clemsha789
Senior Member
- Jul 1, 2023
- 198
- 335
Nchi za wenzetu mifumo inaonana, sio kama kwetu unaweza ukawa na vitambulisho 10 za mambo mbali mbali kama afya,elimu,kazi,makazi. Huku kwetu tunaishi kwa kasoro za mifumo kutoonana, mfano kipengele tu cha uthibitisho wa makazi yako mpaka balozi athibitishe unaishi eneo lake la utawala, binafsi nimeishi london, uk sijawahi kusikia habari ya balozi wala mtendaji/mwenyekiti, ila wabunge ndio wapoNikiwa narudi zangu ghetto imebidi nipite shortcut bahati mbaya nimekosea njia nakujikuta napita njia ya kwenda uhani kwa mtu sio mzuri kwenye vichochoro vya mjini sasa wahusika wakaanza kuwa na mashaka na mimi.
Wakaniweka mtu kati nakuanza kuniuliza maswali with confidence nikawaelezea kuwa naelekea nyumbani ila bahati mbaya nimekosea njia.
Wakaanza kuniuliza balozi wako anaitwa nani? kimsingi sio kwa ubaya licha ya kuishi huu mtaa simjui balozi, mtendaji wala diwani. wakanituhumu kuwa mimi nitakuwa mtu mbaya na sio mkazi wa sehemu husika kisa simjui balozi.
Hivi kweli kwa ingia na kutoka ya jiji hili la Dar es salaam jumlisha wingi wa watu pamoja na harakati za kimaisha kuna umuhimu gani wa kuulizana majina ya viongozi wa ngazi za chini?