Hivi Uchagani watu wanafundishwa nini kuhusu Pesa?

Hivi Uchagani watu wanafundishwa nini kuhusu Pesa?

Nimeoa huko:
1. wananidhamu sana ya pesa,
2. wanapenda kuwa na pesa,
3. pesa kwao ni heshima,
4. ni rahisi kuinuana hasa kwenye familia moja,
5. wanashindana kimaendeleo, wapambanaji,
6. hawana cha bure, ukimuajiri akiona fursa anakupiga au anajiongeza bila kuharibu hesabu zako (wako smart ktk wizi wao).

Najifunza sana kwa mke wangu na baba mkwe wangu.
 
Hakuna jipya zaidi ya kujua thamani ya pesa. Kila mtu anatakiwa awe na pesa ya kula chakula kizuri, kulala mahali pazuri pa kwako, kuvaa vizuri na usafiri wa uhakika (sio lazima uwe na gaari ila uwe na uwezo wa kusafiri popote kutafuta pesa). Kwa vile wazazi wa Kichagga wanajua hilo hatua ya kwanza kwa watoto ni kuwapatia ile elimu ya msingi (basic knowledge) iwe ya msingi, sekondari au chuo. Baada ya hapo kila mmoja anajua lazima atafute pesa kwa mbinu zozote zile ili aweze kutoboa! Wanapambana na ule msemo "Mtegemea cha ndugu hufa maskini" na "Maisha ni popote".
 
Nasikia eti lakini,

Mtoto wa kichaga akiwa mdogo akilia anapewa pesa ashike,

Atanyamaza kulia hapo hapo.

Hiyo itamjenga kuwa rafiki mzuri ni pesa.
 
uchagani spirit ya utafutaji huwa inazoezwa tangu mtu akiwa mtoto mdogo, mfano asilimia kubwa ya watoto wana sungura zao , kuku zao wanazipambania mpka zianze kuzaa matunda , mauzo ya pesa wanazopata wananunulia baadhi ya mahitaji ya shule na zinazobaki zinaendeleza mitaji yao mpka ikuwe , mfano mimi nikiwa msingi niliuza sungura zangu nikanunua baiskei kwa ajili ya kwenda kusagia unga majirani , nilikua natoza mia tano kwa kila kichwa , pesa nilizopata nilizitunza kwenye kibubu , nilipovunja nyingne niliendeleza mradi wa sungura , nanyingne niliongeza nguruwe jike mmoja , nikawa nazipambania na baiskeli yangu nikitoka shule , nasaga mahindi kwa mia 500 nakuchota maji madumu kumi 2000 natunza pesa , kwani nilikua nakula nyumbani , nguo na vingne wazazi wananunua[emoji4] mwisho wa siku nikajikuta na pesa ambazo kwa udogo wangu sikueza kuzicontrol , nikamshirikisha maza , akanishauri tupanue mradi wa ngurue na tununue kuku wa mayai kilacha , vifaranga mia tutunze , namaliza form 4 na pesa nyingi tu , nasubiri matokea kwenda form 5 nikafungua mpesa , tigo pesa na sehemu ya kupika kiti moto , nikapiga biashara mpka matokeo yalivyotoka nikachaguliwa form five pcb same boys nikamwacha mdgo wangu wakike anaefuata aendeleze biashara , ilikua mno , nikiwa likizo nafuatialia ilinisaidia mambo mengi mno kishule , mpka naenda chuo biashara hyo inanibeba , namaliza chuo nipo mazoezi kwa mda wa miaka miwil biashara inakua , nikapata wazo nifungue maabara na phamancy kupitia hyo biashara na sasa nipo apo . hii nikuonyesha misingi huwa inajengwa toka mtoto akiwa mdgo anatakiwa ajue pesa , kuitafuta na jinsi yakuiendeleza , pesa izae pesa na pesa izae pesa na nakuendelea.
 
Safi sana kijana....usome Same na maisha usitoboe...pale ni kambi ya jeshi...
 
Hulka ya kuthamini swala zima la maendeleo, mchaga hawezi kuona majirani zake wamejenga, wanabishara n.k yeye atulie tu!!
Huku watu wengi hufikiri pesa sana zaidi ya hata mapenzi nafikiri ndo maana hata wanaume wanaishi miaka michache zaidi kuliko hao wa Pwani
Mzee unakuta anatafuta pesa km ndo anamiaka 30's hali hata chakula site ni kipotabo na andazi kazi kazi anakazia
 
Maarifa, kianzio, nidhamu na nertwork = Mtaji.

Nimekulia Singida, Kule kuna wachaga wengi wa vipato vya kati, Kuna kitu nilichunguza toka nikiwa mdogo mdogo, kuna duka moja la wachaga lilikua soko kuu, Sikuwahi kumjua mmiliki ila nilichunguza nikagundua wale wauzaji vijana ambao tumezoea kuwakuta pale, ikipita wakati fulani tuseme labda mwaka huyo huyo kijana lazima utamkuta sehemu nyingine akiwa na kiduka chake tayari, ni rahisi kuliona hilo sababu mji ni mdogo uwezekano wa kukutana na watu walewale ni mkubwa. Na lile duka mama utalikuta lipo kwa ukubwa ule ule na wapo vijana wapya ambao baada ya muda na wenyewe utawakuta sehemu nyingine tayari wana vya kwao.

Rafiki yangu binti wa kichaga nimesoma nae wao wakirudi likizo wanaenda kufanya kazi na wanalipwa posho kwenye biashara ya baba yao, wakati mfano mimi nilikua naenda kwenye biashara ya nyumbani kama kuzuga tu haulipwi wala hauwi motivated na kitu chochote, na likizo nzima siku nyingine unaenda siku nyingine huendi biasharani unabaki kuzurura tu, See the difference.

Nimekua, nikafungua biashara na mimi, opposite yangu jirani ni mchaga na ye inaonekana biashara ni mpya ya mpesa, jioni wenzake wakitoka kwenye biashara zao wanaenda kufanya miamala pale kwa mwenzao, (utawasikia wakiongea unajua tu hapa dugu moya)

Maarifa, kianzio,nidhamu na network = Mtaji.
 
Back
Top Bottom