Hivi tungekodi kampuni ya Uingereza kuchunguza makinikia tungejua tulichojua?

Hivi tungekodi kampuni ya Uingereza kuchunguza makinikia tungejua tulichojua?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Ndugu zangu Watanzania, kuna watu bado hawajui au hawaamini kama ukoloni na ubeberu ni matokeo ya hila kubwa ya nchi za magharibi na raia wao ikiwepo marekani. Kuna ushirika mkubwa kati ya nchi za kibeberu na makampuni mbalimbali ya nchi hizo linapokuja suala la kuendelea kumiliki uchumi wa nchi changa hasa za afrika.

Hivi niwaulize swali. Kama hayati Magufuli asingetuongoza kujiamini wenyewe tukakodi kampuni ya kingereza kufanyia uchunguzi yale makinikia acacia wakiita mchanga tungejua kile kilichokua ndani yake?

Januari Makamba ni mtu hawezi kufikiri kwa akili yake hadi akodishe mzungu kwa hela ya umma kufikiri kwa ajili yake. Sijui nini anapata kwa kuwaamini sana wageni hasa wazungu. Tabia kama hiyo ndio analeta kwenye uongozi wa mashirika nyeti chini ya wizara yake. Tangu amewekwa waziri wa nishati tumeona akisaini kandarasi na wageni kusimamia mambo yetu ya uchumi. Kandarasi moja baada ya nyingine.

Tumeona ikiletwa kampuni ya kihindi kukodisha mfumo wa electronic wa usimamizi tanesco kwa dola milioni 30. Kiwango kikubwa sana. Je hakuna watanzania wanaweza kubuni mfumo kwa shughuli kama hiyo. Je hao wahindi walishindanishwa na kampuni zipi?

Juzi tena hapa tumeona mkataba na kampuni ya kingereza eti kushauri tpdc mambo ya kisheria kuhusu uwekezaji. Hizo kampuni zinafuata templates za kinyonyaji tu sisi kubwaga resources zetu kwa wawekezaji. Tumeona timu yetu ya wazalendo ya kina kabudi ikiweka namna mpya ya mikataba kwenye madini hadi nchi nyingi za kiafrika ziki copy na ku paste mikataba yetu. Ukiuliza kama hiyo kampuni ya kingereza imepewaje hiyo kazi huwezi ona kama wameshindanishwaje.

Hawa mareactionaries wapinga maendeleo mama anawarudisha ndio wataturudisha nyuma kwa maendeleo. Wao wanatafuta maendeleo yao binafsi hivyo watatumika na maadui wa maendeleo ya umma.
 
Ni vizuri kujiridhisha kwanza kabla ya kutuhumu,,,, great thinker !

Mikataba yote miwili ilikuwepo tangu Kalemani, na tender zilitangazwa.

Kuhusu LNG tender ilitangazwa 2018 na mlipaji wa gharama za mkataba huo ni benki ya maendeleo ya Africa AFDB.

20220126_235607.jpg
20220126_235720.jpg
20220126_235612.jpg
 
Ndugu zangu watanzania, kuna watu bado hawajui au hawaamini kama ukoloni na ubeberu ni matokeo ya hila kubwa ya nchi za magharibi na raia wao ikiwepo marekani. Kuna ushirika mkubwa kati ya nchi za kibeberu na makampuni mbalimbali ya nchi hizo linapokuja suala la kuendelea kumiliki uchumi wa nchi changa hasa za afrika.
Kwa uandishi wako na mpangilio wa sentensi nahisi Elimu yako siyo zaidi ya Form 4.

Kwa kifupi ripoti ya MAKINIKIA ilikuwa rubbish yaani takataka.

Baada ya kuwa Rais alitaka ku-prove kuwa ACACIA wanatuibia madini kupitia makinikia, ndipo akaunda tume ya Prof Mruma na Prof Osoro. Kiukweli Tume ya Prof Mruma ilikuta kuwa kontaina la 20ft lina 0.7Kg ya madini ya dhahabu na silver. Na kiasi hicho ndiyo kimekuwa kikilipiwa na ACACIA/ Barrick kodi sahihi kuanzia 1998.

Kwa vile Jiwe alidhani tunaibiwa madini wakati si kweli akaichakachua ripoti ya Prof Mruma na kuandika kuwa kuna 7.0 Kg kwa kila container. Hapa ndiyo ile hoja ya ACACIA kukwepa ushuru wa USD 190 bilioni au Tsh 450 Trillioni ndipo ilipojitokeza. Hiki kitu Tundu Lissu aliita professorial rubbish kwa kuwa ni uzandiki mtupu. Na kweli hatujapata hiyo Tsh 450 Trilion aka Noah moja kwa kila Mtanzania.

