Uchaguzi 2020 Hivi Tundu Lissu akishindwa mtafanya nini?

Uchaguzi 2020 Hivi Tundu Lissu akishindwa mtafanya nini?

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Poleni wanasiasa wa pande zote.

Nimekaa naangalia matukio ya kisiasa yanayoendelea nchini kwanzia upinzani hadi chama tawala. Upande wa CCM hawana 🔥 sana sababu wanajua ushindi ni uhakika na lazima.

Upande wa upinzani wamejitoa ufahamu kabisa wamesahau mbinu CCM wanazotumia kushinda wamesahau kuwa bado tuko na tume ileile ya miaka yote hasa ya 2015. Ww mpizani unashindia wapi wakati matokeo hayatangazwi hata na radio za nje tena?.

Kwanini msijiandae kisaikolojia kama mkishindwa ni sawa tu? Nasikitika sana mtu kupoteza muda kwenye box la kura wakati mshindi anajualikana.

Haya tuseme Lissu kashashindwa wewe mpiga kura na mnazi wa upinzani utafanya nini? Mtanzania action ya kwanza ni kukimbia kwenye kicharazio cha simu yake na kuanza kulalamika mitandaoni basi,hakuna zaidi ya hapo. Anaejua mbinu ingine aitaje?

Mimi niliacha siasa toka 2015 toka Edo alivyoshindwa akawauza watu.
 
Waambie baba CCM wapo nyuma ya pazia wanapanga yao wao wapo huku wanapigishana kelele na wananchi utadhani wananchi wanaamua kumbe kuna kikundi cha watu wapo eneo ndio waamuzi wakuu hawa wakitaka kukupora jimbo ni dakika tu.
 
Poleni wanasiasa wa pande zote.

Nimekaa naangalia matukio ya kisiasa yanayoendelea nchini kwanzia upinzani hadi chama tawala. Upande wa ccm hawana 🔥 sana sababu wanajua ushindi ni uhakika na lazma.

Upande wa upinzani wamejitoa ufahamu kabisa wamesahau mbinu ccm wanazotumia kushinda wamesahau kuwa bado tuko na tume ileile ya miaka yote hasa ya 2015. Ww mpizani unashindia wapi wakati matokeo hayatangazwi hata na radio za nje tena?.

Kwanini msijiandae kisaikolojia kama mkishindwa ni sawa tu? Nasikitika sana mtu kupoteza muda kwenye box la kura wakati mshindi anajualikana.

Haya tuseme Lissu kashashindwa ww mpiga kura na mnazi wa upinzani utafanya nini? Mtanzania action ya kwanza ni kukimbia kwenye kicharazio cha simu yake na kuanza kulalamika mitandaoni basi,hakuna zaidi ya hapo. Anaejua mbinu ingine aitaje?

Mimi niliacha siasa toka 2015 toka Edo alivyoshindwa akawauza watu.
Ni wazi kwa joto lililopo huku mtaani Lissu ATASHINDA kwa over 60% isipokuwa anaweza KUTOTANGAZWA.

kifuatacho?

hata mimi sijui.... so, naungana na wewe kuuliza swali kama lako!
 
Hapo tu ndiyo huwaga mnajidanganya kwanza mngejua jpm hawasikilizi kabisa hao beberu wenu mtawaita mbuzi mwaka huu hatishwi na kelele za chura hizo.
Ikawaje sasa akarekebisha sheria juu ya Arbitration? Si ameishia kusalimu amri na kuruhusu zifanyike mahakama za kimataifa sio Tz pekee.

Sema tu ana jeuri ila sio kwamba eti amewa defy. Kma ana hyo jeuri kwanini aliomba mabeberu wamfutie madeni kisa Corona? Kwanini aliomba mabeberu waje kwenye utalii sababu Corona imeisha? Si angesema tu hahitaji pesa zao.

Hya aliwaita Barrick wezi ila ameishia kuwa mbia wao? Si angewafutia kibali tu aanzishe kampuni ya weusi watupu?

Haingii akilini unasema wanakuhujumu afu hapo hapo SGR unajenga kwa mikopo yao na wakandarasi wao.

Waliosema ameingia uchumi wa kati ni hao hao mabeberu na ccm mkaanza kelele mitandaoni. Hvi mtu anayewahujumu mnakubali vp takwimu zake?

Magufuli mnamkuza sana ila sijaona hta kimoja alichowaweza hao "Mabeberu"
 
Poleni wanasiasa wa pande zote.

Nimekaa naangalia matukio ya kisiasa yanayoendelea nchini kwanzia upinzani hadi chama tawala. Upande wa CCM hawana 🔥 sana sababu wanajua ushindi ni uhakika na lazma..

Vichekesho vingine bwana ni hatari sana. Ww unasema uliacha siasa kwa sababu alizozitaja, halafu unawashauri wengine wawaachie tu ccm kisa ww ulishakata tamaa!

Ni sawa na kama umefeli mtihani wa hisabiti kwakuwa hukuwa na mwalimu mzuri, kisha utake na wengine waachane na hilo somo kwa matamanio yako.

