Hivi umewahi kuhisi kuna upendeleo wa baadhi ya watoto kwenye familia yenu?

Hivi umewahi kuhisi kuna upendeleo wa baadhi ya watoto kwenye familia yenu?

Yes it happens; you love all your kids, but you like one the most

1. Single parenting; kuna wale wazazi ambao walijikuta wanalea mtoto peke yao kwa sababu moja au nyingine; automatically mapenzi yao yanakuwa makubwa sana na huyo mtoto kuliko watoto wengine atakaowalea na mwenzie. Mtoto anaumwa, anaumia, kila function upo wewe tu; maisha yenu revolve around each other; automatically upendo utaegemea sana kwao. Ingawa kuna wengine ile chuki juu ya mzazi mwenzie aliyemuacha labda, na uchungu wa kumlea mtoto peke yake; anahamishia uchungu wote kwa mtoto, aisee mtoto atateseka hadi ajiulize kama huyu ni mzazi wangu kweli.

2. Mazingira ya kutungwa mimba, kuilea hadi kujifungua na malezi kwa ujumla. Mzazi/Couple ambayo imehangaika sana kutafuta mtoto afu ikaja kufanikiwa kumpata mtoto baada ya struggles nyingi; upendo kwa huyo mtoto wa kwanza utakuwa ni mkubwa zaidi.

-Kuna wale unakuta wakati mama ana mimba labda ikawa inamsumbua sana, kakaa bed rest, sijui kajifungua ikabidi wabaki months hospitalini na mtoto; hako katoto kanatokea kupendwa zaidi ya wenzie

-Mtoto mgonjwa au anayehitaji special need, anachukua nafasi na muda wa wenzie zaidi. Ndiyo maana kuna baadhi ya wazazi/familia, wanaamuaga kutoongeza watoto wengine ili wampe attention yote yule mwenye special need.

3. Kuna watoto ambao wanapendeka kirahisi zaidi. Mtoto mwingine akishakusalimia amemaliza, huyo anaenda kucheza; wakati mtoto mwingine akishakuona tu kashakukimbilia, mara kakuletea hiki na kile, mara kakufanyia hivi, mara kaja kukaa mkapiga story; yaani anakuonyesha upendo hadi basi. Mtoto wa hivi automatically atakuwa anapendwa zaidi na wenzie. Kuna ka-niece kangu kenyewe hakana habari na mtu yoyite zaidi ya kaka yake; hata akilia haiti mama au baba, anaita tu kaka

4. Mtoto anaye-share/serve interest za mzazi;mzazi anajikuta anampenda mtoto huyo zaidi. Mfano kuna watoto wazito na watoto wepesi wa kazi; kukiwa na kikazi tu huyo ashanyanyuka kusaidia. Mzazi anajikuta yupo karibu na huyo mwepesi zaidi. Labda mzazi anapenda kitu fulani na mtoto anakipenda pia, automatically hawa wawili wanaconnect zadi

5. Last borns wengi wanapendwa zaidi.

6. Mtoto ambaye ni wa jinsia ya pekee kwenye familia yao; mara nyingi anakuwa kipenzi cha wazazi hata na wenzie. Mfano ukute familia ambayo mtoto wa kike ni mmoja tu; huyo anakuwa kipenzi zaidi na roho ya baba yake; wa kiume wa pekee ni pumzi ya mama yake.

7. Watoto wanaopewa majina ya kurithi ya bibi/babu/kipenzi cha mzazi. Ule upendo alionao mzazi kwa yule mwenye jina, huwa unahamishiwa kwa mtoto aliyerithi jina hilo.

N:B Ingawa kupendelea mtoto ni kama kitu kisichozuilika; inabidi wazazi tuwe makini sana. Huwa inaleta chuki na madaraja kwa watoto as wale wengine wanaona kama wenyewe hawapendwi; au wengine wanajikuta wana inferiority complex; anajihisi si bora kuliko yule anayependwa zaidi. Ingawa wazazi huwa tunajitetea sana like "sio kweli, tunawapenda wote sawa".