Ila Tanzania Ina wajinga wengi sana kama kmbwembwe wao bado wanaamini uwongo wa Magufuli
 
Ni vizuri kujiridhisha kwanza kabla ya kutuhumu,,,, great thinker !

Mikataba yote miwili ilikuwepo tangu Kalemani, na tender zilitangazwa...
Magufuli alikuwa anajuwa kiwango cha ujinga wa Watanzania walio wengi na ndiyo ukawa mtaji wake kwa propaganda za UWONGO. Ametuachia population ya wajinga wengi sana kama huyu kmbwembwe, wanapinga kila anachofanya Rais Samia na Makamba. Wajinga wanaamini eti hii mikataba Januari Makamba amepiga simu hizo kampuni ikaja. Kumbe mchakato umeanza mwaka 2018
 
Kwa uandishi wako na mpangilio wa sentensi nahisi Elimu yako siyo zaidi ya Form 4.

Kwa kifupi ripoti ya MAKINIKIA ilikuwa rubbish yaani takataka...
Sasa hayo mambo ya kuchakachua ripoti ya mruma ndio nasikia kwako. Inaonekana ni mzushi tu kwa chuki. Nchi hii watu sio wajinga ila vibaraka na wabinafsi ndio wamejaa. Eti jiwe akachakachua.. kama una shahada chuo kikuu itakua cheti feki.
 
Sasa hayo mambo ya kuchakachua ripoti ya mruma nfio nasikia kwako. Inaonekana ni mzushi tu kwa chuki. Nchi hii watu sio wajinga ila vibaraka na wabinafsi. Eti jiwe akachakachua.. kama una shahada chuo kikuu itakua cheti feki.
Kama ni kweli, vip ulilipwa pesa zako?.
Zile ripoti zilikuwa hovyo sana, technical ripoti huwezi kuandika kishabiki vile. Watanzania wengi uwelewa wetu ni mdogo sana hivyo ni rahisi kudanganywa. Mwendazake alikuwa muongo sana.
 
Sasa hayo mambo ya kuchakachua ripoti ya mruma nfio nasikia kwako. Inaonekana ni mzushi tu kwa chuki. Nchi hii watu sio wajinga ila vibaraka na wabinafsi. Eti jiwe akachakachua.. kama una shahada chuo kikuu itakua cheti feki.
Hujui tu, jiwe kachakachua vitu vingi saaana. Nasema hujui kitu na hakika mtaji wa Jiwe ni watanzania wajinga walio wengi. Hivi inakuingia akilini kampuni ikwepe kodi ya TZS Trillion 450 halafu ulipwe million 300; na ambayo nayo isilipwe then wewe uliyeibiwa uone sawa tu.
 
Hujui tu, jiwe kachakachua vitu vingi saaana. Nasema hujui kitu na hakika mtaji wa Jiwe ni watanzania wajinga walio wengi. Hivi inakuingia akilini kampuni ikwepe kodi ya TZS Trillion 450 halafu ulipwe million 300; na ambayo nayo isilipwe.
Eti jiwe alichakachua vitu vingi..hata aibu huoni?
 
Ndugu zangu watanzania, kuna watu bado hawajui au hawaamini kama ukoloni na ubeberu ni matokeo ya hila kubwa ya nchi za magharibi na raia wao ikiwepo marekani. Kuna ushirika mkubwa kati ya nchi za kibeberu na makampuni mbalimbali ya nchi hizo linapokuja suala la kuendelea kumiliki uchumi wa nchi changa hasa za afrika.

Hivi niwaulize swali. Kama hayati magufuli asingetuongoza kujiamini wenyewe tukakodi kampuni ya kingereza kufanyia uchunguzi yale makinikia acacia wakiita mchanga tungejua kile kilichokua ndani yake?
Kwanza huna taarifa sahihi, kwa sababu wangesema mchanga yasingeitwa tena makinikia!! Tafuta Ripoti ya TMAA ya 2011, na kama huwezi kufanya hivyo basi soma thread yangu inayosema Ripoti ya Kitalaamu Kuhusu Uchenjuaji wa Mchanga wa Madini, ambapo moja ya paragraph inasema:-
2. BGM and BZGM, which are the only mines currently producing and exporting Copper Concentrate were visited to witness production, loading of the concentrates into containers, sampling and sealing of loaded containers ready for transportation to China or Japan for smelting and refining.
Unaona hapo, ni COPPER CONCENTRATE na hakuna popote taarifa inaposema ni MCHANGA!

