Hivi uchoyo/ubinafsi unafaida gani katika maisha yako ya duniani hapa

Hivi uchoyo/ubinafsi unafaida gani katika maisha yako ya duniani hapa

Mkuu binadam ukishamjua hulka yake ni rahisi sana kuishi naye

Hata kama ana tabu kiasi gani utamudu tu

Ni wewe kuignore yatendekayo na kufanya mambo yako na kukamilisha kilichokupeleka pale



Madame S
Akhsante sana
 
Kiongozi.

Si kama ufikiriavyo.

Ni Udhaifu wa Roho tu.

Kama huamini, mwingine analeta Unoko kwenye Vitu ambavyo wala si vyake/si vya kwake au naweza sema ni Mpambe tu fulani. Wakati ukija kwa mwenye vyake/mwenye Mali wala hana tatizo lolote.

Sasa kwa mfano huo tu.

Kwa kukunukuu, unataka kuniambia "anakufanyia hivyo ili na wewe uweze kuwa na akili ya kufikiri utafuta vyako"

Hapana, nakataa
Mi pia nimepingana na hilo, mtu kukuelekeza maisha sio lazma akukomoe. Hicho kinachoonekana hapo ni tabia flani tu mbovu ambayo mtu anaweza kuwa nayo, commonly kama roho ya kwanini. Sasa jiulize kuwa na roho ndogo ndio kumfundisha mtu maisha???
 
Well said mleta Uzi.
Wako watakaosema "Tafuta Chako".

Nadhani litakua jibu superficial sana, ni kwakua hawajajua the extent of the problem. Na utakuata sio kwamba anakuonea wivu au ugumu WA maisha, kwasababu anaweza kua amekuzidi kipato au hata umri...

Nafikiri kua watu wana negative energy to others.

Some people's pleasure depends very much on making others feel pain.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu wa karibu yako ndie anaekufanyia roho mbaya, sasa maisha yakiwa mazuri sioni kama itakuwa vyema umsaidie yule aliekufanyia roho mbaya.
Huyo huyo aliekufanyia roho mbaya baadae utakaporekebisha atasahau yote mabaya aliyokufanyia.

Na baadae ataanza kukulaumu wewe iwapo hatopata msaada kutoka kwako.

Na mbaya zaidi atakapohitaji msaada kutoka kwako, upande wake mathalani mambo ndio yameenda Kombo au yametetereka kidogo. Utaona nongwa yake.

Wanakuwa Watu wa nongwa sana.

Mara nyingi watu wa hivi ni wasahaulifu sana kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.

Ulimwenguni wapo Watu wa namna hii, tena ni wengi sana.

Haya mambo yanatokea na tumeshayashuhudia, na tunayashuhudia kwenye Maisha yetu ya kila siku
 
Uchoyo ubinafsi faida yake ni kuwafundisha watu tegemezi wavivu wazembe kulakulala wasiopenda kujishughulisha wajishughulishe wapate vyakwao sio kukaa na kulalamikia ujinga kama huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani we ni mmojawapo mwenye tabia ya kipuuzi ukidhani ni sifa. Ishi na watu vizuri wewe...
 
Well said mleta Uzi.
Wako watakaosema "Tafuta Chako".

Nadhani litakua jibu superficial kwasababu Tatizo hili ni kubwa sana.
Nafikiri kua watu wana negative energy to others.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli mkuu, na tayari kuna watu wa hivyo washajitokeza kuni attack. Mwisho wa siku kuish na watu vizuri kunajenga kumbukumbu nzuri sana na kuleta baraka zaidi maishani. Watu inabidi tujifunze
 
Sidhani kama kuna faida zaidi ya kujijengea chuki na uhasama mioyoni mwa wanaokuzunguka

Madame S
Yani najiulizaga hivi unajiskiaje kumsumbua binadamu mwenzako pasi na sababu za msingi. Cha ajabu mtu kama huyo utakuta ndio namba moja kanisani au mtu wa swala 5! Unajiuliza sasa huko kwenye nyumba za ibada anafuataga nini kama si unafiki
 
Unoko tu.

Hapo kwenye Motokaa ndio usiseme.

Kuna baadhi ya wakina Baba, Chombo kipo Nyumbani lakini hawataki Watoto zao kugusa, au japo kuwafundisha.