Changamoto niliyoi-notice haswa kwa baadhi ya wamama; ni pale ambapo favorite child wa baba anakuwa si mtoto wa mama wa kumzaa (mtoto wa nje wa mume). Huo moto utakaochochewa kati ya watoto wa nje na wa ndani mmh. Au huyo mtoto akiwa ndiyo mtoto pekee wa baba; hali ndiyo inakuwa tete zaidi . Mungu anatuona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi kudeka tu
Mimi ni litoto la mwisho na nilipendelewa kwa kila kitu. Kunyonya kwenyewe nilinyonya mpaka nikiwa na miaka saba yaani niko nachunga ndama na akili zangu kabisa lakini kichwani napiga akili kuwa nikifika tu home napata lishe ya uhakika kutoka kwa maza. Nakumbuka kulikuwa na mzee mmoja mkorofi sana alikuja pale home ndo akachimba mkwara eti hili litoto mtakuja kuliharibu hili (shwaini zake!). Na kuanzia siku ile ndo nikapotezea kunyonya. Mpaka mama amekuja kuzeeka mpaka kufariki tuko marafiki sana. Imagine anakata roho mi niko mbali lakini niko naye kwenye simu ananiaga.

Hali hii nadhani mwenyewe imeniathiri kiasi fulani (tender heart, huruma sana, kutokuwa na kifua; na mengine mengi tu) ila pia sikujua lakini baadhi ya ndugu zangu hasa wale wawili ninaowafuata wana reservations na mimi na hatuko karibu kivile no matter how hard I try. Wanasema everything came easy for me kwa vile nilikuwa mtoto mpendwa wa familia. Kwa wanangu najitahidi sana kuwa fair japo kuna katoto kamoja yaani nakapenda mpaka basi. Mungu na Atusaidie wazazi tusilete madhara na kupanda mbegu za uhasama; na hata kuacha makovu ya kudumu kwa malaika hawa tuliobarikiwa nao - hasa katika kizazi hiki cha kisasa [emoji1545][emoji1545][emoji1545].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna upendeleo wa kuwa first born au last born. Kuna upendeleo wa kufanana na Baba/Mama. Kuna upendeleo wa kitabia kuwa msikivu, msafi, kufanya vizuri shuleni, kusaidia kazi mbali mbali za nyumbani, kuwa na heshima na adabu si nyumbani tu bali hata kwa majirani na shuleni pia. Hivyo mtoto kama huyu anakuwa hana usumbufu wowote kwa Wazazi wake pale mtaani au shuleni ukilinganisha labda na ndugu zake au watoto wa majirani. Hivyo unakuta Wazazi wanampenda sana huyu japo wanaweza kuwa hawaonyeshi wazi wazi.

Amen, T.G.I.F, wale wenzangu na Mimi wapenda weekend tunaijua ile feeling ya Ijumaa,

Natumaini mpo salama, nimejikuta najiuliza hichi kitu maana ni situation ambayo nimekutana nayo sana kwa watu wengi, kuna ile namna unahisi kabisa kwamba kwenye familia yetu yenye watoto kadhaa, kuna kipenzi cha Baba na pia kuna kipenzi cha Mama, na kuna wale wanabaki wanajua kabisa Mimi siye miongoni mwao..!

Nilikuwa nazungumza na mtu wangu wa karibu siku moja, akanitamkia like 'I was not their best'...! yaani hapo si kwa Baba wala Mama, nilijiskia vibaya mno mno, na hakika ukitazama watoto waliokosa upendo wa hivyo kwa kushuhudia kabisa kuwa wenzie wanakirimiwa kuwaliko kuna namna hawako sawa kabisa kabisa tofauti na yule mtoto aliyepokea upendo wa kumtosha na kumjaziliza..!

Bado sijakuwa mzazi I don't even know how it feels, hivyo natamani nijue, unapenda watoto wote ni kweli lakini kuna yule ambaye anagusa kabisa mtima wako moja kwa moja (nimeongea na wazazi wengi na wamekiri hili), hivi hakuna namna unaweza ficha hili wenzie wasijue na wakajiskia vibaya.?

Ama umewahi pitia ile hali katika ukuaji wako ya kujua wewe ndiye unapendelewa zaidi ama ni kinyume na hapo kuliko wenzio, na ulijiskiaje.??

