Hivi Tanzania kuna sehemu hawajui Kiswahili?

Hivi Tanzania kuna sehemu hawajui Kiswahili?

Mcqueenen

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
6,843
Reaction score
11,702
Hivi Bongo kuna sehemu gani kule ndani ndani, nyuma ya mlima unavuka pori, unaogelea mito yani ukifika unakuta kijiji kizima hata mmoja hajui Kiswahili?

Maana mimi naamini Tanzania ni kubwa sana,nyuma ya ile milima ya morogoro mjini (Udzungwa) au ile ya Mzumbe kule sidhani kama kuna watu.

Hata kama wapo ndo hao hata hawajui wako nchi gani.

Ni wapi unapajua wewe?
 
Mongwe kule kipindi nasoma mzumbe sekondari niliendapo mara moja moja... Watu wanajua kiswahili na vigodoro wanacheza waluguru hao.

Nakumbuka nilitoa mia mbili nikapewa karoti nyingi kwelikweli na ndizi nikapiga deshi lunch... Waluguru noma.
 
Kule Tangeni wanaongea kisukuma tu
 
Mongwe wapi? Ulivuka mlima kwa upande wa pili?
Dah mkuu...umenikumbusha mongwe kuna story ya jamaa fulani ivi aliniambia asili yake ni uko...jamaa ni tapeli wa changarawe anaitwa baba Francis
 
Dah mkuu...umenikumbusha mongwe kuna story ya jamaa fulani ivi aliniambia asili yake ni uko...jamaa ni tapeli wa changarawe anaitwa baba Francis
Mongwe bara bara hazipitiki kipindi cha mvua...kuna ndizi kibao ila kuzileta chini zikishawiva ndiyo kazi....

Nilishafika huko....
 
Mongwe bara bara hazipitiki kipindi cha mvua...kuna ndizi kibao ila kuzileta chini zikishawiva ndiyo kazi....

Nilishafika huko....
Dah!!mimi nilitaka kwenda kumfuatilia mjomba ake uyo tapeli,alisema mjomba ake ni mganga uko mongwe,,,halafu nasikia kule ukikaribishwa wanakupa kuku.
 
Mongwe wapi? Ulivuka mlima kwa upande wa pili?
Nop sikuvuka kiongozi...Tulikuwa wengi nia yetu ilikuwa kufika kilele cha mt.uluguru... Lakini tulipokaribia juu wengine wakaanza kuchoka na kuanguka anguka.. Walioshindwa safari tuliwaacha nyuma ila ilifika kipindi tukabaki wachache na muda uliyoyoma hivyo tukageuza kuwarudia wenzetu... Tukapita mashambani kwa waluguru ndo wakatupa hayo makaroti,ndizi wengine wakapewa hadi cabbage...Tukanywa maji tukaenda kilimahewa kushangaa shangaa baadaye tukarudi shule.
 
Hivi nyuma ya ule mlima kuna watu upande wa pili?
Ukiendelea kuelekea huko unatokea mkoa gani au nchi gani?
Nop sikuvuka kiongozi...Tulikuwa wengi nia yetu ilikuwa kufika kilele cha mt.uluguru lakini tulipokaribia juu wengine wakaanza kuchoka na kuanguka anguka.. Walioshindwa safari tuliwaacha nyuma ila ilifika kipindi tukabaki wachache na muda uliyoyoma hivyo tukageuza kuwarudia wenzetu. Tukapita mashambani kwa waluguru ndo wakatupa hayo makaroti,ndizi wengine wakapewa hadi cabbage, tukanywa maji tukaenda kilimahewa kushangaa shangaa baadaye tukarudi shule.
Mongwe mkuu kuna waluguru,sijui wamasai na wasukuma baadhi japo sikusikia kisukuma nilipoenda.
 
Ukienda sehemu hizi kuna BAADHI ya Watz hawajui Kiswahili. Longido, Monduli, Mbulu, Missenyi (waganda Kyaka), Kibondo, Kakonko, Kasulu. Mwisho kabisa nahisi 50% ya Wasukuma hawaongei Kiswahili.
 
Hivi nyuma ya ule mlima kuna watu upande wa pili?
Ukiendelea kuelekea huko unatokea mkoa gani au nchi gani?
Utatokea nchi hiihii ya tz... Moro hiyohiyo...Ila kuna jamaa alituambia eti kuna upande wa mlima ukivuka upande wa pili unatokea mjini halafu distance yake ni fupi sema kikwazo ni mlima tu... Ndo tulitaka tujue kama ni kweli au cheche coz ukiwa town unauona mlima vzr tu.
 
Back
Top Bottom