Hivi Ulaya kuna utaratibu wa kuulizwa jina la balozi wa mtaa/mtendaji kata, diwani au mbunge ili kuthibitisha kama ni mkazi wa sehemu husika?

Hivi Ulaya kuna utaratibu wa kuulizwa jina la balozi wa mtaa/mtendaji kata, diwani au mbunge ili kuthibitisha kama ni mkazi wa sehemu husika?

Nikiwa narudi zangu ghetto imebidi nipite shortcut bahati mbaya nimekosea njia nakujikuta napita njia ya kwenda uhani kwa mtu sio mzuri kwenye vichochoro vya mjini sasa wahusika wakaanza kuwa na mashaka na mimi.

Wakaniweka mtu kati nakuanza kuniuliza maswali with confidence nikawaelezea kuwa naelekea nyumbani ila bahati mbaya nimekosea njia.

Wakaanza kuniuliza balozi wako anaitwa nani? kimsingi sio kwa ubaya licha ya kuishi huu mtaa simjui balozi, mtendaji wala diwani. wakanituhumu kuwa mimi nitakuwa mtu mbaya na sio mkazi wa sehemu husika kisa simjui balozi.

Hivi kweli kwa ingia na kutoka ya jiji hili la Dar es salaam jumlisha wingi wa watu pamoja na harakati za kimaisha kuna umuhimu gani wa kuulizana majina ya viongozi wa ngazi za chini?
Nchi za wenzetu mifumo inaonana, sio kama kwetu unaweza ukawa na vitambulisho 10 za mambo mbali mbali kama afya,elimu,kazi,makazi. Huku kwetu tunaishi kwa kasoro za mifumo kutoonana, mfano kipengele tu cha uthibitisho wa makazi yako mpaka balozi athibitishe unaishi eneo lake la utawala, binafsi nimeishi london, uk sijawahi kusikia habari ya balozi wala mtendaji/mwenyekiti, ila wabunge ndio wapo
 
Ulaya ni Ulaya Afrika ni Afrika siyo vyote vya Ulaya vinafaa Afrika na si kila vya Afrika vinafaa Ulaya. Tz jirani akifiwa ni msiba mkubwa wa Mtaa ila Ulaya ni biashara kwa kampuni Ulaya ukifirwa ni jambo la kawaida ila Tz utazomewa kila kichochoro.
Hii Tz utake usitake lazima tukujue kwa undani kwa asili ndipo upelelezi ndipo Ulipozaliwa. Tupo zetu kitaa ikifika usiku huingii mtaani kama hujulikani maana utahojiwa na sungusungu mpaka asili ya ukoo wako wakishindwa kukujua wanaita Njagu .Kwa ufupi ndiyo Usalama wetu
Alijichanganya jamaa mmoja akahamia mtaani akiwa anamiliki shoga yaani Nyumba ilizungukwa na Wanamtaa na kuanza kushambuliwa na mawe Mpaka walipokuja manjagu kuwanusuru.

Hii ndiyo raha ya Tz.
Mtaa gani huo..? Ambao mnajua wafirwaji na wafilaji??
 
Pole sana; maswali ya kipumbavu sana kuulizwa dunia ya leo. Frankly speaking, sijawahi hata kujua majina ya hao watu mtaani ninakoishi!
Siku litakukuta jambo hao wote utawajua na utawaomba msaada na wakuringie kukufahamu....lilinikuta jambo 2018 sio la kusahau nlijua kule juu wanamaliza kila kitu nlirudi kuwatafuta mjumbe, m/kiti wa mtaa ndo mambo mengine yaliendelea
 
Mkuu, si kweli usemayo kwamba wazungu wanaweza kukuua endapo wakosea kupita kwenye kitaa chao kwani mambo hayo yalikuwepo zamani lakini siku hizi yapotea sana.

Isipokuwa ipo mitaa ya wazungu halisi yaani wale wasopenda wageni ambao huwaita "strangers" mingi ina mifumo ya CCTV nje ya nyumba zao na pia kitaa wana mfumo wauita "neighbourhood watch"

Mara nyingi huamua kukufualitia na kupigiana simu kwa kutumia mfumo wa "neighbourhood watch"ili kufahamu ni nyumba ipi waingia.

Wakikuona waishia kwingine hukuacha lakini wakikuona siku ya pili na ya tatu basi hupiga tu simu polisi ambao ndo wenye mamlaka ya kukusimamisha na kuuuliza ID yako na kufahamu una malengo gani na kitaa kile.
Nilikuwa nakumbukia yule jamaa mweusi ( Ahmaud Arbery) aliyeuwawa marekani akifanya mazoezi na wazungu watatu waliomfukuzia kwa gari.
 