Natamani wajuzi wa malezi na wazazi waliweke hili sawa ili tujifunze, maana kuna kizazi chenye watu wenye tabia za ajabu sana kinazidi kutengenezwa hivi sasa na hakuna anayewaza kuhusu hili kabisa..! Kuna watu unaweza walaumu kwa tabia wanazokuonyesha ukaishia kuwalaumu na kuwachukia kumbe ni MALEZI yao tu maskiini ndiyo yamewafikisha walipo..!!

Anyways Karibuni..!
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Hili toto dogo lilikuwa nyweeeee nyweeeeee na sasa wamekuwa kidogo. So ikitokea leo hii amelia hata I won't bother much nishazoea naona ni deko tu. Hili ni litubdu, likorofi na ngumi nje ila mwepesi kushtaki.

Hizi lawama akina Mama tunazipataga sana. Sisemi hazipo lakini sometimes ni unfounded kabisa jamani hatuwabagui watoto wetu.

Ila sasa kuna vitu vidogo vidogo vinavyoweza kuleta taswira hii.

Mfano Mimi mtoto wangu mkubwa hakunisumbua kabisa katika malezi pamoja na kuwa sikuwa very experienced. Hata kulia hakuwa mlizi. So sikuzoeaga kabisa sauti yake akilia. Ni mpole by nature na sio mkorofi.

Hili toto dogo lilikuwa nyweeeee nyweeeeee na sasa wamekuwa kidogo. So ikitokea leo hii amelia hata I won't bother much nishazoea naona ni deko tu. Hili ni litubdu, likorofi na ngumi nje ila mwepesi kushtaki.

Lakini mkubwa akilia wallah it drives me crazy. I hate the sight of tears on my sons face. I hate to the core the sound of my elder son crying na ni mwepesi sana kureact sababu nahisi ameonewa na hapo ndo utaona familia zetu za kiafrika zikisema unampemdelea mtoto mmoja 🙄🙄🙄🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️
 
Ukweli ni kwamba hakuna mzazi anayependa Watoto wote wapo watoto kadhaa lazima awapende zaidi. Upendo haugawanyiki wapo utakaowapenda kwakua ni uzazi wako na wapo utawapenda zaid, nitatoa mifano.
-Bibi yangu.
Katika watoto waote 11 mtoto mmoja tu ndio anapendwa zaidi kuliko hata sisi wajukuu hatupendwi kama huyo bamdogo apendavyo. Hivi ukipika uji nani wa kupewa sufuria alambe kama sio mtoto mdogo ila siku hiyo bibi alimpatia mwanae huyo sufuria la uji alambe wakati bamdogo nae ana mtoto mdogo.

-Mimi mwenyewe
Katika wadogo zangu yupo mmoja wa kike ndio roho yangu. Inawezekana ndio binaadamu namba moja ninaempenda zaid kwa ajili yake niko tayari kumfanyia lolote na vile napenda Watoto wa kike hafu kwetu hamna kizazi cha watoto wa kike,picha yake Ndio wallpaper yangu kwenye simu😎😎

-Mungu
Tunaambiwa Mungu hana Upendeleo ni kweli ila kuna viumbe Mungu anawapenda zaidi.
1. Yesu ndio kiumbe namba moja kuliko kiumbe chochote mbele za Mungu.
2. Kwa binaadamu Daudi ndio Mwanadamu aliyependwa na anayependwa na Mungu kuliko mtu yoyote katika hiatoria ya ulimwengu. Zamani ulikua hata ukiongopa hapo hapo unakufa ila Daudi alikua anachezea sharubu za Mungu awezavyo. Kaua watu wengi, kaiba wake za watu wengi, Kasema uongo sana na madhambi mengine kibao
Ila adhabu pekee aliyopewa ni kutokumjengea Mungu Hekalu, sasa hiyo ni adhabu au alipunguziwa usumbufu.
 
Sina mtoto wala nini ila Kuna watoto wa ndugu zangu ila nampenda mtoto mmoja sana kuliko wengine and I Feel we share some kind of bond, na yeye hunipenda hivo hivo, so same na wazazi wanapenda watoto wote ila Kuna wanaowapenda zaidi kuliko wengine I think sio dhambi hutokea tu hyo Hali hata kwenye bible ukisoma jinsi Esau na mdogo wake kila mtu alipendwa mwingine na baba mwingine na mama.
I think kwangu sio dhambi hutokea tu damu kuendana Ile deep waswahili husema
Siyo kwa Essau na Yakobo tu ambapo Essau alipendwa na baba, Yakobo akapendwa na mama.

