Hivi Transcript ni haki ya Mwanafunzi kupatiwa na Chuo?

Kuna shida mahali na pa kuanzia ni kwa Mkuu wa chuo

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Kitaje jina hicho chuo kumzungusha mtu kwa miaka miwili ni uzembe uliopitiliza, ndani ya miaka miwili angeweza kupata ajira, kujiendeleza kielimu n.k. Hiyo kitu ingemkuta mtu mtata unaenda kufungua kesi mahakamani upewe transcript na ulipwe fidia. Tatizo inawezekana huyo anayedai ana uoga mwingi ndio maana anazungushwa.
 
Mkuu haujaelewa Cheti hupewi km hujafanya clearance, cheti wametoa Ila transcript wameizuia maana clearance ilishafanyika na msajiri alishasaini mwanafunzi hana tatizo lolote na wakicheck taarifa za mwanafunzi km ana tatizo lolote inaonyesha mwanafunzi hana tatizo lolote na walishathibitisha mbele ya msajiri Ila kumpatia transcript yake mwanafunzi ndio kuna mvutano, achukue hatua zipi? Elezea hatua za kufuata km unazijua mkuu
 
Mkuu wa chuo anajua? Kwanini kama hana tatizo wamzuilie? Be specific shida ni nini ili tukusaidie. Haileti sense mwanafunzi hana tatizo halafu anyimwe transcript.

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Itakuwa wanataka rushwa period.
 
Nenda kwa mkuu wa wilaya husika inapigwa simu Moja tu itaprintiwa hata saa Tano usiku
 
Taja chuo wewe
 
Safari ni ndefu saana. Mhitimu chuo hajui kama transcript ni haki yake?? Afanye nini kuipata??

Jinyonge tu. Kabla ya kufa, wadai Ada yako wakulipe
 
Mkuu wa chuo anajua? Kwanini kama hana tatizo wamzuilie? Be specific shida ni nini ili tukusaidie. Haileti sense mwanafunzi hana tatizo halafu anyimwe transcript.

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
Sijafahamu km mkuu wa Chuo anajua, kuhusu kwanini km mwanafunzi hana tatizo kwanini wamzuilie hilo swali hata Mimi najiuliza, kwanini wazuie transcript km mwanafunzi wanasema wenyewe kua hana tatizo na wamethibitisha mbele yake mwanafunzi na mbele ya msajiri kua huyu mwanafunzi hana tatizo lolote baada ya kukagua taarifa zake zinaonyesha mwanafunzi hana tatizo lolote Ila transcript kwanini hawampi? Hilo swali pia mimi najiuliza
 
Una uhakika na anayosema mwanafunzi wako? Ysmkini anakudanganya nenda mwenyewe kajiridhishe ndo ujue cha kufanya.

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
UKWELI MCHUNGU.

Kwa vyuo vingi vyenye LEVEL YA DPLM na vilivyo chini ya NACTE mwanafunzi anaposajiliwa taarifa zake huenda NACTE na matokeo yake hujazwa NACTE.

Kila mtihani wa kumaliza NTA LEVEL moja kwenda nyingine matokeo hutumwa NACTE na kujazwa katika MFUMO WA NACTE.

Ili baada ya kumaliza mwanafunzi matokeo huwa NACTE ili baadaye apewe AVN ( AWARD VERIFICATION NUMBER) namba hii ndiyo hutumika kuombea chuo kikuu kama unajiunga na ndiyo huwa utambulisho wa NACTE kuwa wewe ni mhitimu.

PICHA INAANZA HIVI.

Vyuo vingi huwa na janja janja kwa kusajiri wanafunzi nje ya muda hususani vya private, baada ya kumsajili mwanafunzi huendelea kusoma na matokeo yake anapata

LAKN ANAKUWA NACTE HAKUSAJILIWA NA TAARIFA ZAKE HAZITUMWI KULE, NA KUNA MUDA WANASHINDWA KUMUINGIZA NACTE COZ WALIMSAJILI KWA JANJA JANJA.

Cheti kinatolea na CHUO na si simple tu hakina mbambamba lakini TRANSCRIPT hii kitu haina ujanja lazima iwe na muunganiko na matokeo yake NACTE

Sasa chuo kama kilishindwa kumsajili NACTE na kilikuwa hakitumii matokeo yake HAPA JUWA UMEPIGWA.


Nimeandika kwa uzoefu na nimeona kwa macho.

Kukupa cheti siyo issue ila transcript hii haina uongo wala kufoji lazima ujisalimishe NACTE.

USHAURI.

Hakuna sababu yoyote ya kumnyima mtu transcript kama hakuna shida nyingine.

Vyuo vinajuwa watanzania wengi akifatilia kitu huwa anakata tamaaa.

MAMBO YA KUFANYA.

1. Kama uliyeandika ni mzazi NENDA CHUONI, onana na msajili kuwa mkali wakazie mwanzo mwisho.

2. Baada ya kutoka kwa msajiri nenda kwa Mtaaluma mkazie balaa.

3. Baada ya hapo nenda kwa mkuu wa chuo, PS akikukatalia komaa mpaka uingie.

4. Ukiona hujapata majibu NENDA NACTE

Ukienda nacte kama ni chuo kilicho chini ya mfumo wa NACTE huko ndiyo utaambiwa kwenye mfumo yupo au hayupo.

AU

CHUKUA NAMBA YAKE YA USAJILI UOMBE

AWARD VERIFICATION NUMBER,

Kama matokeo yake yapo NACTE itakwambia kama hayapo mfumo utakwambia pia.

Kuomba namba hiyo ya AVN ni rahisi ingia website ya NACTE utakuta utaratibu na unalipia kati ya elfu 3 au elfu 10.

FANYA HIVO UTAPATA JIBU SAHIHI.
 
Una uhakika na anayosema mwanafunzi wako? Ysmkini anakudanganya nenda mwenyewe kajiridhishe ndo ujue cha kufanya.

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
Siwezi nikashindwa kuamini km kungekua na tatizo hata Cheti asingepewa wangezuia na cheti pia kwanini transcript?
 
Sawa mkuu nauchukua ushauri wako,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…