Mwiba zaidi, Ripoti ikasema:-
1. The study has revealed that a commercially viable Copper Concentrate smelter requires a feedstock of not less than 150,000 tonnes per year. At full capacity, BGM and BZGM production is about 60,000 tonnes of Copper Concentrate annually, which would only account for 40% of the capacity of a viable Copper Concentrate smelter. Currently, no commercial-scale proven technologies exist which are suitable for small scale Copper Concentrate smelting of less than 100,000 tonnes per year, but this matter continues to be investigated.
Kwamba, madini yanayopatikana kwenye makinikia hayatoshelezi kutufanya tujenge mtambu wa kuchambua hayo makinikia hapa hapa!!

Watu wakatoa povu ile mbaya, wengine wakatukana lakini kila mwenye akili timamu anafahamu JPM HAKUZUNGUMZIA TENA suala la kujenga Copper Concerates smelters, na HADI KESHO MAKINIKIA YANASAFIRISHWA!!

So, suala la JPM kuajiri wataalamu kutoka nje, mosi lisingekuwa na mantiki kwa sababu sekta ya madini sio ngeni kwetu na kwahiyo tunao hao watalaamu! Lakini kama angeamua kufanya hivyo, Wataalamu hao wangetuepusha na aibu ya kusema tunadai Sh 420 trillion na matokeo yake tunaishia kupata vibilioni kadhaa!!!
Januari makamba ni mtu hawezi kufikiri kwa akili yake hadi akodishe mzungu kwa hela ya umma kufikiri kwa ajili yake. Sijui nini anapata kwa kuwaamini sana wageni hasa wazungu. Tabia kama hiyo ndio analeta kwenye uongozi wa mashirika nyeti chini ya wizara yake.
Tangu amewekwa waziri wa nishati tumeona akisaini kandarasi na wageni kusimamia mambo yetu ya uchumi. Kandaradi moja baada ya nyingine.
Siwezi kurudia kwa sababu HatibuZ amekuonesha tenda ilitangazwa lini! In short, hata JPM Administartion ilifahamu hatuna watu wenye uzoefu kwenye sekta ya gesi na mafuta! Hili jambo lipo wazi sana, hivyo nashangaa kwanini watu tunataka kuleta uzalendo fake wakati we all know hii sekta ni mpya!!

Kama hujawahi kuwa na commercial oil and gas industry from engineering level, hivi mnatarajia hao wataalamu wa Kitanzania hiyo kazi walikuwa wanafanyia?!
Tumeona ikiletwa kampuni ya kihindi kukodisha mfumo wa electronic wa usimamizi tanesco kwa dola milioni 30. Je hakuna watanzania wanaweza kubuni mfumo kwa shughuli kama hiyo. Je hao wahindi walishindanishwa na kamuni zipi?
Hapo tena jaribu kutafuta taarifa uone huo mradi kwanza sponsor ni nani, na umeanza wakati gani!
Juzi tena hapa tumeona mkataba na kampuni ya kingereza eti kushauri tpdc mambo ya kisheria kuhusu uwekezaji. Hizo kampuni zinafuata templates za kinyonyaji tu sisi kubwaga resources zetu kwa wawekezaji. Tumeona timu yetu ya wazalendo ya kina kabudi ikiweka namna mpya ya mikataba kwenye madini hadi nchi nyingi za kiafrika ziki copy na ku paste mikataba yetu. Ukiuliza kama hiyo kampuni ya kingereza imepewaje hiyo kazi huwezi ona kama wameshindanishwaje.
Hawa mareactionaries wapinga maendeleo mama anawarudisha ndio wataturudisha nyuma kwa maendeleo. Wao wanatafuta maendeleo yao binafsi hivyo watatumika na maadui wa maendeleo ya umma.
Tafuteni taarifa, na mjifunze!!
 
Sasa hayo mambo ya kuchakachua ripoti ya mruma nfio nasikia kwako. Inaonekana ni mzushi tu kwa chuki. Nchi hii watu sio wajinga ila vibaraka na wabinafsi. Eti jiwe akachakachua.. kama una shahada chuo kikuu itakua cheti feki.
kmbwembwe chukua toka kwangu. Ripoti ya Mruma iliandikwa kitaalamu ila ilipofika kwake akaichakachua isome Kilo 7 badala ya gramu 700.

Kama angekuwa haja hakachua basi tungepata Ile USD 190 Billion
 
Magufuli alikuwa anajuwa kiwango cha ujinga wa Watanzania walio wengi na ndiyo ukawa mtaji wake kwa propaganda za UWONGO. Ametuachia population ya wajinga wengi sana kama huyu kmbwembwe, wanapinga kila anachofanya Rais Samia na Makamba. Wajinga wanaamini eti hii mikataba Januari Makamba amepiga simu hizo kampuni ikaja. Kumbe mchakato umeanza mwaka 2018
Kwani wewe umefika la ngapi hadi unaona watanzania wajinga? Wewe unajipima vipi kama una akili kwenye jeshi la wajinga? Au hayo mawazo ya kuamini na kuabudu wazungu ndio unafikiri una akili?