Hata kwa Kaini na Habili... (Habili alipendwa zaidi na Mungu).

Umenivutia sana kwamba at least you know the Bible halafu umesema huna mtoto, vipi kuolewa au kuwa na mchumba?[emoji3]
 
Mambo ya kupendwa au kutokupendwa huwa siyajali,siamini kama kuna mtu ananipenda hata atake kunidhibitishia vipi.
 
Amen, T.G.I.F, wale wenzangu na Mimi wapenda weekend tunaijua ile feeling ya Ijumaa,

Natumaini mpo salama, nimejikuta najiuliza hichi kitu maana ni situation ambayo nimekutana nayo sana kwa watu wengi, kuna ile namna unahisi kabisa kwamba kwenye familia yetu yenye watoto kadhaa, kuna kipenzi cha Baba na pia kuna kipenzi cha Mama, na kuna wale wanabaki wanajua kabisa Mimi siye miongoni mwao..!

Nilikuwa nazungumza na mtu wangu wa karibu siku moja, akanitamkia like 'I was not their best'...! yaani hapo si kwa Baba wala Mama, nilijiskia vibaya mno mno, na hakika ukitazama watoto waliokosa upendo wa hivyo kwa kushuhudia kabisa kuwa wenzie wanakirimiwa kuwaliko kuna namna hawako sawa kabisa kabisa tofauti na yule mtoto aliyepokea upendo wa kumtosha na kumjaziliza..!

Bado sijakuwa mzazi I don't even know how it feels, hivyo natamani nijue, unapenda watoto wote ni kweli lakini kuna yule ambaye anagusa kabisa mtima wako moja kwa moja (nimeongea na wazazi wengi na wamekiri hili), hivi hakuna namna unaweza ficha hili wenzie wasijue na wakajiskia vibaya.?

Ama umewahi pitia ile hali katika ukuaji wako ya kujua wewe ndiye unapendelewa zaidi ama ni kinyume na hapo kuliko wenzio, na ulijiskiaje.??

Natamani wajuzi wa malezi na wazazi waliweke hili sawa ili tujifunze, maana kuna kizazi chenye watu wenye tabia za ajabu sana kinazidi kutengenezwa hivi sasa na hakuna anayewaza kuhusu hili kabisa..! Kuna watu unaweza walaumu kwa tabia wanazokuonyesha ukaishia kuwalaumu na kuwachukia kumbe ni MALEZI yao tu maskiini ndiyo yamewafikisha walipo..!!

Anyways Karibuni..!
Nafanya kila kitu kwa wazazi wangu lakini mama hanikubali kabisa na mimi ndie pekee nina mwekekeo na ni last born. Kidogo mzee alikua hana shida before hajatangulia mbele ya haki, Allah amrehemu.

Kuna mabro chenga, lakin ndio kila kitu. Nikihoji chochote juu ya kutowajibika na kukaa tu pale home kusubiri mim niweke mambo sawa, mama anachukia na sipendi awe anajisikia vibaya.

Licha ya kujitahdi kupambana kwa ajili ya faimilia pale ambapo nitakua sina response nnayoipata ukiwa huna kifua unaweza kulia.

Sijali na wala siwaonyeshi kwamba nahisi hivyo. I'm taking care of them at my best ili kupata baraka za Muumba. Mapenzi ya mtu/mzazi ni hisia binafsi na huwezi lazimisha mpendwe sawa. Maisha yanaendelea.
 
Mimi last born kwenye familia yetu , upendeleo nimepata lkn si ule wa kubagua wengine kwasababu ya ule mtoto wa mwisho hata Kaka zangu na dada zangu walikuwa wananipenda vile vile

mzee alisema yeye hataki kulaumiwa na mtoto yeyote Kama elimu wote nitahakikisha mnasoma na kweli mzee katusomesha watoto wake wote hadi elimu ya dini isipokuwa dada yetu wa kwanza yy alikataaga kusoma alimwambia anataka kuolewa .

