Hivi TARURA mmejiangalia na kujitathmini jinsi mnavyokamua wananchi pesa?

Hivi TARURA mmejiangalia na kujitathmini jinsi mnavyokamua wananchi pesa?

Chotti de Alba

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2013
Posts
348
Reaction score
106
Wadau. Salam.

Hivi TARURA mmejiangalia na kujitathmini jinsi mnavyokamua wananchi pesa?

Ngoja niwape scenario. Mfano mimi nimeenda kupaki gari pale makumbusho nje ya jengo la LAPF, Mdada wa parking kaniona kapiga picha kaniandikia deni. Baada ya kupiga picha yeye anaondoka anaenda upande mwengine. Mimi nakua nimeingia na kutoka in less than 30 minutes so obviously deni najua ni 500. Unapotoka, huyo dada wa maegesho humuoni maana anakua ana kazi ya kukagua hizo parking upande/sehemu nyingine. Unaondoka

Swali. Je? Ni wakati gani huyo dada anajua nimeondoa gari pale na kwamba deni ni 500 na halizidi hapo?

Je? Ni alama gani inayomuonesha kuwa ile gari pale imekaa nusu saa au masaa mawili? Anakadiria?

TARURA watu wamejikuta wana madeni hadi ya elfu tisini. Sio sawa. Kama serikali haina vyanzo vya mapato vinavyoeleweka ombeni donation wananchi tuwachangie kama watoto yatima. Tujue tu.

NB: mawakala na wasemaji wa serikali naombeni msije na majibu yenu ya lipa deni. Nimekuja niulize swali je bei za maegesho ni za makadirio? Kijana wa parking anajuaje gari imekaa muda kiasi flani ikiwa mda unatoka yeye anakua upande mwengine. ?

A21E414D-019D-47CD-971D-45FAC59FAF57.jpeg
 
Wanajamvi kuna kitu kimenitokea mimi Binafsi kuhusu hizi Fine za TARURA najiuliza kama kweli tuna Bunge linalojali maslahi ya Wananchi.

Mimi nilipaki sehemu watu wa TARURA wakaja kuweka hiyo parking fee ya 500 ila nilipowauliza Risiti wakasema sasa hivi hawatoi,nikawauliza nalipaje bila control namba wakasema nidownload application sijui inaitwa Semi huko playstore, nimeitafuta sijaiona.

Kutokana na pilika za Maisha nikasafiri,leo nimerudi imebidi nimtafute mtoza hizi fee wa Tarura aniangalizie Deni nilipe kama anaweza kunionyesha control number,kaniangalizia nikakuta Deni ni 31,500 eti kila wiki wanatoza Faini elf 10.

Nimejiuliza mambo gani haya hivi faini ya Tsh 500 kweli iwe elf 10 kwa wiki zaidi ya asilimia 1000 huko?na kila wiki wanapiga faini ina maana kwa mwezi mtu uliyechelewa kulipa mia 5 unalipa elf 40?Si uhuni na utapeli huu?

Bunge linakuwa wapi Masheria ya kinyonyaji kama haya yakipita.

Tunaomba Waziri wa Tamisemi ingilia kati ifanyike kampeni ya Elimu ya kutosha wananchi wajue hili balaa,wakati ule hakuna kilichofanyika.
 
Wanajamvi kuna kitu kimenitokea mimi Binafsi kuhusu hizi Fine za TARURA najiuliza kama kweli tuna Bunge linalojali maslahi ya Wananchi.

Mimi nilipaki sehemu watu wa TARURA wakaja kuweka hiyo parking fee ya 500 ila nilipowauliza Risiti wakasema sasa hivi hawatoi,nikawauliza nalipaje bila control namba wakasema nidownload application sijui inaitwa Semi huko playstore, nimeitafuta sijaiona...
Mbona ni Aibu kwa serikali. Mama Samia ameliona hili swala? Ameongea chochote? Sio sawa
 
Mimi nadaiwa 23,500 nimepaki sehemu tatu tu na hata sikuwa najua huu utaratibu, jana nimeona sehemu ikabidi nami niangalie chombo yangu, dah serikali imekuwa ya kihuni hii.
 
Mi nilishaamua silipi na wakanikamata mkamataji namshindilia ngumi mpaka nihakikishe anayapeba mapafu mkononi uhuni mwingi sana.
 
Labda ndio chanzo kipya cha mapato ,maana hawana hata wanalojua ni tozo tu, kuna jamaa wanalalamika magari yako mbeya yanadaiwa parking ya Dodoma, kuna ya Mwanza yanadaiwa parking ya Dar na hayajawahi hata kutoka katika mikoa husika.

Kuna jamaa zangu wanatamani hata wangezaliwa Ukraine sio Bongo, yaani kila kukicha kinaibuka kituko, huku mibunge inadai namba maalum za magari kwa kweli Mungu aingilie kati tu , mimi hatua inayofuata baada ya kubeba boksi kwa muda ni kukana Uraia tu maana hakuna namna sasa.
 
Labda ndio chanzo kipya cha mapato ,maana hawana hata wanalojua ni tozo tu, kuna jamaa wanalalamika magari yako mbeya yanadaiwa parking ya Dodoma, kuna ya Mwanza yanadaiwa parking ya Dar na hayajawahi hata kutoka katika mikoa husika , kuna jamaa zangu wanatamani hata wangezaliwa Ukraine sio Bongo, yaani kila kukicha kinaibuka kituko, huku mibunge inadai namba maalum za magari kwa kweli Mungu aingilie kati tu , mimi hatua inayofuata baada ya kubeba boksi kwa muda ni kukana Uraia tu maana hakuna namna sasa.
Hamna bunge hapa!
 
Bora wizi wa kujengewa miundombinu kuliko wizi wa kuongezewa tozo hewa
 
Tutaelewana mdogo mdogo si mlikesha bar siku ya msiba ngoma bado mbichi ana miaka mitatu mbele.
 
Kwamba kila kitu kifike mezani kwa Samia?

Hakuna taasisi za kujitathimini?
Mama huwa anasoma mitandao ya kijamii. Ataliona hili. Naona wasaidizi wake wameshindwa kazi. Mama ataweza👏
 
Wadau. Salam.

Hivi TARURA mmejiangalia na kujitathmini jinsi mnavyokamua wananchi pesa?

Ngoja niwape scenario. Mfano mimi nimeenda kupaki gari pale makumbusho nje ya jengo la LAPF, Mdada wa parking kaniona kapiga picha kaniandikia deni. Baada ya kupiga picha yeye anaondoka anaenda upande mwengine...
Ushuru wa magari haujaanza leo wala Jana..

Uliambiwa kama huna pesa usinunue gari kwa kutaka wakuone,panda bajaji ..

Mwisho deni linakuwa kwa nini hulipi?
 
Mkubwa vita ya Urusi ndio imewafanya TARURA kuwa wanyama tena wa mwituni
 
Back
Top Bottom