Hivi umewahi kuhisi kuna upendeleo wa baadhi ya watoto kwenye familia yenu?

Hivi umewahi kuhisi kuna upendeleo wa baadhi ya watoto kwenye familia yenu?

Nashukuru wazazi wangu waliweza kubalance hiyo hali. Tupo wa 4 lkn sijawahi hisi nani anapendwa zaidi. Tumekuwa treated equally kwenye kila kitu.
Now nina Mtoto mmoja tu mapenzi yote yapo kwake.
 
Ukweli ni kwamba hakuna mzazi anayependa Watoto wote wapo watoto kadhaa lazima awapende zaidi. Upendo haugawanyiki wapo utakaowapenda kwakua ni uzazi wako na wapo utawapenda zaid, nitatoa mifano.
-Bibi yangu.
Katika watoto waote 11 mtoto mmoja tu ndio anapendwa zaidi kuliko hata sisi wajukuu hatupendwi kama huyo bamdogo apendavyo. Hivi ukipika uji nani wa kupewa sufuria alambe kama sio mtoto mdogo ila siku hiyo bibi alimpatia mwanae huyo sufuria la uji alambe wakati bamdogo nae ana mtoto mdogo.

-Mimi mwenyewe
Katika wadogo zangu yupo mmoja wa kike ndio roho yangu. Inawezekana ndio binaadamu namba moja ninaempenda zaid kwa ajili yake niko tayari kumfanyia lolote na vile napenda Watoto wa kike hafu kwetu hamna kizazi cha watoto wa kike,picha yake Ndio wallpaper yangu kwenye simu😎😎

-Mungu
Tunaambiwa Mungu hana Upendeleo ni kweli ila kuna viumbe Mungu anawapenda zaidi.
1. Yesu ndio kiumbe namba moja kuliko kiumbe chochote mbele za Mungu.
2. Kwa binaadamu Daudi ndio Mwanadamu aliyependwa na anayependwa na Mungu kuliko mtu yoyote katika hiatoria ya ulimwengu. Zamani ulikua hata ukiongopa hapo hapo unakufa ila Daudi alikua anachezea sharubu za Mungu awezavyo. Kaua watu wengi, kaiba wake za watu wengi, Kasema uongo sana na madhambi mengine kibao
Ila adhabu pekee aliyopewa ni kutokumjengea Mungu Hekalu, sasa hiyo ni adhabu au alipunguziwa usumbufu.
Shukrani sana Da'Vinci kwa mifano hai, ila hapo mwishoni pamenichekesha, enwei, msalimie 'roho yako' I'm praying akuwe smart kama kaka yake..!
 
Nafanya kila kitu kwa wazazi wangu lakini mama hanikubali kabisa na mimi ndie pekee nina mwekekeo na ni last born. Kidogo mzee alikua hana shida before hajatangulia mbele ya haki, Allah amrehemu.

Kuna mabro chenga, lakin ndio kila kitu. Nikihoji chochote juu ya kutowajibika na kukaa tu pale home kusubiri mim niweke mambo sawa, mama anachukia na sipendi awe anajisikia vibaya.

Licha ya kujitahdi kupambana kwa ajili ya faimilia pale ambapo nitakua sina response nnayoipata ukiwa huna kifua unaweza kulia.

Sijali na wala siwaonyeshi kwamba nahisi hivyo. I'm taking care of them at my best ili kupata baraka za Muumba. Mapenzi ya mtu/mzazi ni hisia binafsi na huwezi lazimisha mpendwe sawa. Maisha yanaendelea.
Mungu azidi kukupigania ndugu yangu, akakujaze faraja ya kweli itokayo kwake, hilo nalo litapita, jipe moyo mkuu...!
 
Mimi last born kwenye familia yetu , upendeleo nimepata lkn si ule wa kubagua wengine kwasababu ya ule mtoto wa mwisho hata Kaka zangu na dada zangu walikuwa wananipenda vile vile

mzee alisema yeye hataki kulaumiwa na mtoto yeyote Kama elimu wote nitahakikisha mnasoma na kweli mzee katusomesha watoto wake wote hadi elimu ya dini isipokuwa dada yetu wa kwanza yy alikataaga kusoma alimwambia anataka kuolewa .