Na kitu ambocho nimegundua katika watoto sita wa mzee mm ndio nilikuwa mtoto mtulivu tofauti na ndungu zangu wao walivyokuwa wadogo walikuwa watukutu ,walipiga watoto wenzao kwhy zile shuruba za kipigo kwa mzee sikuzipata hata mabrother walikuwa hawanipigi bali ilikuwa ukinigusa umelikoroga.

Changamoto niliyoipata walikuwa wananichukulia mtoto muda wote hata nilivyo fika 19-20 walini treat Kama bado mtoto😆😆 .
 
Amen, T.G.I.F, wale wenzangu na Mimi wapenda weekend tunaijua ile feeling ya Ijumaa,

Natumaini mpo salama, nimejikuta najiuliza hichi kitu maana ni situation ambayo nimekutana nayo sana kwa watu wengi, kuna ile namna unahisi kabisa kwamba kwenye familia yetu yenye watoto kadhaa, kuna kipenzi cha Baba na pia kuna kipenzi cha Mama, na kuna wale wanabaki wanajua kabisa Mimi siye miongoni mwao..!

Nilikuwa nazungumza na mtu wangu wa karibu siku moja, akanitamkia like 'I was not their best'...! yaani hapo si kwa Baba wala Mama, nilijiskia vibaya mno mno, na hakika ukitazama watoto waliokosa upendo wa hivyo kwa kushuhudia kabisa kuwa wenzie wanakirimiwa kuwaliko kuna namna hawako sawa kabisa kabisa tofauti na yule mtoto aliyepokea upendo wa kumtosha na kumjaziliza..!

Bado sijakuwa mzazi I don't even know how it feels, hivyo natamani nijue, unapenda watoto wote ni kweli lakini kuna yule ambaye anagusa kabisa mtima wako moja kwa moja (nimeongea na wazazi wengi na wamekiri hili), hivi hakuna namna unaweza ficha hili wenzie wasijue na wakajiskia vibaya.?

Ama umewahi pitia ile hali katika ukuaji wako ya kujua wewe ndiye unapendelewa zaidi ama ni kinyume na hapo kuliko wenzio, na ulijiskiaje.??

Natamani wajuzi wa malezi na wazazi waliweke hili sawa ili tujifunze, maana kuna kizazi chenye watu wenye tabia za ajabu sana kinazidi kutengenezwa hivi sasa na hakuna anayewaza kuhusu hili kabisa..! Kuna watu unaweza walaumu kwa tabia wanazokuonyesha ukaishia kuwalaumu na kuwachukia kumbe ni MALEZI yao tu maskiini ndiyo yamewafikisha walipo..!!

Anyways Karibuni..!

Mimi kwetu wa mwisho Kati ya saba, hadi Leo Mabro zangu Wana jelasi na Mimi sababu wao walikulia kipindi cha ukata, halafu mie nilikulia maisha matamu sababu Mama alikuwa kwenye Ajira.

Now Nina watoto watatu, ninaempenda zaidi bint yangu wa pili (3yrs), japokuwa siishi nao, tunaonana kwa mwaka Mara moja (likizo),
Sababu ya kumpenda, ni mcheshi sana.
Wa kwanza wa kiume (12yrs) hatuna ushikaji (analijua Hilo) kutokana Tabia ya uchafu uliopitiliza, hapendi kuoga, kuswaki, kufua ni Mzembe Dunia nzima.
Wa mwisho cha kiume bado mdogo (6 mths), sijamfaidi kabisa nilikaa nae week moja wakati katoka kuzaliwa hadi Leo hatujaonana tena.
 
Upendeleo huwa unakuwepo, kuna ule ambao it is obviously tu last born huwa anapendelewa kuliko wenzie, ukiachana na lb huwa kuna mtoto unakuta anakuwa na vitabia vizuri lazma wazazi au mzazi ampendelee....

Mi binafsi sijioni nahisi sina nnaempenda kuliko wenzie, naona nawapenda sawa, ila mwenzangu namuona anaupendo zaidi kwa first born kwa sababu ni mtoto mpole hana utundu.
Basii wanao wana bahati sana kuwa na Mama wa aina yako, maana wengi wanapitia maisha ya upendeleo nje nje maskiini..!!
 
Back
Top Bottom