Hivi UKIMWI upo kweli kwa wasanii wetu wa Bongo Movie na Bongo Flavor?

Sio una huruma,ukikutana na mtu anayetimia arv virus vinakuwa vimefubaa makali,vimelala
 
Mmmh aisee ila hii kitu inatisha wakuu tuombe tu Mungu atunusuru aisee

Aunt anatajwa miaka mingi ila ananona tu khaaa
 
Misosi, tizi na kuzingatia kumeza pipi. Wanatangulia wazima unashangaa wenye ngwengwe wanatamba
 
Kazeze lipo la kushato mkuu ,Jichanganye tu ,ni hatari ,OGOPA ,muulize JANJARO.
 
Vile vidonge ni $600, hapo ni wastani wa milioni moja na nusu....sidhani kama wanayo hiyo nguvu.

Na pia sio 100% hakikisho la kuzuia/kudhibiti wale jamaa, ila hutumika tu kama tahadhari in case jamaa wameingia.
Vile si unapewa bure tu hospitali! Mi mwenyewe ninavyo napiga hapa leo siku ya 14. Na uzuri vya siku hivi sio vikali, havileti mawenge kama vya zamani maana nishakunywaga miaka minne iliyopita.

Cha msingi ni kwenda hospitali ya serikali, ila kama Mwananyamala wanataka ulipie 7,000 ya kumwona daktari eti! Nikawachomoleaga nikaenda Magomeni.
 
Wasanii wa bendi walikufa sana na ngoma kipindi hicho hakuna ARV
 
Niliiogopa ngoma nilipoenda kupima kabla ya ndoa, tangu hapo sitaki kuchepuka haki tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…