Nina hakika kama ni elimu hunizidi kwa hiyo acha dharau na kujiamini bure.

Kauli kama hizo za kusema watanzania ni wajinga eti mtaji wa magufuli ni watanzania wajinga zinatolewaga na wajinga na wabinafsi.
 
Sasa hayo mambo ya kuchakachua ripoti ya mruma nfio nasikia kwako. Inaonekana ni mzushi tu kwa chuki. Nchi hii watu sio wajinga ila vibaraka na wabinafsi. Eti jiwe akachakachua.. kama una shahada chuo kikuu itakua cheti feki.
Typical JPM Supporter...

Nyie watu mkiambiwa ukweli mnakimbilia kuita watu vibaraka au eti wana chuki!

Kama alichosema Stuxnet sio kweli, zile Trillion 425 zimeishia wapi?!
 
Eti jiwe alichakachua vitu vingi..hata aibu huoni?
1. Vitambulisho vya machinga unaweza chukulia mkopo.
2. ATCL inaingiza faida in billions
3. Kesi za mikataba ya madini zitasikilizwa na mahakama za ndani.
4. Tuna stahiki za Trillion 450!! but akakubali USD 300M
5. Atashughulika na mafisadi ilihali waliotajwa ripoti ya makinikia, Tanzanite, hawajakamtwa mpka leo.
 
Mkuu Chige uko deep sana kwenye sekta hii. Uwasilishaji wako unafunga mjadala. Nina uhakika hata mtoa thread kmbwembwe ataridhika na kukupa hats off
Man,

Huyo kmbwembwe KATU hawezi kuridhika kwa sababu, wakati naanza kumsoma nilidhani anakosa tu uelewa wa haya mambo, na WALA SIO DHAMBI kukosa uelewa!

Lakini baada ya kusoma posts zake zingine nimegundua issue hapa sio kukosa uelewa bali ufuasi!!
 
Kama hayati magufuli asingetuongoza kujiamini wenyewe tukakodi kampuni ya kingereza kufanyia uchunguzi yale makinikia acacia wakiita mchanga tungejua kile kilichokua ndani yake?
Mbona kwenye kashfa ya Tegeta Escrow kampuni ya kiingereza ya SFO iliibua madudu? Mbona PwC/E &Y ilichunguza kashfa ya Richmond na kuibua madudu. In fact madini yetu huwa yanakaguliwa na kampuni za nje maana kwenye biashara za kimataifa lazma uwe na global recognized firms kusimamia soko kma SGS. Nani ataamini ripoti ya Mruma ilihali hata maabara kubwa za kijiolojia hatuna? Na ndio maana hata kesi za kibiashara zinaenda ICSID ili kuwepo na neutrality otherwise kila nchi ingevutia kwake mashauri hayo.

Hata CCM ilani yake imeandikwa na wasomi wa nje kutokea Ghana na wengine uchina n.k sasa ukidhani uzalendo ni kuchukua mtanzania tu bila ya experience wala uweledi then utakua na shida kubwa sana.

Kingine mambo ya sayansi methodology zinafahamika so kama mtu akidanganya una uwezo wa kufuata methodology aliyoandika pale na utapata majibu ya kuprove. So hta makinikia kma ingekuja taasisi huru pengine ingekua neutral kuliko kina Mruma coz tyr Rais alikua ana majibu kabla ya uchunguzi so wasingeweza dissapoint.
 
Ndugu zangu watanzania, kuna watu bado hawajui au hawaamini kama ukoloni na ubeberu ni matokeo ya hila kubwa ya nchi za magharibi na raia wao ikiwepo marekani. Kuna ushirika mkubwa kati ya nchi za kibeberu na makampuni mbalimbali ya nchi hizo linapokuja suala la kuendelea kumiliki uchumi wa nchi changa hasa za afrika...
Kwa hiyo mlivyojua matatizo yenu Kama Nchi yameisha?
 
Typical JPM Supporter...

Nyie watu mkiambiwa ukweli mnakimbilia kuita watu vibaraka au eti wana chuki!

Kama alichosema Stuxnet sio kweli, zile Trillion 425 zimeishia wapi?!
False propaganda na indoctrination aliyotuachia Magufuli imetuachia population kubwa ya wajinga. Tuna kazi kubwa sana ya kuwaelewesha. Let him continue to rot in Chato
 
False propaganda na indoctrination aliyotuachia Magufuli imetuachia population kubwa ya wajinga. Tuna kazi kubwa sana ya kuwaelewesha. Let him continue to rot in Chato
Kabisa ametengeneza misukule mingi sana. Alitaka awe Mungu wetu ila Mungu halisi akasema huwezi chukuwa utukufu wangu. Watanzania walikuwa robot la Mwendazake.
 
Back
Top Bottom