Waapii, ni kwamba vyombo vyenu vya habari vimetiwa ndani ya mtungi havisemi, vipo kimya, havina uthubutu na usemi kama vya Kenya. Kwenu utekaji mbona issue ya kawaida sana akina Ben Saanane na wengine wengi ambao tunaona wakitajwa Jamii Forums, maana vyombo vya kawaida vimeingiwa hofu, visije vamiwa na Makonda kama alivyofanya akina SHILAWADU.
Hili la MO lilikua limewatoa jasho sana nyie miCCM wa mitandaoni, naona mtapata afueni maana mumetengezewa pa kutokea baada ya hizi nyuzi mnaanzisha za kuelekeza pua Kenya. Watanzania walivyo na ile herd mentality waliyorithi kutoka ujamaa watafuata mkumbo bila kuhoji, hivyo mtapumzika, lakini kiaina mpira unaweza kurudi huko huko, labda mpumzike siku chache tu.