vibesen xxx
JF-Expert Member
- Jul 23, 2022
- 3,187
- 6,620
Nidhamu ya pesa! Ndio uchawi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Safi sana kijana....usome Same na maisha usitoboe...pale ni kambi ya jeshi...uchagani spirit ya utafutaji huwa inazoezwa tangu mtu akiwa mtoto mdogo, mfano asilimia kubwa ya watoto wana sungura zao , kuku zao wanazipambania mpka zianze kuzaa matunda , mauzo ya pesa wanazopata wananunulia baadhi ya mahitaji ya shule na zinazobaki zinaendeleza mitaji yao mpka ikuwe , mfano mimi nikiwa msingi niliuza sungura zangu nikanunua baiskei kwa ajili ya kwenda kusagia unga majirani , nilikua natoza mia tano kwa kila kichwa , pesa nilizopata nilizitunza kwenye kibubu , nilipovunja nyingne niliendeleza mradi wa sungura , nanyingne niliongeza nguruwe jike mmoja , nikawa nazipambania na baiskeli yangu nikitoka shule , nasaga mahindi kwa mia 500 nakuchota maji madumu kumi 2000 natunza pesa , kwani nilikua nakula nyumbani , nguo na vingne wazazi wananunua[emoji4] mwisho wa siku nikajikuta na pesa ambazo kwa udogo wangu sikueza kuzicontrol , nikamshirikisha maza , akanishauri tupanue mradi wa ngurue na tununue kuku wa mayai kilacha , vifaranga mia tutunze , namaliza form 4 na pesa nyingi tu , nasubiri matokea kwenda form 5 nikafungua mpesa , tigo pesa na sehemu ya kupika kiti moto , nikapiga biashara mpka matokeo yalivyotoka nikachaguliwa form five pcb same boys nikamwacha mdgo wangu wakike anaefuata aendeleze biashara , ilikua mno , nikiwa likizo nafuatialia ilinisaidia mambo mengi mno kishule , mpka naenda chuo biashara hyo inanibeba , namaliza chuo nipo mazoezi kwa mda wa miaka miwil biashara inakua , nikapata wazo nifungue maabara na phamancy kupitia hyo biashara na sasa nipo apo . hii nikuonyesha misingi huwa inajengwa toka mtoto akiwa mdgo anatakiwa ajue pesa , kuitafuta na jinsi yakuiendeleza , pesa izae pesa na pesa izae pesa na nakuendelea.
hahahahhaha masandale ilininyoosha mkuu[emoji28]Safi sana kijana....usome Same na maisha usitoboe...pale ni kambi ya jeshi...