yaani wamo uwajani ili tu waandikwe magazetini
Wenye skills bongo Ni wengi Sana Tena Sana. Tatizo nguvu. Miili na misuli haikuandaliwa tangu utotoni kwa ajili ya kucheza mpira.

Hebu angalia miili ya wachezaji wa Zanzibar,utafikiri walikumbwa na utapiamlo.

Vipaji vipo lkn hawaandaliwi.
 
Nimetoka kuangalia hiyo ya yanga sasa naangalia ya liverpool vs brentford naona ni vitu viwili tofauti
labda kama umeuliza kujifurahisha mtu unafananisha ligi ya epl na nbc pl? kuanzia kwenye viwanja, uwekezaji wametuacha mbali sana yaani sawa na kumfananisha fei toto na iniesta
 
Ulaya wanatuzidi kila kitu, yaani sisi tunawazidi ujinga tu na kuwasingizia watu vyesi feki bila kusahau unafiki.
 
Tatizo la mpira wa kitanzania ni kutopewa nafasi hata ya kutuliza mpira..
Wachezaji wanafata mpira unapokwenda,,
Hawafati njia.

Wakati wachezaji wa ulaya wanapata nafasi ya kutuliza mpira na kufanya watakacho.

Huku kwetu bongo ukitaka kufanya kama Mbappe au Messi unavunjwa kiuno muda wowote na adui wa timu pinzani..
 
Back
Top Bottom