Uchaguzi 2020 Hivi Tundu Lissu amepewa ulinzi na Serikali?

Uchaguzi 2020 Hivi Tundu Lissu amepewa ulinzi na Serikali?

KAMA NI YEYE KWELI. SASA WAKATI WA MABOMU NA MAWE ANAKUWA WAPI? MAANA NAONA LISSU AKISIMAMA MBELE NA KUJITETEA PAMOJA NA KUWAHOJI POLISI PEKE YAKE, NANI ANAMLINDA MWENZAKE HAPO?
Kwa sasa hivi hamna mtu atamrushia Lissu jiwe abaki salama, siyo lisu tuu hata rungwe...unda chama chako upate hiyo privilege kwa miezi 2
 
View attachment 1601611

Katika kipindi hiki cha kampeni za urais, nimekuwa nikimwona huyo jamaa aliyevaa ‘Kaunda suti’ ya buluu hapo kwenye picha, akiwa pembeni ya Tundu Lissu karibu kila sehemu.

Nikiangalia mavazi yake pamoja na hako ka peni alikokachomekea kwenye mfuko wake wa shati, naona ana fit profile ya wale walinzi kutoka serikalini ambao huwalinda viongozi wa nchi.

Najua kwa nchi kama Marekani, wagombea urais wa vyama vikuu [Republican na Democrats na pengine hata wale wa kujitegemea kama Ross Perot] hupatiwa ulinzi wa Secret Service.

Sasa kwa Tanzania sijui. Kama kuna anayejua, itapendeza akitujuza wale ambao hatujui.

Manake kila nikimwangalia huyo jamaa naona kama vile anatoka kwenye hicho kitengo cha walinzi wa viongozi.

Kama anatokea huko, ni jambo ambalo ni la mwaka huu tu hususan kwa Tundu Lissu au ni ndivyo ilivyo miaka yote ya uchaguzi?
Wanaweza kuwa ni walinzi toka serikalini sioni tatizo kwa hilo.
 
Kwanini huyo Mungu hakuzizuia hizo risasi 16 kuliko kumwacha atandikwe nazo?
Ili ukuu wake uonekane. Ili watu kama wewe mjue kuwa Yeye ndio mwenye uwezo wa kuokoa. Zaburi 68:20 "Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana"

Mungu hakuangaika kumzuia Daniel asitupwe kwenye tundu la simba ila alihakikisha simba hawamgusi hata vazi lake. Mungu hakuhangaika kuzuia kina Meshaki wasitupwe kwenye tanuru la moto ila alihakikisha hawaungui na wala moshi hauwapati. Mungu ajaanza jana wala leo kutenda haya na huu ni uthibitisho tosha kuwa Lissu anaongozwa na Roho wa Mungu aliye hai.

Jambo la kukumbukwa Mungu hajawahi kufanya kazi kwa hasara. Alipomuokoa Musa na mkono wa farao alimpa kazi ya kuwatoa Israeli utumwani, alipo muokoa Daudi mbele ya Goliath alimfanya kuwa mfalme wa Israeli, baada ya kumuokoa Daniel na Simba alimpa kuwa waziri mkuu, alifanya hivyo kwa Yusuph pia.
 
Wakuu.

Mlinzi wa Lisu amepewa na Serikali au CHADEMA wamempatia, au yeye mwenyewe?

The guy yupo very serious sana
IMG_20201023_203811.jpeg
 
Back
Top Bottom