Hivi umeshawahi kukutana na mwanamke mwenye kigugumizi?

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
Wakuu,
Habari za muda huu......, nyie wapenda shikamoo hamlambi shikamoo yangu hata kwa dawa...

Nisikuchosheni,

Kuna kitu kidogo tu napenda tujadili kidogo... hivi wewe umeshawahi kukutana na mwanamke mwenye kigugumizi? Katika maisha yangu yote niliyoishi (sijala chumvi nyingi, ni kama pakiti tatu na nusu tu hivi) sijawahi kukutana na mwanamke mwenye kigugumizi.

Mimi kama mwanaume mwenye kigugumizi napata hasira kuona hadi sasa sijawahi kukutana na mwanamke mwenye kigugumizi.

Kwa nini tuteseke sisi tu?

Hivi kweli kuna wanawake kwenye kigugumizi kweli?

Wanafananaje?

Uzi tayari...
 
Nawafahamu wawili wanavyo, ila ni vyakawaida, sio vikali sana.

1. Kimemfanya anaongea haraka, sometimes haeleweki.

2. Kimemfanya anaongea taratibu. Maskini mdogoangu,
anaweza ongea af akanyamaza ghafla ukadhani kamaliza,
ukianza kuongea nae anarudi ulingoni. Huyu hafanyi
kukwama kwama kwa maneno, pumzi inakwamia kifuani
kabla hajayasema, so kikimshika anakua kimya kabisa
kwa sekunde kadhaa.
 
Duh, kigugumizi kinatesa sana....kuna huyo mwamba hadi apige kitu ndo aongee...kwa hiyo akiwa anaongea unakaa nae mbali kidogo, la sivyo utakula mabanzi ya maana....
 
Mi nazani kigugumizi kupona ni Mungu tuu, Europe and Usa wana the best speech therapists lakini bado watu wa vigugumizi wapo kibao tuu.
ila ukimuwahi akiwa mtoto inakuwa rahisi zaidi..
vigugumizi vingi bongo huwa ni ile watoto wanaona fasheni wanaanza kuigana mwishowe inakuwa tabia
 
ila ukimuwahi akiwa mtoto inakuwa rahisi zaidi..
vigugumizi vingi bongo huwa ni ile watoto wanaona fasheni wanaanza kuigana mwishowe inakuwa tabia
Yes ni kweli kabisa kuna vingine ukiwahi ukiwa mtoto unapona. Sema hua utaratibu bongo hatuna.
 
Dah bongo bana....yani unafurahia matatizo ya mwenzako.

ndomana umeme ukikatika mnachunguli kama na kwa jirani haupo halafu kama haupo mnafurahi na kuridhika kabisa
Ni utani tu mkuu...by the way hatuchekani sote ni walewale....

Ila hapo kwenye umeme uko shihi kabisa...πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…