Carleen
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 7,982
- 27,272
Amen, T.G.I.F, wale wenzangu na Mimi wapenda weekend tunaijua ile feeling ya Ijumaa,
Natumaini mpo salama, nimejikuta najiuliza hichi kitu maana ni situation ambayo nimekutana nayo sana kwa watu wengi, kuna ile namna unahisi kabisa kwamba kwenye familia yetu yenye watoto kadhaa, kuna kipenzi cha Baba na pia kuna kipenzi cha Mama, na kuna wale wanabaki wanajua kabisa Mimi siye miongoni mwao..!
Nilikuwa nazungumza na mtu wangu wa karibu siku moja, akanitamkia like 'I was not their best'...! yaani hapo si kwa Baba wala Mama, nilijiskia vibaya mno mno, na hakika ukitazama watoto waliokosa upendo wa hivyo kwa kushuhudia kabisa kuwa wenzie wanakirimiwa kuwaliko kuna namna hawako sawa kabisa kabisa tofauti na yule mtoto aliyepokea upendo wa kumtosha na kumjaziliza..!
Bado sijakuwa mzazi I don't even know how it feels, hivyo natamani nijue, unapenda watoto wote ni kweli lakini kuna yule ambaye anagusa kabisa mtima wako moja kwa moja (nimeongea na wazazi wengi na wamekiri hili), hivi hakuna namna unaweza ficha hili wenzie wasijue na wakajiskia vibaya.?
Ama umewahi pitia ile hali katika ukuaji wako ya kujua wewe ndiye unapendelewa zaidi ama ni kinyume na hapo kuliko wenzio, na ulijiskiaje.??
Natamani wajuzi wa malezi na wazazi waliweke hili sawa ili tujifunze, maana kuna kizazi chenye watu wenye tabia za ajabu sana kinazidi kutengenezwa hivi sasa na hakuna anayewaza kuhusu hili kabisa..! Kuna watu unaweza walaumu kwa tabia wanazokuonyesha ukaishia kuwalaumu na kuwachukia kumbe ni MALEZI yao tu maskiini ndiyo yamewafikisha walipo..!!
Anyways Karibuni..!