stakehigh
JF-Expert Member
- Aug 9, 2019
- 7,134
- 4,556
Inaelekea wewe uko kwenye mradi wa kutaka kumuepusha Magufuli na ukweli wa ushindani katika uchaguzi huu. Yaani asishuhudie ukweli wa matokeo halisi ya kura hata kama zitapuuzwa na yeye kutangazwa mshindi. Mtu aliye na “obsession” ya kupendwa, kusikilizwa peke yake na kuabudiwa hupata maumivu makali akijionea uthibitisho kuwa kiuhalisia anachukiwa na kudharauliwa sana. Na kwamba amezungukwa na wanafiki wachumia tumbo kibao ambao baadhi yao pia hushiriki “siri” ya kuficha matokeo halisi na kutumia mabavu kumtangazia ushindi feki.
Umesema kweli: CCM “watashinda kwa kishindo” lakini hawatakwepa maumivu ya “forgery” hiyo. Na duniani hakuna siri ya zaidi ya mtu mmoja. Hivyo, jua kuwa wapinzani hawajajitoa fahamu kama unavyofikiri, bali wanataka kutoa dozi kali ya maumivu kwa Magufuli na CCM yake pengine kuzidi chaguzi zilizopita ili kuongeza mtafaruku ndani ya chama na serikali vinavyosimama kwa nguvu ya dola. And, who knows? Labda huo muujiza wanaojinasibu nao wapinzani unaweza kutokea safari hii!
Kwa sisi wengine, haijalishi kama Lissu anatangazwa mshindi au la, bali ni ule msisimko wa mchakato wenyewe wa uchaguzi mkuu na “impact” yake kwa saikolojia ya watawala na Watanzania kwa ujumla. Ujio wa Lissu umechangamsha uchaguzi huu kwa namna yake. Vinginevyo tungeupuuza kabisa. Manake ingekuwa ni mwendo wa kuhubiriwa injili ya upande mmoja tu. Very boring. Hapa ndipo unapoweza kutumia ule usemi wa “raha ya safari ni mwendo, mandhari, mikao na mitikisiko njiani na SI kufika”.
lowasa mwenye uzoefu wa ccm miaka karibia 50 amenawa mikono na yeye alikua ndan ya ccm , uyo mbuzi anaepungia miti ndo unasema amechangamsha uchaguzi? mbna mshindi anajulikana mpaka 2100