Hivi ukitoa hela kwenye ATM halafu ukaiacha pale kwenye kibox chake inaweza kurudi ndani kama card?!

Naomba kadi yako mara moja nijaribu
 
Itakuwa NMB hii, mimi pia ilinifanyia unyama huu na nilikuwa na shida sana na hela.
Ilibaki kidogo nimpige mtoa huduma NMB ni pasua kichwa salary ilichelewa sana mpaka 28 July, nilipojaribu kutoa hela ilikwama tena
 
Kwanini uandikie mate na wino upo??
Chukua kadi yako nenda nayo ATM
Ndio maana bandari wanapewa DP WORLD waTZ tunataka kutafuniwa kila kitu
 
Ko mpk unataka mpk hili ambalo hata ww unaliweza tusubir mzungu ajaribu alete majibu kwny vitabu watoto zenu wakariri,acha uzito Mkuu
 
Haiwezekani kabisa.
 
Wakati mwingine kiwango unachoandika kinakuwa hakupi kwenye cash ndio maana inahesabu sana...
 
Ukisikia vikengele tega macho hapo unapepesa.
 
Haiwezekani kabisa.
Sasa ndio iliwezekana ATM ya NMB Biafra.
Nilitoa hela ikahesabu, ikafungua mlango, haikutoa hela na ikahesabu tena na kufunga. Nikapata msg kuwa umetoa pesa kiasi fulani, sekunde chache baadaye nikapata msg Kiasi cha TZS ...... kimerudishwa kwenye akaunti yako inayoishia na .....
NMB karibu yako.

Hilo zoezi nilirudia mara 2 na ikafanya hivyo hiyo hadi nikaamua kutolea ATM ya CRDB Mwanamboka.
 
Nenda uitoe halafu uiache utajua inakuwaje
 
Hapo basi cash ilikuwa hazijatoka labda ndio ikakupa msg hiyo.
 
Scenarios 2 tofauti! Mwache mleta mada aende kwenye ATM atoe hela halafu aziache hapo halo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…