Kama wewe umeacha siasa, nenda jukwaa la mapenzi, waachie wanaotaka kuendelea na siasa. Huyo aliyekuagiza kuwa mbinu hii itawabeba ccm, mwambie watu wameishia kukuchora tu.
 
Vichekesho vingine bwana ni hatari sana. Ww unasema uliacha siasa kwa sababu alizozitaja, halafu unawashauri wengine wawaachie tu ccm kisa ww ulishakata tamaa! Ni sawa na kama umefeli mtihani wa hisabiti kwakuwa hukuwa na mwalimu mzuri, kisha utake na wengine waachane na hilo somo kwa matamanio yako. Kama wewe umeacha siasa, nenda jukwaa la mapenzi, waachie wanaotaka kuendelea na siasa. Huyo aliyekuagiza kuwa mbinu hii itawabeba ccm, mwambie watu wameishia kukuchora tu.
Alichoeleza jamaa ni ukwel mchungu
 
Lisuu anapigwa chini, magufuli Anachukua nchi

Hakuna mtakachokifanya chadema

This is life, this is the world
 
Lissu sio wa kusema hewala bwana. Na magu akitumia silaha za moto ICC na mabeberu wanakuja.
Tunajua mabeberu watakuja kuiba mali na utajiri wetu waliowekewa ngumu na Rais wetu kipenzi na Mzalendo nambari wani, Rais Magufuli. Ila wambie wakija kwa shari watakiona Zaidi ya kile kilichowapata huko Mashariki ya mbali na huko Afghanistan. Sisi siyo wale wakutishiwa na mabeberu. Tuko tayari kuifia Tanzania wakati wengine wakipanda ndege na kuelekea Ubelgiji waliko ahidiwa UKIMBIZI NA UDAYASIPORA na kuwaacha wale anaowadanganya SOLEMBA!
 
Poleni wanasiasa wa pande zote.

Nimekaa naangalia matukio ya kisiasa yanayoendelea nchini kwanzia upinzani hadi chama tawala. Upande wa CCM hawana [emoji91] sana sababu wanajua ushindi ni uhakika na lazima.

Upande wa upinzani wamejitoa ufahamu kabisa wamesahau mbinu CCM wanazotumia kushinda wamesahau kuwa bado tuko na tume ileile ya miaka yote hasa ya 2015. Ww mpizani unashindia wapi wakati matokeo hayatangazwi hata na radio za nje tena?.

Kwanini msijiandae kisaikolojia kama mkishindwa ni sawa tu? Nasikitika sana mtu kupoteza muda kwenye box la kura wakati mshindi anajualikana.

Haya tuseme Lissu kashashindwa wewe mpiga kura na mnazi wa upinzani utafanya nini? Mtanzania action ya kwanza ni kukimbia kwenye kicharazio cha simu yake na kuanza kulalamika mitandaoni basi,hakuna zaidi ya hapo. Anaejua mbinu ingine aitaje?

Mimi niliacha siasa toka 2015 toka Edo alivyoshindwa akawauza watu.

Inaelekea wewe uko kwenye mradi wa kutaka kumuepusha Magufuli na ukweli wa ushindani katika uchaguzi huu. Yaani asishuhudie ukweli wa matokeo halisi ya kura hata kama zitapuuzwa na yeye kutangazwa mshindi. Mtu aliye na “obsession” ya kupendwa, kusikilizwa peke yake na kuabudiwa hupata maumivu makali akijionea uthibitisho kuwa kiuhalisia anachukiwa na kudharauliwa sana. Na kwamba amezungukwa na wanafiki wachumia tumbo kibao ambao baadhi yao pia hushiriki “siri” ya kuficha matokeo halisi na kutumia mabavu kumtangazia ushindi feki.

Umesema kweli: CCM “watashinda kwa kishindo” lakini hawatakwepa maumivu ya “forgery” hiyo. Na duniani hakuna siri ya zaidi ya mtu mmoja. Hivyo, jua kuwa wapinzani hawajajitoa fahamu kama unavyofikiri, bali wanataka kutoa dozi kali ya maumivu kwa Magufuli na CCM yake pengine kuzidi chaguzi zilizopita ili kuongeza mtafaruku ndani ya chama na serikali vinavyosimama kwa nguvu ya dola. And, who knows? Labda huo muujiza wanaojinasibu nao wapinzani unaweza kutokea safari hii!

Kwa sisi wengine, haijalishi kama Lissu anatangazwa mshindi au la, bali ni ule msisimko wa mchakato wenyewe wa uchaguzi mkuu na “impact” yake kwa saikolojia ya watawala na Watanzania kwa ujumla. Ujio wa Lissu umechangamsha uchaguzi huu kwa namna yake. Vinginevyo tungeupuuza kabisa. Manake ingekuwa ni mwendo wa kuhubiriwa injili ya upande mmoja tu. Very boring. Hapa ndipo unapoweza kutumia ule usemi wa “raha ya safari ni mwendo, mandhari, mikao na mitikisiko njiani na SI kufika”.
 
Back
Top Bottom