Hivi Transcript ni haki ya Mwanafunzi kupatiwa na Chuo?

Cheti ni cover tu na unapewa kama hujafeli domo lolote ila transcript ni MATOKEO yako ya chuo na hiyo ni muhimu zaidi na inazuiliwa kama una deni chuoni.

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
Mkuu matokeo yake yapo clean hakuna alipofeli na wamethibitisha hilo hivi unanielewa lakini ninachokwambia kua wamekagua kuhusu kuanzia matokeo na kila kitu km mwanafunzi anadaiwa na Chuo wamekuta mwanafunzi hana tatizo na wala Chuo hakimdai mwanafunzi, issue ni KUPRINT transcript na kumpatia tu hapo ndio kuna mvutano kuiprint hio transcript ndio danadana zinaanzia hapo
 
Ni haki yako, baadhi ya vyuo unalipia 10k bank unapeleka payslip wanakuprintia chap
 
Mkuu unatuchosha si waulize kwanini hawaptint? Au wanaprint kwa pesa? Shida iliyopo kwako ni ROHO ya unyonge, waulize kwanini wakupe sababu

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Ni haki yako, baadhi ya vyuo unalipia 10k bank unapeleka payslip wanakuprintia chap
Sasa km kuna issue ya kulipia mboni hawajawahi kusema kuhusu hilo maana nijuavyo Mimi transcript inalipiwa moja kwa moja kwenye ada na ada yote ilishalipwa mwanafunzi hadaiwi hata shilling 1 na Chuo,
Mkuu unatuchosha si waulize kwanini hawaptint? Au wanaprint kwa pesa? Shida iliyopo kwako ni ROHO ya unyonge, waulize kwanini wakupe sababu

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
Sawa mkuu, wanasema ameshapewa taarifa zako anaetakiwa kuprint atakuprintia tu subiri kila akienda kuangalia km tayari ishaprintiwa wanamwambia bado bado haijaprintiwa subiri itaprintiwa tu huku siku zinaenda
 
Waulize taratibu za kuprintiwa lazima kuna malipo kidogo kama wafanyavyo vyuo vingine.

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Waulize taratibu za kuprintiwa lazima kuna malipo kidogo kama wafanyavyo vyuo vingine.

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
Mkuu km kungekua na MALIPO wangesema tangu awali hawajawahi kusema hivyo na km ni inalipiwa wangesema na wangetoa control number Ila hakuna huo utaratibu wa kuilipia transcript
 
Nenda Mahakamani.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Ungekitaja ili wajirekebishe.
Kusema chuo X na kutoa malalamiko hapa hautapata msaada wowote.
 
Ukotaja jina watokuja huku kusema unakiaibisha chuo, kua mpole kijana fuatilia kiupole watakupa nl haki yako
 
Sawa mkuu, Chuo kipo hapahapa mkoa wa Dar es Salaam haina haja ya kukitaja Ila wanazungusha alafu ukiwa mfuatiliaji sana wanachukia na wanakua wakali km pilipili ndio maana nikakuuliza transcript ni haki au ni ombi ?
🤣🤣🤣Usikute ni .... hao,mie nilikomaa hadi wakanipa,ila ilikuwa mtiti,na ni kero,eti walikuwa wanauliza ulikuwa wapi miaka yote hiyo?like what the f.ck?kwani kuna time limitation ya kutoa transcript?
Mimi nilipoajiriwa awali walipokea cheti tu,hawakuhitaj transcript,sasa nataka hamia organization x wanataka transcript,ilikuwa nkazeze.
 
Nidm jina la chuo nikukonect upate, kama ndiko nilikosoma.
 
MIMI nilihitimu Chuo Y kipo mkoa wa Tanga, Lushoto hakukua na longolongo za hivi unapewa Cheti na transcript hapo hapo unasaini unaenda zako bila kuzungushana, sasa nimeshangaa hiki Chuo X mbona kina taratibu za ajabu kiasi hiki yaan transcript tu ndio kuzungushana na mwanafunzi namna hii kwanini ?
 
Taja jina la chuo ili upate ufumbuzi,yawezeiana kuna wengine wamo humu walipitia chuo hicho wakafanyiwa hivyo na wakatumia njiwa ya kupata kwa urahisi,kutaja jina la chuo sio kosa kwako,sabau hiyo ni taasisi ya elimu,na wengine wanaosoma hapo una waanda wajue kitakachowapata.
 
Sawa mkuu, Chuo kipo hapahapa mkoa wa Dar es Salaam haina haja ya kukitaja Ila wanazungusha alafu ukiwa mfuatiliaji sana wanachukia na wanakua wakali km pilipili ndio maana nikakuuliza transcript ni haki au ni ombi ?
Haki ya mwanachuo baada ya kuhitimu, na pale akisha clear kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…