Mi ni wa huko lakini amna chochote tunafundishwa.
Ni jamii yetu tu kina babu zetu waliwahi mjini tu, hichi kitu jamii nyingine hawaelewi wachagga hatufundishwi pesa.
Sema tu tuliwahi na bado tunawahi mjini ndiyo hicho tu, mbona wakinga sasa hivi wanawahi mjini na jamii nyingine kama waha, wakuria, wanyakysa, wamakonde, wamaasai, na wasukuma.
hizi jamii nilizo zitaja hapo juu nao pia wanawahi mjini miaka hii japo kuwa walikuta wachagga na wahindi washawahi mjini ni hicho tu kiongozi.
Na kuwahi mjini siyo bongo tu watu wako marekani toka miaka ya 90's mi nina uncle zangu miaka hiyo wapo wanaishi marekani.
Ninafahamu wazee walio wahi kariakoo enzi hizo una ambiwa wana ardhi pale na kijibanda cha mangi, leo hii wana ghorofa ile ardhi imepanda thamani.
Amna cha zaidi kwa wachagga useme kabila nyingine hawawezi kuwa kama wao, japo tu kabila nyingi zimeridhika na maisha mi naona hivo.
kabila hizo mmoja akipata utasikia kaja baba, mama, shangazi, mjomba, mtoto wa baba mkubwa, mawifi, mashemeji, n.k yaani wote wanaenda kwa mji mmoja wa mtu mwenye familia moja wanakula na kulala hapo kisa eti wamesikia anafanya benki.😅😅 hii kitu inafanya mtu ashindwe kujikwamua kiuchumi yaani mtu mshahara laki7 au laki 5 mnamgandaa hivyo hawezi tobo.
kwa wachagga wengi huu utaratibu amna.
yaani wewe ni mgeni ukija kwetu utabidi uulizwe ratiba yako ikoje upo kwetu mpaka lini na kama tuna 3 bedroom tutakuambia hatuna nafasi hivyo utalala huku unatafuta guest japo wakuu mi roho hiyo sina😅😅ila wengi wa wakwetu ninao wafahamu.