Hivi ukitoa hela kwenye ATM halafu ukaiacha pale kwenye kibox chake inaweza kurudi ndani kama card?!

Hivi ukitoa hela kwenye ATM halafu ukaiacha pale kwenye kibox chake inaweza kurudi ndani kama card?!

Sijawahi kujaribu au kama kuna mtu imewahi kumtokea akachelewa kuitoa hela baada ya kutoka je itadumbukia tena ndani au itakaa hapo hapo itaganda tu inasubiria.

Na kama ikirudi mahesabu yatakuwaje kwenye account yatajirudi tena kama awali au balance iatapungua.

Changamsheni kichwa kidogo.
Naomba kadi yako mara moja nijaribu
 
Itakuwa NMB hii, mimi pia ilinifanyia unyama huu na nilikuwa na shida sana na hela.
Ilibaki kidogo nimpige mtoa huduma NMB ni pasua kichwa salary ilichelewa sana mpaka 28 July, nilipojaribu kutoa hela ilikwama tena
 
Kwanini uandikie mate na wino upo??
Chukua kadi yako nenda nayo ATM
Ndio maana bandari wanapewa DP WORLD waTZ tunataka kutafuniwa kila kitu
 
Salam..

Sijawahi kujaribu au kama kuna mtu imewahi kumtokea akachelewa kuitoa hela baada ya kutoka je itadumbukia tena ndani au itakaa hapo hapo itaganda tu inasubiria.

Na kama ikirudi mahesabu yatakuwaje kwenye account yatajirudi tena kama awali au balance iatapungua.

Changamsheni kichwa kidogo.
Ko mpk unataka mpk hili ambalo hata ww unaliweza tusubir mzungu ajaribu alete majibu kwny vitabu watoto zenu wakariri,acha uzito Mkuu
 
Sina hakika ila ikirudi lazima itakwenda kuongezwa kwenye akaunti.

Nasema hivyo kwa sababu kuna siku nilikuwa natoa, ATM ikawa inahesabu hela then inafungua kamlango na haitoi kitu halafu inafunga inahesabu tena.

wakataji huo napata msg 2, ya kutoa hela na ya kurudishwa hela kwenye akaunti.
Haiwezekani kabisa.
 
Daaa umenikumbusha...
Kuna siku nilienda kutoa hela,
Mashine inahesabu weee, ikimaliza inafunguka halafu hela haiji, kama mara mbili hivii,

Kwenye simu msg imekuja umetoa kiasi flana cha helaa...

Nje kuna foleni, nikisema niende ndani jeee ikitoka chap wahuni wakiiwahi?(nyuma kumesimama jamaa flan kavu kweli)

Nikamuambia mlinzi naomba uzuie hapa asikanyage mtuu...., watumie mashine nyingne.

Kufika ndani wakanirekebishia, ila aliniambia haiwezekani kutoka...
Nikajisemea haya ni maneno tuu,
Nikamwambia we maliza kazi yako nitoke chapi hii ni pesa dada..., akatabasamu nikakwapua kadi yangu nikatoka.
Wakati mwingine kiwango unachoandika kinakuwa hakupi kwenye cash ndio maana inahesabu sana...
 
Kuna siku natoa pesa, kulia kwangu nasikia mashine ina beep ule mlio wa kuwa pesa imetoka, mimi nikawa bize na ATM yangu, mlio ukawa unaendelea tu, nikajisemea ngoja nichungulie, lahaula naona pesa shaaaa zinarudi ndani. Nahisi mteja mwenye haraka alitoa pesa sasa akaona pesa hazitoki akamua kusepa. Kumbuka inaanza kutoka kadi then mashine inahesabu pesa ndio zintoka.
Ukisikia vikengele tega macho hapo unapepesa.
 
Haiwezekani kabisa.
Sasa ndio iliwezekana ATM ya NMB Biafra.
Nilitoa hela ikahesabu, ikafungua mlango, haikutoa hela na ikahesabu tena na kufunga. Nikapata msg kuwa umetoa pesa kiasi fulani, sekunde chache baadaye nikapata msg Kiasi cha TZS ...... kimerudishwa kwenye akaunti yako inayoishia na .....
NMB karibu yako.

Hilo zoezi nilirudia mara 2 na ikafanya hivyo hiyo hadi nikaamua kutolea ATM ya CRDB Mwanamboka.
 
Salam..

Sijawahi kujaribu au kama kuna mtu imewahi kumtokea akachelewa kuitoa hela baada ya kutoka, je itadumbukia tena ndani au itakaa hapo hapo itaganda tu inasubiria.

Na kama ikirudi mahesabu yatakuwaje kwenye account yatajirudi tena kama awali au balance itapungua.

Changamsheni kichwa kidogo.
Nenda uitoe halafu uiache utajua inakuwaje
 
Sasa ndio iliwezekana ATM ya NMB Biafra.
Nilitoa hela ikahesabu, ikafungua mlango, haikutoa hela na ikahesabu tena na kufunga. Nikapata msg kuwa umetoa pesa kiasi fulani, sekunde chache baadaye nikapata msg Kiasi cha TZS ...... kimerudishwa kwenye akaunti yako inayoishia na .....
NMB karibu yako.

Hilo zoezi nilirudia mara 2 na ikafanya hivyo hiyo hadi nikaamua kutolea ATM ya CRDB Mwanamboka.
Hapo basi cash ilikuwa hazijatoka labda ndio ikakupa msg hiyo.
 
Sina hakika ila ikirudi lazima itakwenda kuongezwa kwenye akaunti.

Nasema hivyo kwa sababu kuna siku nilikuwa natoa, ATM ikawa inahesabu hela then inafungua kamlango na haitoi kitu halafu inafunga inahesabu tena.

Wakata huo napata msg 2, ya kutoa hela na ya kurudishwa hela kwenye akaunti.
Scenarios 2 tofauti! Mwache mleta mada aende kwenye ATM atoe hela halafu aziache hapo halo!
 
Back
Top Bottom