Hivi Transcript ni haki ya Mwanafunzi kupatiwa na Chuo?

Nashangaa hiko chuo kutompa mwanafunzi transcript yake, khaaah
 

πŸ˜‚ si useme tu ni TPSX YZ unahofu nini ndugu??
 
mmh, kuprint haiizidi hata lisaa kwanini asisubiri? kuna shida mahali
 
Boraa wee umefafanua vizuri hapaa.
 
Sio Chuo hicho mkuu, Wala sio hicho
Basi hiko wanafunzi wake wanalalamika kwelikweli mtaani hawapewi kila siku ni njoo ijumaa.


Hiko chako kitaje hapa kama kweli unahitaji msaada
 
Basi hiko wanafunzi wake wanalalamika kwelikweli mtaani hawapewi kila siku ni njoo ijumaa.


Hiko chako kitaje hapa kama kweli unahitaji msaada
Sasa si bora hio njoo IJUMAA Ina uafadhari, unaambiwa wewe nenda tutawasiliana huambiwi ni IJUMAA au JUMATATU we kasubiri tutaendelee kuwasiliana, ukienda tena Chuoni baada ya wiki ukiwaambia nmefuata transcript hawakukumbuki hata kidogo unaanza tena upya na moja kujielezea Mimi ni fulani fulani ilikua hivi na hivi nilikuja hivi na hivi ikawa hivi na hivi process zinaanza upya hawajafanya chochote issue ipo vile vile hakuna transcript iliyoprintiwa wanakwambia nenda tutawasiliana siku zinaenda tu, sasa hii ni haki ya mwanafunzi au inabidi mwanafunzi sasa aandike barua ya maombi ya kupatiwa transcript yake kwenda kwa mkuu wa Chuo husika au ?
 

HOngera sana kwa uvumilivu, endelea kukaa kimya ukivumilia huku siku zinaenda.

Ingelikua mimi mwezi mmoja tu naambiwa nenda rudi nahamia kwa mkuu wa chuo
Wiki 1
Wiki inayofuata ni barua na file nabeba hadi kwa ofisi kuu ya serikali inayohusika πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hii nchi bila kusemeana kwa wakubwa hawa wa chini hawatimizi majukumu yao.
Yani kitu cha kuprint dk 1 nisumbuke mwaka??
 
Uvumilivu una mwisho mkuu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…