Hakuna mahusiano ,kati ya wingi wa watu na movement

Acheni mazoea ,serikali sio wehu wanasema mikataba ya upangaji itolewe na ofisi ya mtaa,Ili kukidhi vigezo vya UTAMBUZi ,kama hivyo ,utafilwa siku nyingine

Imagine ,choo hicho pangekuwa na mke wa mtu anakojoa huko au anaoga ,kelele yake hiyo ndg yangu wangekumeza
 
Acheni mazoea ,serikali sio wehu wanasema mikataba ya upangaji itolewe na ofisi ya mtaa,Ili kukidhi vigezo vya UTAMBUZi ,kama hivyo ,utafilwa siku nyingine,........
Huo sio uungwana kutumia lugha ya matusi...........kama huwezi kuheshimu watu....jiheshimu mwenyewe itakusaidia maishani.
 
Nikiwa narudi zangu ghetto imebidi nipite shortcut bahati mbaya nimekosea njia nakujikuta napita njia ya kwenda uhani kwa mtu sio mzuri kwenye vichochoro vya mjini sasa wahusika wakaanza kuwa na mashaka na mimi.

Wakaniweka mtu kati nakuanza kuniuliza maswali with confidence nikawaelezea kuwa naelekea nyumbani ila bahati mbaya nimekosea njia.

Wakaanza kuniuliza balozi wako anaitwa nani? kimsingi sio kwa ubaya licha ya kuishi huu mtaa simjui balozi, mtendaji wala diwani. wakanituhumu kuwa mimi nitakuwa mtu mbaya na sio mkazi wa sehemu husika kisa simjui balozi.

Hivi kweli kwa ingia na kutoka ya jiji hili la Dar es salaam jumlisha wingi wa watu pamoja na harakati za kimaisha kuna umuhimu gani wa kuulizana majina ya viongozi wa ngazi za chini?
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Ulaya kuna vichochoro Uwani kwa watu?

Una bahati kweli, bora hao wamekuuliza balozi wako n.k, Ulaya ukatishe uwani wa mtu wala haulizwi umetokea wapi, wewe ungepigwa risasi tu.
 
Au mbwa huwa yuko maeneo hayo ya uwani au back garden.
BabaMorgan kazengua tu. Hata hizo tabia za kukatisha kitaa sio kivile huko Ulaya, na isitoshe ukionekana ni mweusi ndio kabisa, lazima uitiwe polisi, yani kuna mitaa ulaya hutembei tembei kwa Uhuru kama huku kwetu. Ana bahati kweli na ashukuru mungu wake.
 
Acheni mazoea ,serikali sio wehu wanasema mikataba ya upangaji itolewe na ofisi ya mtaa,Ili kukidhi vigezo vya UTAMBUZi ,kama hivyo ,utafilwa siku nyingine,........
Huo sio uungwana kutumia lugha ya matusi...........kama huwezi kuheshimu watu....jiheshimu mwenyewe itakusaidia maishani.
Haya ,kuwa makini usije ingiliwa kinyume na uumbwaji
 
BabaMorgan kazengua tu. Hata hizo tabia za kukatisha kitaa sio kivile huko Ulaya, na isitoshe ukionekana ni mweusi ndio kabisa, lazima uitiwe polisi, yani kuna mitaa ulaya hutembei tembei kwa Uhuru kama huku kwetu. Ana bahati kweli na ashukuru mungu wake.
Kuna jamaa yangu mmoja yeye zamani alikuwa apiga kazi ya cleaning kwenye baa moja hivi ya kibabe hujaza sana watu yaani huchukua kama 60k a night na ipo kwenye eneo la wazungu wale khasa wale.

Sasa akawa apangua viti atoe nje ili aweze kupiga deki (mopping) na mambo mengine hivyo ni lazima atoe nje kwanza.

Kumbe siku ile wazungu walikuwa wakipita pale nje ya baa ile na walipomwona mtu mweusi atoa viti nje wakaita polisi kwamba kuna mwizi amevunja baa ile na atoa viti nje.

Zilikuja kama 5 Polisi vans na polisi na mbwa na pona yake jamaa ni kwamba walimkuta apiga mop na walipomuuliza masuali mawili matatu wakamwacha apige kazi.

Hivyo kuna sehemu au vitaa wazungu wakimwona mtu mweusi ni shida sana kwao.
 
Back
Top Bottom