Hivi uharamu wa Gongo, Bangi na kitimoto ni nini?

Wee jamaa ondoa kitimoto hapo juu🤧🤧🤧
 
Noma sana!
 
Kwenye suala la kitimoto tuachane unafiki[emoji39][emoji39] wengi huwa tunazifakamia vzr sema kuna miezi mabuchani huwa zinadoda [emoji848][emoji848]
 
Ngamia hacheui lakini analiwa na sisi waislamu bila shaka yoyote
 
Tuanza na Mkuu wa Meza 🐖 KitiMoto

Huyu ana mnyoo ambao umethibitika kitabu kwamba haufi hata ukiwekwa kwenye nyuzijoto 130 na zaidi yaan hata akiwekwa kwenye lile joto la kuyeyushia chuma hafi na huyo mnyoo chakula chake kikubwa ni protein na hupendelea zaidi protein ya kwenye ubongo wa mwanadamu, hivyo basi akiingia mwilini hukimbilia kwenye ubongo kisha anaanza kuishi uko

Anaitwa Taenia solium husababisha Cysticercosis pamoja na Taeniasis

Bangi hii bwana ni uraibu na ina uraibu mkubwa nakumbuka Bro's wangu wawili km sio watatu imewachukua hii kitu

Wa kwanza alikua akivuta bangi ndio anapata stimu za kulima so akienda shamba chakula chake kikubwa kilikua ni Bangi na alikua analima mchana wa jua Kali saaana yaan akishapiga bangi zake kete kadhaa akishanyonga akavuta mipuli yake kadhaa anaingia shamba analima na alikua analima sio kawaida, but siku ya siku ilimchukua maana alianguka shambani ile kumuwaisha hospital wakagundua kaishiwa maji ikabidi wamwekee dripu za maji wakaangaika madaktari weee kumkomboa ila hakumaliza wiki akavuta pumzi ya mwisho

Wa pili yeye pia alikua anavuta bangi ila hali chakula chochote kwa hio the same alivuta siku sababu ya kupungukiwa maji na alikua ameanza kua mental retarder, naye akavuta pumzi ya mwisho bangi ikamchukua

Wa mwisho yeye alikua ndio anaanza kuingia kwenye uraibu wa kuvuta bangi sasa bahati mbaya siku hio amevuta akapanda kwenye bodaboda wanaenda club na wenzake si akajisahau kwamba yupo kwenye bodaboda akajirusha akaangukia kichwa huo ndio ukawa mwisho wake maana alipasuka fuvu la kichwa na damu zilivilia kwenye ubongo baada ya siku 3 tukamzika

Gongo sio nzuri hii pia imenipotezea brother wangu mwingine, yeye huyu alikua akishapiga urabu wake anawavizia wake za watu anaokunywa nao gongo kisha anawamega, basi akategewa mtego kuna mke wa mtu alikua anammendea mmewe akawa amegundua mchezo wa jamaa kwamba Jamaa anamla mkewe sasa siku ya siku Jamaa akajichanganya akaenda kwa huyo mwanamke wakafanye yao Jamaa alipokutwa red-handed akakatwa bega kwa panga, bro hakumaliza wiki nae alipoteza maisha

Sasa umeona ubaya wa hivyo vitu kwenye jamii na mifano hai tunayo

NB:

Kuna watu bangi haiwadhuru ila inawachukua taratibu wanakufa kidogo kidogo yaan inawatafuna kidogo kidogo

Kuna watu Kitimoto hawadhuru ila inawachukua wanakufa kidogo kidogo mpaka aje kushtuka mwili mzima umejaa minyoo tupu hapo ndipo mtu anarukwa na akili

Kuna watu gongo haiwadhuru ila inawachukua taratibu wanakufa kidogo kidogo yaan sura ya kizee ila ni mtoto tu wa miaka 20

Sipendi bangi
Sipendi gongo
Sipendi kitimoto

Nayajua madhara yake ni makubwa kuliko wengine wanavyoyachukulia

Nitarudi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…