Hivi Transcript ni haki ya Mwanafunzi kupatiwa na Chuo?

stow away

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2022
Posts
11,073
Reaction score
21,945
Naomba kuuliza wadau kuhusu hilo suala la transcript zinazotolewa vyuoni, hizi transcript ni haki ya Mwanafunzi kupatiwa na Chuo au ni mpaka mwanafunzi afukuzane na uongozi wa Chuo ndio wampe transcript?

Nasema hivi sababu kuna Chuo X kilichopo maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam kinamzungusha mwanafunzi kumpa transcript yake huu unaenda mwaka wa Pili kila mwanafunzi akienda anaambiwa transcript haijaprintiwa bado Mara anaambiwa anaeprint hayupo amesafiri visingizio haviishi, sasa nauliza hizi transcript kutoka kwenye vyuo vyetu ni haki ya Mwanafunzi kupatiwa pale anapomaliza Chuo au ni mpaka aombe sana ndio apatiwe transcript yake ?!
 
Akomae apewe, ni chuo gani hiko chenye mbambamba namna hiyo khaaah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sawa mkuu, Chuo kipo hapahapa mkoa wa Dar es Salaam haina haja ya kukitaja Ila wanazungusha alafu ukiwa mfuatiliaji sana wanachukia na wanakua wakali km pilipili ndio maana nikakuuliza transcript ni haki au ni ombi ?
 
Sawa mkuu, Chuo kipo hapahapa mkoa wa Dar es Salaam haina haja ya kukitaja Ila wanazungusha alafu ukiwa mfuatiliaji sana wanachukia na wanakua wakali km pilipili ndio maana nikakuuliza transcript ni haki au ni ombi ?

Unaongeza tatizo kwa kutokitaja
Jina.acha kukumbatia udumavu wa akili fikiria nje ya box kijana
 
Taja jina la chuo usadike sio dhambi usiogope

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
Kuna mengi nitayaeleza baadae nikipata wasaa kuhusu huu mkasa Ila kwa sasa nilihitaji kujua km transcript ni haki au ni ombi, sasa km ni haki ikiwa km Chuo kimegoma kutoa transcript na kimeizuia, Mwanafunzi achukue hatua zipi ili apatiwe transcript yake ?
 
Kitaje,,,unazungumzia taasisi ya elimu. Itaje Kisha hiyo transcript atapewa.
 
Kitaje,,,unazungumzia taasisi ya elimu. Itaje Kisha hiyo transcript atapewa.
Mkuu km unajua hatua za kufuata ili ipatikane elezea maana hapo ndio panaleta utata wapi pa kuanzia? Mwanafunzi hana tatizo maana alipoenda wamecheck mbele ya msajiri km mwanafunzi ana tatizo wakasema mwanafunzi hana tatizo lolote Ila sasa transcript kutoa na kumpa ndio inakua ngumu maana ipo ndani ya laptop inaonekana na mara zote amekua akienda anaonyeshwa transcript yako ipo hii hapa Ila kuiprint ili apewe ndio anazungushwa achukue hatua zipi ili aweze kupatiwa? Sio Chuo Cha kata ni Chuo cha Serikali
 
Transcript ni matokeo yote ya chuo kwa mihula na miaka yako. Na ni haki yako sio ombi, kama inazuiliwa basi clearance haijakaa sawa yaweza kuwa unadaiwa bado lakini mdaiwa anatoa ubishi kuwa hadaiwi, hapo huwezi kupewa. Fanya clearance!

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…