hapo ni wazungu na waarabu mkuu wameleta hizo imani
Kwa upande wa walioleta imani hapa Afrika, nakubaliana na wewe mkuu kuwa waarab na wazungu walituletea imani zao ili waweze kutimiza malengo yao. Na kweli wali/wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza kile walichokitaka.
zinazosababisha watu wanaamini hamasi kuua wayahudi ni thawabu au wayahudi kuua waarabu ni baraka it goes both ways brethren
Hapa kwa Hamas kuua wayahudi ili kupata thawabu au wayahudi kuua waarab ili wapate baraka sio kweli.
Huenda umeandika kwa kutokujua au kutofuata uhalisia wa kile kinachoendelea pale Mashariki ya kati.
Ukweli ni kwamba kile kinachoendelea pale ni vita ya mkandamizaji (Israel) na mkandamizwaji (Palestina)
WAKANDAMIZWAJI ni wapalestina ambao ni mchanganyiko wa waarab, hayahudi na race zingine kidogo (sina uhakika kama unafahamu kuwa katika palestina kuna wayahudi ambao ni wapalestina) ila wapo wengi tu mpaka leo.
WAKANDAMIZAJI ni waisrael ambao ni mchanganyiko wa wazungu, wayahudi na waarab (sina uhakika pia kama unafahamu kuwa israel kuna waarab ambao ni waisrael, wazungu, waethiopia nk)
Waisrael ambao asilimia kubwa ya waliopo katika uongozi ni wazungu, wamekuwa wakianzisha operation za mara kwa mara kama vile kuvamia maeneo ambayo kimataifa tayari yanajulikana kuwa ni ya wapalestina, kuwatoa watu katika nyumba zao, kuwaua, kuwatesa, kuwafungulia kesi zisizoisha na kuwafunga bila sababu za msingi, kuwakatia umeme, maji na kuhakikisha hakuna huduma zozote za msingi ambazo wanapata hao wapalestina wanaovamiwa.
Wapalestina ambao wengi wao ni waarab, baada ya kuona wananyang'anywa nyumba zao, maeneo yao, wanafungwa, wanateswa na kuuwawa bila hatia huku wakiendelea kunyimwa uhuru wa kujitawala. Sasa wakaamua kutengeneza makundi ya kupambana na wale wanaotumia nguvu (Israel) kuua babu zao, bibi zao, baba zao, mama zao, wajomba zao, shangazi zao, ndugu zao nk. Hiki kinachofanywa na Hamas kimeshafanywa na watu wengi hapa duniani.
Ukichunguza watu ambao wameingia katika makundi ya waasi kupambana na serikali utakuta kuwa ni wale ambao walinyimwa haki zao za msingi na serikali yao, na wengine unakuta ndugu zao na wazazi wao waliuwawa katika operation zilizofanywa na serikali hali iliyopelekea watoto wao kuamua kujiunga na waasi ili kutetea haki zao za kuuwawa kwa wazazi wao au kunyimwa kabisa haki zao. Hivyo kusema kuwa Hamas wanapigana kwa sababu ya dini yao ni uongo. Kama ingekuwa ni hivyo basi nchi za kikristo kama vile SA, Hispania, Malta na nyinginezo zisingepambana kuwasaidia. Hata huko Marekani kuna wakristo wengi tena wazungu wameshasimama sana kupinga utawala wa kimabavu wa kiisrael pale Mashariki ya kati.
Hizo nchi zinapambana kuwasaidia maana wanajua fika kuwa wapalestina wanapigania ardhi yao na uhuru wao. Ingekuwa ni swala la dini basi wangeziachia Saudi Arabia, Jordan, na nchi zingine za kiarab ziwapiganie.
Pia ingekuwa wayahudi wanaua waarab ili wapate baraka sio kweli, ingekua hivyo basi wasingekuwa wanaua mpaka waandishi wa habari wa kizungu na wafanyakazi wa misaada wazungu kutoka nchi za Ulaya na Marekani kwenyewe.