Naomba kuuliza wadau kuhusu hilo suala la transcript zinazotolewa vyuoni, hizi transcript ni haki ya Mwanafunzi kupatiwa na Chuo au ni mpaka mwanafunzi afukuzane na uongozi wa Chuo ndio wampe transcript?
Nasema hivi sababu kuna Chuo X kilichopo maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam kinamzungusha mwanafunzi kumpa transcript yake huu unaenda mwaka wa Pili kila mwanafunzi akienda anaambiwa transcript haijaprintiwa bado Mara anaambiwa anaeprint hayupo amesafiri visingizio haviishi, sasa nauliza hizi transcript kutoka kwenye vyuo vyetu ni haki ya Mwanafunzi kupatiwa pale anapomaliza Chuo au ni mpaka aombe sana ndio apatiwe transcript yake ?!
UKWELI MCHUNGU.
Kwa vyuo vingi vyenye LEVEL YA DPLM na vilivyo chini ya NACTE mwanafunzi anaposajiliwa taarifa zake huenda NACTE na matokeo yake hujazwa NACTE.
Kila mtihani wa kumaliza NTA LEVEL moja kwenda nyingine matokeo hutumwa NACTE na kujazwa katika MFUMO WA NACTE.
Ili baada ya kumaliza mwanafunzi matokeo huwa NACTE ili baadaye apewe AVN ( AWARD VERIFICATION NUMBER) namba hii ndiyo hutumika kuombea chuo kikuu kama unajiunga na ndiyo huwa utambulisho wa NACTE kuwa wewe ni mhitimu.
PICHA INAANZA HIVI.
Vyuo vingi huwa na janja janja kwa kusajiri wanafunzi nje ya muda hususani vya private, baada ya kumsajili mwanafunzi huendelea kusoma na matokeo yake anapata
LAKN ANAKUWA NACTE HAKUSAJILIWA NA TAARIFA ZAKE HAZITUMWI KULE, NA KUNA MUDA WANASHINDWA KUMUINGIZA NACTE COZ WALIMSAJILI KWA JANJA JANJA.
Cheti kinatolea na CHUO na si simple tu hakina mbambamba lakini TRANSCRIPT hii kitu haina ujanja lazima iwe na muunganiko na matokeo yake NACTE
Sasa chuo kama kilishindwa kumsajili NACTE na kilikuwa hakitumii matokeo yake HAPA JUWA UMEPIGWA.
Nimeandika kwa uzoefu na nimeona kwa macho.
Kukupa cheti siyo issue ila transcript hii haina uongo wala kufoji lazima ujisalimishe NACTE.
USHAURI.
Hakuna sababu yoyote ya kumnyima mtu transcript kama hakuna shida nyingine.
Vyuo vinajuwa watanzania wengi akifatilia kitu huwa anakata tamaaa.
MAMBO YA KUFANYA.
1. Kama uliyeandika ni mzazi NENDA CHUONI, onana na msajili kuwa mkali wakazie mwanzo mwisho.
2. Baada ya kutoka kwa msajiri nenda kwa Mtaaluma mkazie balaa.
3. Baada ya hapo nenda kwa mkuu wa chuo, PS akikukatalia komaa mpaka uingie.
4. Ukiona hujapata majibu NENDA NACTE
Ukienda nacte kama ni chuo kilicho chini ya mfumo wa NACTE huko ndiyo utaambiwa kwenye mfumo yupo au hayupo.
AU
CHUKUA NAMBA YAKE YA USAJILI UOMBE
AWARD VERIFICATION NUMBER,
Kama matokeo yake yapo NACTE itakwambia kama hayapo mfumo utakwambia pia.
Kuomba namba hiyo ya AVN ni rahisi ingia website ya NACTE utakuta utaratibu na unalipia kati ya elfu 3 au elfu 10.
FANYA HIVO UTAPATA JIBU SAHIHI.