Watu wa aina hii huwatenda hayo yote wanaoishi nao, kisha kama haitoshi, utasikia wanawatangaza na kulalamika kwa watu kama, YAANI MIMI NINA MIZIGO NYUMBANI KWANGU. Watu ninawalisha, nawatunza, yaani wananitegemea mimi mpaka ninashindwa kuwanunulia watoto wangu vyakula vizuri.
Hapo hapo wanasahau kuwa hao wanaowaita mizigo unakuta ndo wanaofanya kazi za nyumbani, kuhudumia mifugo na pengine mavazi na breakfast wanajihangaikia wenyewe.
Ushauri: Kama unaona hupendi watu wakae nyumbani kwako, usiwatoe walipo, wapelekee msaada kule kule kwao. Kuliko kuwaleta au kuwakaribisha kwako na kuanza kufanya vitimbwi na kuwasimanga!