Na kitu ambocho nimegundua katika watoto sita wa mzee mm ndio nilikuwa mtoto mtulivu tofauti na ndungu zangu wao walivyokuwa wadogo walikuwa watukutu ,walipiga watoto wenzao kwhy zile shuruba za kipigo kwa mzee sikuzipata hata mabrother walikuwa hawanipigi bali ilikuwa ukinigusa umelikoroga.

Changamoto niliyoipata walikuwa wananichukulia mtoto muda wote hata nilivyo fika 19-20 walini treat Kama bado mtoto😆😆 .
you have to be thankful hata kuipata hiyo nafasi ya kudeka deka, wenzio wanaitamani na hawaipati ujue, Heshima imfikie Baba yako hakika.!
 
Udhaifu mkubwa sana kwa mzazi kuonyesha upendo wa wazi kwa mtoto mmoja na kuwa ignore wengine. My two kids nitahakikisha hakuna atakayejua ni yupi anapendwa zaidi ya mwenzake. I'll balance my love kwao.
A huge Amen to that, na Mungu azidi kukusaidia uendelee kuwa Baba bora kaka mkubwa.!
 
Nashukuru wazazi wangu waliweza kubalance hiyo hali. Tupo wa 4 lkn sijawahi hisi nani anapendwa zaidi. Tumekuwa treated equally kwenye kila kitu.
Now nina Mtoto mmoja tu mapenzi yote yapo kwake.
aaaw'...!
Mshukuru Mungu ulipata wazazi bora kabisa..! I can't imagine kanavyodeka kenyewe..!
 
It differs from one parent to another. Other kids, relatives and neighbours may suspect but without 100% assurance.

Ule upendo huwa haufichiki BAK ujue, mzazi anajikaza weeh' ila anateleza tu na ghafla dunia inajua fav child ni yupi,
 
Honestly mimi ndio my mom favorites hata wadogo zangu wanajua hilo sio kwamba wao hawapati upendo. But me and my mom we have been through a lot, by the time wanazaliwa mambo yapo kwenye reli. Funny thing imefikia hatua wakitaka kitu kwa bi mkubwa wakihisi anaweza kukataa, wanakuja kwangu kwanza wakiamini hua mama hachomoi nikimwambia.
Basii vitoto vinavyojua vinapendwa huwa vinajua kudeka, huwa huvimbi kweli Cvez.??
 
Ukweli ni kwamba hakuna mzazi anayependa Watoto wote wapo watoto kadhaa lazima awapende zaidi. Upendo haugawanyiki wapo utakaowapenda kwakua ni uzazi wako na wapo utawapenda zaid, nitatoa mifano.
-Bibi yangu.
Katika watoto waote 11 mtoto mmoja tu ndio anapendwa zaidi kuliko hata sisi wajukuu hatupendwi kama huyo bamdogo apendavyo. Hivi ukipika uji nani wa kupewa sufuria alambe kama sio mtoto mdogo ila siku hiyo bibi alimpatia mwanae huyo sufuria la uji alambe wakati bamdogo nae ana mtoto mdogo.

-Mimi mwenyewe
Katika wadogo zangu yupo mmoja wa kike ndio roho yangu. Inawezekana ndio binaadamu namba moja ninaempenda zaid kwa ajili yake niko tayari kumfanyia lolote na vile napenda Watoto wa kike hafu kwetu hamna kizazi cha watoto wa kike,picha yake Ndio wallpaper yangu kwenye simu[emoji41][emoji41]

-Mungu
Tunaambiwa Mungu hana Upendeleo ni kweli ila kuna viumbe Mungu anawapenda zaidi.
1. Yesu ndio kiumbe namba moja kuliko kiumbe chochote mbele za Mungu.
2. Kwa binaadamu Daudi ndio Mwanadamu aliyependwa na anayependwa na Mungu kuliko mtu yoyote katika hiatoria ya ulimwengu. Zamani ulikua hata ukiongopa hapo hapo unakufa ila Daudi alikua anachezea sharubu za Mungu awezavyo. Kaua watu wengi, kaiba wake za watu wengi, Kasema uongo sana na madhambi mengine kibao
Ila adhabu pekee aliyopewa ni kutokumjengea Mungu Hekalu, sasa hiyo ni adhabu au alipunguziwa usumbufu.
Ila daudi alipendwa Sana na MUNGU japokuwa alikuwa mtata sana

Na yeye alielewa pia ni jinsi gani MUNGU anampendelea
 
Mimi ni litoto la mwisho na nilipendelewa kwa kila kitu. Kunyonya kwenyewe nilinyonya mpaka nikiwa na miaka saba yaani niko nachunga ndama na akili zangu kabisa lakini kichwani napiga akili kuwa nikifika tu home napata lishe ya uhakika kutoka kwa maza. Nakumbuka kulikuwa na mzee mmoja mkorofi sana alikuja pale home ndo akachimba mkwara eti hili litoto mtakuja kuliharibu hili (shwaini zake!). Na kuanzia siku ile ndo nikapotezea kunyonya. Mpaka mama amekuja kuzeeka mpaka kufariki tuko marafiki sana. Imagine anakata roho mi niko mbali lakini niko naye kwenye simu ananiaga.