Au kuwafundisha Wake zao, halafu unakuta wanaishi au wameshaishi Miaka mingi ndani ya Ndoa yao.

Mtu yuko tayari akiwa anaumwa akodiwe Chombo kupelekwa Hospitalini, kuliko kutumiwa Chombo kilicho Nyumbani. Eti kwasababu tu mwenye Chombo chake amepatwa na Maradhi.

Kwa kweli kuna Watu wa ajabu sana hapa Ulimwenguni
Hahahahahaha, unajikuta unaosha tu na kupigia picha. Ila kuna watu wachungu mno, mtu ndugu yako anaumwa kazidiwa unaona shida kumpa ride eti akatafutiwe usafiri mwengine. Gari yako inabebea malaya tu
 
Yani najiulizaga hivi unajiskiaje kumsumbua binadamu mwenzako pasi na sababu za msingi. Cha ajabu mtu kama huyo utakuta ndio namba moja kanisani au mtu wa swala 5! Unajiuliza sasa huko kwenye nyumba za ibada anafuataga nini kama si unafiki
Mkuu nafsi tu na roho ya mtu ndio hupelekea hivo

Pengine mioyoni mwao wanajisikia nafuu kuona unavyohaha kutokana na tabu wanazokupatia wao huona sahihi tu

Madame S
 
Hatari Sana. Mama wa nyumba anaweka vitu vya kupika chumbani kwake, sasa uone anavyomgombeza dada wa kazi kwa matumizi Mabaya! Mama anawaka vitu vidogo hadi kero. Kwakweli hii tabia inaudhi
 
Hauna faida yeyote basi tu ni roho ya mtu ilivyo mbaya au utakuta mwanamke kaolewa ndugu wa mume wakija mwendo wa maharage tu na dagaa mpaka waondoke
Inashangaza sana[emoji134] utasema hela ya matumiz anatoa yeye.. ubaya wa watu wabinafs/wachoyo huwa wanajisahau kwamba kuna cku hawatakuwepo dunian cku1.. sasa hapo malipiz ni kwa watoto waliowaacha..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni bora kutafuta vyako ndugu...

Maisha magumu sana sasahivi...
 
Watu wa aina hii huwatenda hayo yote wanaoishi nao, kisha kama haitoshi, utasikia wanawatangaza na kulalamika kwa watu kama, YAANI MIMI NINA MIZIGO NYUMBANI KWANGU. Watu ninawalisha, nawatunza, yaani wananitegemea mimi mpaka ninashindwa kuwanunulia watoto wangu vyakula vizuri.

Hapo hapo wanasahau kuwa hao wanaowaita mizigo unakuta ndo wanaofanya kazi za nyumbani, kuhudumia mifugo na pengine mavazi na breakfast wanajihangaikia wenyewe.

Ushauri: Kama unaona hupendi watu wakae nyumbani kwako, usiwatoe walipo, wapelekee msaada kule kule kwao. Kuliko kuwaleta au kuwakaribisha kwako na kuanza kufanya vitimbwi na kuwasimanga!
 
Haaaaaaaaaaaaaaaa umenikumbusha jirani yangu mmoja hapa... Amekuja kuwekeza samaki kwangu..


Ana wageni masela wenzake. Mboga naona ni dagaa maharage tangu wafike dah Nimeshangaa sana


Mahondaw wa Smart911
 
Watu wa aina hii huwatenda hayo yote wanaoishi nao, kisha kama haitoshi, utasikia wanawatangaza na kulalamika kwa watu kama, YAANI MIMI NINA MIZIGO NYUMBANI KWANGU. Watu ninawalisha, nawatunza, yaani wananitegemea mimi mpaka ninashindwa kuwanunulia watoto wangu vyakula vizuri.

Hapo hapo wanasahau kuwa hao wanaowaita mizigo unakuta ndo wanaofanya kazi za nyumbani, kuhudumia mifugo na pengine mavazi na breakfast wanajihangaikia wenyewe.

Ushauri: Kama unaona hupendi watu wakae nyumbani kwako, usiwatoe walipo, wapelekee msaada kule kule kwao. Kuliko kuwaleta au kuwakaribisha kwako na kuanza kufanya vitimbwi na kuwasimanga!
[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24][emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
Back
Top Bottom