Hali hii nadhani mwenyewe imeniathiri kiasi fulani (tender heart, huruma sana, kutokuwa na kifua; na mengine mengi tu) ila pia sikujua lakini baadhi ya ndugu zangu hasa wale wawili ninaowafuata wana reservations na mimi na hatuko karibu kivile no matter how hard I try. Wanasema everything came easy for me kwa vile nilikuwa mtoto mpendwa wa familia. Kwa wanangu najitahidi sana kuwa fair japo kuna katoto kamoja yaani nakapenda mpaka basi. Mungu na Atusaidie wazazi tusilete madhara na kupanda mbegu za uhasama; na hata kuacha makovu ya kudumu kwa malaika hawa tuliobarikiwa nao - hasa katika kizazi hiki cha mabroila [emoji1545][emoji1545][emoji1545].
nisiwe muongo huwa siwezi kuvumilia nikiona mtoto hata wa miaka mitatu kasoro ananyonyeshwa😁😁😁

I imagine ningekuwa ndugu yako ningepata feelings za kukubutua mara ngapi kwa siku

ila pole mkuu kwa kumpoteza mother, Mungu amlaze mahali pema 🙏🙏
 
Hii topic muhimu sana na ina ukweli mwingi tu sema si rahisi sana kuielezea vizuri.
Mie pia ni muathirika wa hii kitu, nilikua karibu sana na Baba kuliko Mama, japo Baba alitupenda wote.

Baada ya yeye kutangulia mbele za haki nikawa nimebaki sina pa kushika.
 
Amen Dear.

It applies to most things in life actually.

Kitu kikiwa common una adapt tu, hakuna maajabu.

Lakini hata unavyo mtaja huyo mtoto wa pili inaonyesha kabisa mambo yake ya kulia lia na utundu yanakukera, unatumia hili toto...litundu...wakati wa kwanza hata kumtaja unachagua kwa umakini herufi za kutumia.
 
Leo niende personal maana mada imenigusa

Kuna kuona mtu flani anapendwa kitu ambacho kwangu ni kawaida ila kuna kubaguliwa

mzazi kukuchukulia kama of low class, yaani ndugu yako yoyote anaona anakumudu maana mkienda kwa mzazi ni nadra kuwa balanced na kukaa upande wako hata kama unaonewa

yaani nilibaguliwa na kuoneshwa LIVE, imagine mpo sebuleni ndugu zako wanaomba hela ya nguo wanapewa bila shaka ila wewe unaomba hela ya masomo ya ziada school tena cheaper mara hata 100 lakini unanyimwa kwa kejeli na ndugu zako wanakucheka

ilikuwa worse than that !!

Ila imenijenga kuwa mtu wa kutopenda misaada kirahisi au vitu vya bure. I fight on my own, kheri nipate buku nisonge ugali nile kuliko kumuomba mtu 100k ambayo anaweza kunipa

Kingine nampenda first born wetu, Alinionesha kunipenda sana na alikuwa karibu kuniprotect. ile Ukinigusa ujiandae kupambana nae na 90% ya kupigana kwake home sababu ni mimi 😂😂😂, Japo ni kivuruge hatari ila kama kuna mtu dunia hii najua ananipenda without a doubt bhasi ni yeye and i love him sana sana sanaaaa

nimeshakuwa emotional ngoja niishie haps 😁
 
ni baraka sana kama amekuja kutulia ukubwani, hivi ninyi hiyo hali haikuwasumbua kabisa.?
Haikusumbua kabisa maana Mimi na last born tukawa kipenzi cha baba,naona Mzee nae aligundua mkewe ana mpenda sana bro.ndio alikuja kutulia saivi katika watoto yeye ndo msomi zaidi na kazi pesa nzuri,wakati alikua ndo mkorofi zaidi ya wote,nunda
 
Back
Top Bottom